Kuwa wa kwanza kupinga unyama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa wa kwanza kupinga unyama

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kuku dume, May 29, 2012.

 1. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani Wakuu!

  Jeshi la polisi limekuwa likitumia nguvu kupita kiasi kushambulia wananchi ambao mara nyingi huwa wanatekeleza haki yao ya KIKATIBA.

  Moyo unaniuma kwa kuwa vitendo hivyo vya jeshi letu vina madhara lukuki kwa jamii yetu ila kubwa zaidi ni kuzuia haki na kusababisha majeraha, vilema na wakati mwingine vifo.

  Ninasikitika kwamba tunawapa kichwa polisi wetu kutekeleza unyama kwa kuwa TUNATUMIA kodi za wananchi kujitibu.

  Kwa kipindi hiki kuna VVU na vimelea vingine vya magonjwa ambavyo huenea kwa njia ya damu lakina nashangaa bado wanatumia RUNGU moja kupiga watu lukuki. Tuko tayari kulea taifa la maradhi?

  Okoa Watanzania. Payuka wakati wa katiba mpya.
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Wazo zuri tutatiririka kwa wajumbe wa kukusanya maoni.
   
 3. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Pia polisi hapaswi kuua au kupiga raia kisa anaandamana
   
 4. w

  warea JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 244
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawajui walitendalo!
  Kuna kipindi jeshi la polisi walikuwa na programu ya kuzuia maambukizi ya ukimwi, wamesahau marungu yao pia yanaweza kueneza ukimwi!
   
 5. Bumpkin Billionare

  Bumpkin Billionare JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 1,336
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwenye maandamano risasi zinapigwa, kwenye kuchoma kanisa.....inapatikana ripoti ya zimamoto tu
   
 6. kuku dume

  kuku dume JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Apr 22, 2012
  Messages: 415
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lazima tuiweke hii wazi kwenye katiba mpya kama polisi atakutibu kwa majeraha atakayo kusababishia pamoja na matatizo mengine au la.
   
Loading...