Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

Mbunge akichaguliwa jimboni hawezi fanya kazi za mbunge kabla hajaapishwa kuwa mbunge na hivyo kwakuwa waziri anateuliwa miongoni mwa wabunge, waziri hawezi kuteuliwa na kuanza kazi zq uwaziri kabla ya kuapishwa kiapo cha bunge! Hii tafsiri rahidi na kwamba hivi viapo vinategemeana lazima uvipata vyote na utaweza kutekeleza majukumu yako ya uwaziri maana hiyo kazi ya uwaziri ni kaxi ya bunge maana ni wajibu wa bunge kuisimamia serikali! Sijadoma shetia lakini baada ya kupitia vifungu hivi kwenye katiba na kuangalia practices za nyumba ni wazi hapa katiba imesiginwa!
 
Makelele tu, wacha niongeze castle light, hivi mnadhani magamba wanajali kuvunja ama to honor the constitution!? Wastage of time hapa, haya majamaa sio malofa kiasi hicho mkumbuke aisee, ni sawa kwa maoni yenu mnaona jk kavunja katiba lakini kiukweli haieleweki kwa kuwa hii mihimili inapigana tafu tu. Awe kavunja hajavunja hakuna tofauti, life goes on!
 
Katika Baraza jipya la mawaziri kuna wabunge wapya ambao waliteuliwa na Rais jana na leo kuwa mawaziri. Mawaziri hao ni Prof. Sospeter Muhongo ambaye aliteuliwa na Rais kuwa mbunge jana na leo ametuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Mwingine ni Bi. Saada Mkuya Salum aliyeteuliwa na Rais kuwa mbunge masaa machache kabla ya kuteuliwa tena kuwa Naibu Waziri wa Fedha (huyu tayari ameshabatizwa "Waziri Voda fasta").

Kwa mujibu wa taarifa toka Ikulu uteuzi wao kama wabunge unaanza mara moja. Kikao cha bunge kinatarajiwa kuanza tena Juni mwaka huu ambapo tutategemea wabunge wateule kuapishwa. Hata hivyo, mawaziri wote wapya wanatarajiwa kuapishwa tarehe 7 Mei mwaka huu. Hii inamaanisha kuwa Prof. Sospeter Muhongo na Bi. Saada Mkuya Salum wataapishwa kuwa Waziri na Naibu Waziri kabla ya kuapishwa kuwa wabunge.

Je, inawezekana Waziri au Naibu waziri kuapishwa kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge?

=================================================

Majibu ya Naibu Spika, Job Ndugai:

Hata hivyo taarifa ya Ikulu haikusema wabunge hao wateule wataapishwa lini na wapi, lakini Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alipoulizwa jana alisema alisema kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, mtu yeyote anayeteuliwa kuwa mbunge, ataapishwa katika mkutano wa Bunge unaofuata baada ya uteuzi wake, bila kujali ni mbunge wa kuteuliwa au wa jimbo.

Ndugai alisema kwa msingi huo, wabunge hao wateule wataapishwa wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge la Bajeti unaotarajiwa kuanza mjini Dodoma, Juni 12.

Alipoulizwa itakuwaje ikitokea wateule hao wa Rais wakateuliwa pia kuwa mawaziri na kuendelea na kazi kabla ya kuapishwa kuwa wabunge, Naibu Spika alisema kwa hali ya kawaida, hilo haliwezekani.

?Kwa mujibu wa Katiba, mawaziri watateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, na anakuwa mbunge mteule hadi pale anapoapishwa, na ndiyo maana baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, kazi ya kwanza ya Bunge ni kuchagua Spika na Naibu Spika, ambao baadaye watafanya kazi ya kuwaapisha wabunge, na ndipo atateuliwa Waziri Mkuu na kisha mawaziri,? alifafanua Naibu Spika

Source: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=29712

========================================================

TAARIFA YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KWA VYOMBO VYA HABARI

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri. Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.

Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:

?Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge?

Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.

Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria. Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.

Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.

Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

06 Mei, 2012
Kwa tafsiri yangu, huu ni uvunjaji tuu wa katiba!. Niliuliza swali, JK alipoyasamehe yale majizi ya EPA alitumia kifungu gani?. Hivi rais anayo mamlaka kuizuia sheria isichukue mkondo wake?!.

Katiba inasema rais kwa mashauriano na waziri mkuu atateua mawaziri miongoni mwa wabunge. Mbunge mteule anakuwa mbunge pale tuu baada ya kuapishwa!. Unless hata mbunge mteule ni mbunge kamili hata kabla ya kuapishwa!. What is significance ya kiapo?.

Uteuzi wa wabunge hao wapya umefanyika kwa mujibu wa katiba ila hao ni wabunge wateule tuu!. Kuwateua wabunge wateule kuwa mawaziri pia ni kwa mujibu wa katiba. Kwa tafsiri yangu, rais hawezi kuwaapisha wateule hao kuwa mawaziri kabla hawajaapishwa kuwa wabunge!. Ubunge ni pre-condition ya uwaziri unless we just put the cart before the horse!.

Huo nao ni uvunjaji wa katiba!. Kwa jinsi tulivyojaza wanasheria vilaza, hakuna wa kumshauri rais kuwa mbunge mteule si mbunge mpaka ale kiapo!.

Kama alivyoisamehe ile mijizi ya EPA, hakuna aliemwambia rais kuwa hana mamlaka hayo ya kuizuia sheria kuchukua mkondo wake!. Japo alichukua uamuzi huo kwa kutolikata tawi alilolikalia, kama aliwapenda sana angeacha sheria ichukue mkondo wake halafu kwa mamlaka yake akawasamehe!.

Mamlaka ya rais ni kusamehe wafungwa sio kuisamehe mijizi kabla haijafikishwa mbele ya vyombo vya sheria. Ule ulikuwa uvunjaji wa katiba na akiwaapisha wabunge wateule kuwa mawaziri kabla hawajawa wabunge nao ni uvunjaji wa katiba!.

Pasco.
Kesho kosa hili linajirudia
 
Kesho kosa hili linajirudia
Mkuu umeshaambiwa ibara ya 56 na 68 havitegemeani.
Halafu ni aibu kwa mwanasheria kama wewe kuwaita wanasheria wenzako vilaza.
Ningekuona jasiri sana kama leo ungekimbilia mahakamani kwa hati ya dharura kuomba tafsiri ya vifungu hivyo toka kwa wasomi wenzio kama ilivyofanyika kwenye kesi ya mita 200
 
Matatizo ya kujifunzia sheria JF. Rais alisema anawateua kuwa wabunge mara moja, na kuwateua tena kuwa mawaziri. Nyie kuleni peremende tu humu wenye kazi ndio wanaoteuana. JPM kaza buti. Kama mmekwaza nendeni mkamshitaki si kuna mahakama huko sheria ndio msumeno msumeno.

Je, nini kinafuata baada ya kuteuliwa? Je, wakiteuliwa hawawezi kufanya kazi walizoteuliwa wazifanye? Je, sheria zinasema nini kwa mtu ambaye ameteuliwa na bado kuapishwa hususan mbunge kufanya kazi aliyoteuliwa kufanya. Je, kuna kosa lolote lililofanyika? Kama kosa lipo ni lipi? Je,hakuna kipengele kinachompa madaraka mteuzi kufanya hivyo (ie rais).
 
Kwa Tanzania huu mtindo wa kutafsiri katiba na kanuni kama vile unavyotafsiri sheria za physics kuna siku itatugharimu vibaya. Hii inaonesha ni jinsi gani mamalaka zetu ziko juu ya sheria. Simply mbuge, Diwani na hata Rais hawezi kuwa halali kama hajaapishwa . Hivi hawa wanasheria wa Serikali kina Tulia wamesoma sheria kutoka Vyuo gani? Ama ni style ile ile ya Kivukoni LLB!
 
Katika Baraza jipya la mawaziri kuna wabunge wapya ambao waliteuliwa na Rais jana na leo kuwa mawaziri. Mawaziri hao ni Prof. Sospeter Muhongo ambaye aliteuliwa na Rais kuwa mbunge jana na leo ametuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Mwingine ni Bi. Saada Mkuya Salum aliyeteuliwa na Rais kuwa mbunge masaa machache kabla ya kuteuliwa tena kuwa Naibu Waziri wa Fedha (huyu tayari ameshabatizwa "Waziri Voda fasta").

Kwa mujibu wa taarifa toka Ikulu uteuzi wao kama wabunge unaanza mara moja. Kikao cha bunge kinatarajiwa kuanza tena Juni mwaka huu ambapo tutategemea wabunge wateule kuapishwa. Hata hivyo, mawaziri wote wapya wanatarajiwa kuapishwa tarehe 7 Mei mwaka huu. Hii inamaanisha kuwa Prof. Sospeter Muhongo na Bi. Saada Mkuya Salum wataapishwa kuwa Waziri na Naibu Waziri kabla ya kuapishwa kuwa wabunge.

Je, inawezekana Waziri au Naibu waziri kuapishwa kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge?

=================================================

Majibu ya Naibu Spika, Job Ndugai:

Hata hivyo taarifa ya Ikulu haikusema wabunge hao wateule wataapishwa lini na wapi, lakini Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alipoulizwa jana alisema alisema kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, mtu yeyote anayeteuliwa kuwa mbunge, ataapishwa katika mkutano wa Bunge unaofuata baada ya uteuzi wake, bila kujali ni mbunge wa kuteuliwa au wa jimbo.

Ndugai alisema kwa msingi huo, wabunge hao wateule wataapishwa wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge la Bajeti unaotarajiwa kuanza mjini Dodoma, Juni 12.

Alipoulizwa itakuwaje ikitokea wateule hao wa Rais wakateuliwa pia kuwa mawaziri na kuendelea na kazi kabla ya kuapishwa kuwa wabunge, Naibu Spika alisema kwa hali ya kawaida, hilo haliwezekani.

?Kwa mujibu wa Katiba, mawaziri watateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, na anakuwa mbunge mteule hadi pale anapoapishwa, na ndiyo maana baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, kazi ya kwanza ya Bunge ni kuchagua Spika na Naibu Spika, ambao baadaye watafanya kazi ya kuwaapisha wabunge, na ndipo atateuliwa Waziri Mkuu na kisha mawaziri,? alifafanua Naibu Spika

Source: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=29712

========================================================

TAARIFA YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KWA VYOMBO VYA HABARI

Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri. Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.

Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:

?Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge?

Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.

Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria. Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.

Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.

Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

06 Mei, 2012

Elimu nzur
 
Swali hili limeulizwa tena, hopefully huu uzi utakuwa na majibu.
 
Back
Top Bottom