Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, May 4, 2012.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  May 4, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Katika Baraza jipya la mawaziri kuna wabunge wapya ambao waliteuliwa na Rais jana na leo kuwa mawaziri. Mawaziri hao ni Prof. Sospeter Muhongo ambaye aliteuliwa na Rais kuwa mbunge jana na leo ametuliwa kuwa Waziri wa Nishati na Madini. Mwingine ni Bi. Saada Mkuya Salum aliyeteuliwa na Rais kuwa mbunge masaa machache kabla ya kuteuliwa tena kuwa Naibu Waziri wa Fedha (huyu tayari ameshabatizwa "Waziri Voda fasta").

  Kwa mujibu wa taarifa toka Ikulu uteuzi wao kama wabunge unaanza mara moja. Kikao cha bunge kinatarajiwa kuanza tena Juni mwaka huu ambapo tutategemea wabunge wateule kuapishwa. Hata hivyo, mawaziri wote wapya wanatarajiwa kuapishwa tarehe 7 Mei mwaka huu. Hii inamaanisha kuwa Prof. Sospeter Muhongo na Bi. Saada Mkuya Salum wataapishwa kuwa Waziri na Naibu Waziri kabla ya kuapishwa kuwa wabunge.

  Je, inawezekana Waziri au Naibu waziri kuapishwa kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge?

  =================================================

  Majibu ya Naibu Spika, Job Ndugai:

  Hata hivyo taarifa ya Ikulu haikusema wabunge hao wateule wataapishwa lini na wapi, lakini Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alipoulizwa jana alisema alisema kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Bunge, mtu yeyote anayeteuliwa kuwa mbunge, ataapishwa katika mkutano wa Bunge unaofuata baada ya uteuzi wake, bila kujali ni mbunge wa kuteuliwa au wa jimbo.

  Ndugai alisema kwa msingi huo, wabunge hao wateule wataapishwa wakati wa Mkutano wa Nane wa Bunge la Bajeti unaotarajiwa kuanza mjini Dodoma, Juni 12.

  Alipoulizwa itakuwaje ikitokea wateule hao wa Rais wakateuliwa pia kuwa mawaziri na kuendelea na kazi kabla ya kuapishwa kuwa wabunge, Naibu Spika alisema kwa hali ya kawaida, hilo haliwezekani.

  "Kwa mujibu wa Katiba, mawaziri watateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge, na anakuwa mbunge mteule hadi pale anapoapishwa, na ndiyo maana baada ya kumalizika kwa Uchaguzi Mkuu, kazi ya kwanza ya Bunge ni kuchagua Spika na Naibu Spika, ambao baadaye watafanya kazi ya kuwaapisha wabunge, na ndipo atateuliwa Waziri Mkuu na kisha mawaziri," alifafanua Naibu Spika

  Source: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=29712

  ========================================================

  TAARIFA YA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI KWA VYOMBO VYA HABARI

  Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, tarehe 4 Mei, 2012 alitangaza mabadiliko katika safu ya Baraza la Mawaziri. Katika uteuzi wa Mawaziri na Manaibu Waziri, Mheshimiwa Rais aliwateua Mawaziri wapya kutoka miongoni mwa Wabunge aliokuwa amewateua na kuwatangaza. Baada ya uteuzi huo, kumetolewa maoni kwamba hatua ya Mheshimiwa Rais kuwateua Wabunge Wapya ambao hawajaapishwa Bungeni kuwa Mawaziri ni kitendo cha uvunjaji wa Katiba.

  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inayachukulia maoni haya kama ni jambo lenye maslahi ya jamii na linalohitaji kufafanuliwa; kwa upande mmoja lakini pia, kutolewa kwa elimu ya Umma; kuhusu Mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge.

  Msingi wa Katiba tunaoanza nao ni maelekezo ya masharti yaliyomo kwenye Ibara ya 55(4) kwamba:

  "Mawaziri na Naibu Mawaziri wote watateuliwa kutoka miongoni mwa Wabunge"

  Pili, ni mamlaka ya Rais ya uteuzi wa Wabunge aliyopewa na masharti ya Ibara ya 66(1)(e) yenye aina ya Wabunge wasiozidi kumi watakaoteuliwa na Rais kutoka miongoni mwa watu wenye sifa zilizotajwa katika aya za (a) na (c) za ibara ya 67 na angalau Wabunge watano kati yao wakiwa Wanawake. Wabunge aliowateuwa Mheshimiwa Rais wanatokana na Ibara hii.

  Tatu, baada ya hatua zote hizi ikumbukwe kwamba aliyeteuliwa au kuchaguliwa kuwa Mbunge anakuwa Mbunge ama baada ya kutangazwa na Msimamizi wa Uchaguzi; au baada ya kuteuliwa na Tume ya Uchaguzi kwa wale Wabunge wa viti maalum au anapochaguliwa na Baraza la Wawakilishi au anapoteuliwa na Rais akitumia Mamlaka yake ya uteuzi yanayotokana na Ibara ya 66(1)(e). Hivyo Wabunge wanaohusika hawahitaji kuapishwa kwanza Bungeni ili wawe Wabunge. Kiapo cha Mbunge Bungeni kinamwezesha tu kushiriki katika shughuli za Bunge.

  Katiba ya nchi haiweki kwa Rais masharti kwamba kabla ya kumteua Mbunge wa aina hiyo kuwa Waziri au Naibu Waziri Mbunge huyo awe ameapishwa Bungeni kwanza. Masharti mawili muhimu na ya kuzingatia ni kwamba mteule wa nafasi ya uwaziri au Naibu Waziri hatashika madaraka yake ila mpaka kwa mujibu wa Ibara ya 56 ya Katiba, awe ameapa kwanza mbele ya Rais kiapo cha uaminifu na pia kiapo kingine chochote kinachohusika na utendaji wa kazi yake kitakachowekwa kwa mujibu wa Sheria iliyotungwa na Bunge. Sharti la pili, litahusu kiapo cha Uaminifu katika Bunge kabla Mbunge hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge kwa masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba. Viapo hivyo havitegemeani na vinaweza kufanyika kwa nyakati tofauti.

  Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali inasisitiza kwamba Wabunge ambao hawajaapishwa ndani ya Bunge ni Wabunge na wanapoteuliwa kushika nafasi ya Uwaziri au Naibu Waziri ni halali kwa kuwa uteuzi huo haukiuki masharti yoyote ya Kikatiba au Sheria. Aidha, katika kutekeleza madaraka ya kazi ya Uwaziri au Naibu Waziri Mbunge atahitaji kiapo mbele ya Rais hata kama hajaapishwa Bungeni. Busara ya uandishi wa Katiba na Sheria imetambua kwamba kunaweza kukatokea uteuzi wa aina hiyo wakati Bunge limeahirishwa kama ilivyo sasa. Masharti ya Ibara ya 68 ya Katiba yatazingatiwa katika kikao cha Bunge kijacho.

  Bila shaka ufafanuzi huu utaleta uelewa katika jambo hili na kuepusha mikangayiko isiyokuwa ya lazima.

  Imetolewa na Jaji Frederick M. Werema (Mb)
  MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

  06 Mei, 2012
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  May 4, 2012
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Good observation!

  But who cares?
   
 3. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #3
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  mkuu soma ibara ya 68 ya Katiba ya Jamhuri.ya Muungano wa Tanzania utapata jawabu
   
 4. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #4
  May 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 3,058
  Trophy Points: 280
  hebu wenye kuelewa/kujua hili watusaidie kwakweli.
   
 5. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #5
  May 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  EMT hata mimi sijaelewa vizuri nadhani kuna mgongano fulani wa kikatiba. Katiba inasema Mbunge hatoanza kazi zake zake kama Mbunge mpaka atakapoapa kiapo cha ubunge. Sasa kuna maswali mawili: je rais akishakuteua kuwa mbunge unakuwa tayari mbmunge na haki zote bila kuapishwa na kutekelewa masharti ya kikatiba (kuwasilisha orodha ya mali, nyaraka za kuwa mbunge n.k)? Na je mbunge wa kuteuliwa na Rais anakuwa mbunge by the virtue of his/her appointment bila kulazimika kuapa na kutimiza masharti mengine?

  Lakini swali lako la msingi ni kubwa zaidi - kwa vile mawaziri ni lazima watoke miongoni mwa wabunge je waziri anaweza kula kiapo cha kuwa waziri kabla hajala kiapo cha kuwa mbunge. Jibu langu mimi ni hapana! Unless kama kuna precedence ambayo watu wanaweza kutukumbusha ambapo watu waliteuliwa na rais kuwa wabunge na wakapewa uwaziri KABLA ya kula kiapo cha Ubunge kwanza. I stand to be corrected.
   
 6. everybody

  everybody JF-Expert Member

  #6
  May 4, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kweli wewe ni bingwa wa reverse....nafikiri ulitakiwa kuanza na hiyo blue ifuate nyekundu...anyway tumekupata..
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  May 4, 2012
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Ibara inasema:

  Kimsingi kitu pekee ambacho mbunge mteule anaweza kukifanya kabla ya kuapishwa ni uteuzi wa spika - which is true kwa sababu spika ndiye anayeapisha wabunge!
   
 8. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #8
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu EMT wenzio tangia juzi tumelifanyia kazi hilo suala na tukapata jawabu. Anaweza akashika uwaziri bila kuapishwa ila.hawezi kushiriki shughuli za bunge kabla ya kuapishwa. hiyo wataapishwa june kabla ya kuanza sughuli za bunge
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #9
  May 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 3,058
  Trophy Points: 280
  Kiapo chaWabungeSheria ya1984 Na.15ib.13​
  68​
  . Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo chauaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakiniMbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
  hajaapishwa.
   
 10. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #10
  May 4, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watafanya kazi zao za uwaziri kama kawaida ila hawataruhusiwa kujibu chochote wala kuwakilisha sehemu yoyote mpaka hapo Semamba na Dodoma watakapowatambua!!
   
 11. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #11
  May 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 3,058
  Trophy Points: 280
  Ahsante kwa ufafanuzi...
   
 12. M

  Mtanganyika mweusi Member

  #12
  May 4, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau wa katiba wanadai hata ofisini kwa spika anweza kuapishwa sio lazima ndani ya ukumbi wa bunge
   
 13. Rogie

  Rogie JF-Expert Member

  #13
  May 4, 2012
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 3,058
  Trophy Points: 280
  nadhani red ya pili imeeleweka zaidi. Red ya kwanza swali linakuja je atakuwa anawajibika kwa nani?
   
 14. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #14
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kwa maana hiyo ni batili kuwa waziri kwa sababu uwaziri ni kazi za bunge? nilidhani kuwa tafasiri yake ni kwamba hataingia bungeni kujibu maswali ama kuwasilisha chochote bungeni kabla ya kuapa.
   
 15. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #15
  May 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Rais wa Tanzania ni demigod fulani anayeweza kubadili sheria wakati akiwaapisha kwa kusema hakuna alipokatazwa hata kuwaapisha kimpigo kama mawaziri na wabunge, kwanza yeye mwenyewe (rais) ni sehemu nzima ya bunge.

  On a serious note.

  Labda kuna tafsiri ya hii ibara ya katiba inayoweza kufanya kiapo kiwe ni formality tu.

  68. Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla hajaapishwa.

  Kama wanaomchagua Spika ni wabunge tu, na tunayemuita "mbunge mteule" anaweza kumchagua Spika (kabla ya kuapishwa na kuwa mbunge rasmi) basi "mbunge mteule" anaweza kuteuliwa kuwa waziri na kuapishwa uwaziri kabla ya kuapishwa ubunge.

  NB: Ameitwa "mbunge" hata kabla hajaapishwa. Katiba haijamuita hata "mbunge mteule".
   
 16. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #16
  May 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0

  Nimeipenda hii, Kwani kuwa mbunge ni sharti uwe umeapa kwa spika wa bunge. Sasa kama Spika ataitisha bunge la dharura kwa ajili ya kuwaapisha wabunge hawa kabla hawajawa mawaziri hilo litakuwa jambo zuri kwa katiba. Vinginevyo Wabunge na spika wa bunge waende wakaapishwe Dodoma week end hii kabla ya kuapishwa kuwa mawaziri jumatatu. Hapa CCM wasijifanye wanajua sheria, katika inaweka wazi kuhusu nani awe waziri. Rais hana mamlaka ya kusema ubunge wa mtu unaanza mara moja, unless mara moja hiyo imtake spika amwapishe mara moja kwanza.
   
 17. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #17
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #18
  May 4, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,197
  Trophy Points: 280
  Ibara ya 68 inatuambia mtu anakuwa mbunge kabla ya kuapishwa, kuapishwa ni kuonyesha utii kwa Spika tu, some formality inayohitajika ili mbunge aweze kushiriki shughuli za bunge. Uwaziri kabla ya kuapishwa ubunge hauhitaji Waziri afanye shughuli za bunge (kuna kazi za bajeti zitakazoingiliana na bunge hapa zitaendaje? Delicate).

  Ibara ya 68 haimuiti mtu aliyechaguliwa/teuliwa kuwa mbunge "mbunge mteule" inamwita "mbunge".
   
 19. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #19
  May 4, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Kwa mujibu wa kanuni wanatakiwa waapishwe kwenye mkutano wa kwanza kikao cha kwanza baada ya kuteuliwa/kuchaguliwa. hivyo itabidi waapishwe bungeni kwenye kikao na si ofisini kwa spika.
   
 20. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #20
  May 4, 2012
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  MM - There is LACUNA kwenye kifungu cha 68. Kimeeleza kuhusu kazi za bunge na uchaguzi wa spika lakini hakijaeleza kuwa je mbunge anaweza kuteuliwa kushika majukumuiyasiyo ya kibunge ambayo yanataka mteuliwa awe mbunge?. Maana yake ni kwamba, kifungu cha 68 hakijaweka wazi, so either way-inaweza fanyika. Anaweza tumikia au anaweza asitumikie-vyovyote vile atakuwa hajavunja katiba. Nafikiri 'Gap' hii ndiyo inayowafanya wabunge hao wateuliwa Ku-qualify kufanya kazi za uwaziri nje ya bunge ila watatakiwa kuapishwa na spika pindi bunge litakapokaa ili waweze kushiriki shughuli za kibunge.

  Conclusion yangu ni kuwa: Hakuna kizuizi kwa mawaziri hao wapya kuapishwa kabla ya kuapa kwa spika. Ila watatakiwa kuapishwa na spika ili waweze kujibu maswali ya wabunge bungeni. Hii ndiyo katiba yetu mianya kibao.
   
Loading...