Kuwagawia pedi watoto wa shule ya msingi, wamebalehe?

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,977
11,391
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Igombe wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa na nyuso za furaha baada ya kupewa vifaa vya usafi vitakavyowasaidia katika mzunguko wao wa kila mwezi na kuepuka magonjwa mbalimbali yanayotokana na kutumia vifaa visivyo salama. (g sengo)
4.JPG
 
Aisee nadhani wanawasaidia wazazi wao na walimu wao kupitia mgongo wa wanafunzi
 
Haya mambo mengine yanapaswa kufanywa kimya kimya? tumefikia mahali tunaonyeshana hata ......Ugh!
 
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Igombe wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa na nyuso za furaha baada ya kupewa vifaa vya usafi vitakavyowasaidia katika mzunguko wao wa kila mwezi na kuepuka magonjwa mbalimbali yanayotokana na kutumia vifaa visivyo salama. (g sengo)
4.JPG
.....kwa nini kuwapiga picha na huo msaada wakiwa wameuinua juu kwa dalili zote zinazoonyesha kuwa wameelekezwa?...with all respect to our lovable mothers, and sisters, safari yao ya ukombozi kukubaliza ndani ya "afrika ya waafrika huru"bado ni ndefu......aluta continua!
 
Huu in ujinga sana anzia mwll mkuu na uongozi wa shule.
Hv ndivo vitu vinavyoleta magonjwa km festula, UTI n.k still Mtoto anapewa vitu hivo, watz tusiwe wajinga kupita kiasi cha kupitiliza.
 
Mkuu naomba nikuambie kuwa, nilikimbilia kufungua picha, nkachunguza sana wala sikumwona wa kiume bali wote walio inua pedi juu ni wasichana tu. Kwa hivyo naomba nikusahihishe kuwa; Wasichana hawa balehi bali huvunja ungo.
Lakini pia nachukulia ka hili ni kuwadhalilisha tu watoto wetu.
Ndo maana tunasema maadili yanaporomoka kupita kiasi. Pedi jamani zilikuwa ni kituko hata kuiona. Mama zetu walifukia au kutumbukiza choo cha shimo. Leo wadada mnatupa hata kwenye taka ngumu. Ni maajab mapya haya.
Sikuwahi kuiona ya dadangu japo tulikuzana pamoja. Niliona tu maziwa yeshaota lakini hiyo kitu sikuiona. Mola atuepushe na balaa hili. Ati wanasaidiwa wasipatwe na maradhi. Hayo maradhi yameanza leo??
 
Hao watoto n wadogo sana kuwapa hayo mavitu...wanawakomaza tu na kutuharibia watoto....!!
 
Back
Top Bottom