Last_Joker
JF-Expert Member
- Nov 23, 2018
- 269
- 410
Unajikuta mwaka unaisha bado upo solo, hakuna bae wala boo, hakuna mtu wa kukutumia "umelalaje baby?" wala wa kukupa good morning texts zenye emoji ya jua na moyo... lakini wewe hujisikii vibaya. Au labda unajisikia, ila umezoea? Swali linakuja – je, kuwa single muda mrefu ni uhuru mtamu au ni jeraha lisilotibika la mapenzi yaliyopita?
Wako huru kama tai – wana-focus na maisha, kazi, ndoto zao. Na hawataki kuharibu hiyo "peace" yao kwa kuleta mtu atakayewa-balance emotionally.
Wanasema “mapenzi ni ya muda, amani ni ya kudumu.”
Unakuta mtu alikuwa romantic mbaya, sasa hata SMS ya hi inamkumbusha betrayal. Anaona mapenzi ni scam, watu wote ni waongo, na hakuna love ya kweli.
Kuwa single kwake si kwamba anapenda, ni self-defense. Ni kujilinda dhidi ya heartbreak ya pili au ya kumi.
Lakini vigezo hivyo vimekuwa vikali hadi mtu wa kawaida hawezi kuvipita.
Labda tatizo siyo kukosa mapenzi, bali ni kutoweka realistic expectations. Mapenzi ya ki-movie hayaishi Tanzania, jamani 😂
Kuwa single muda mrefu ni uhuru halisi au ni kivuli cha maumivu yaliyopita?
Drop maoni yako pale chini – tuchambue mapenzi bila presha, bila bias, kwa lugha ya mtaa!
“Single Life” ni Peace au ni Kujiburudisha Kimya Kimya?
Kuna watu wakiamka asubuhi wanashukuru Mungu hawana stress za wapenzi. Hakuna mtu wa kulalamika, hakuna kufuatiliana, hakuna pressure ya birthday gifts au posting za anniversary.Wako huru kama tai – wana-focus na maisha, kazi, ndoto zao. Na hawataki kuharibu hiyo "peace" yao kwa kuleta mtu atakayewa-balance emotionally.
Wanasema “mapenzi ni ya muda, amani ni ya kudumu.”
Lakini Vipi Wale Waloumia Mpaka Wakakata Tamaa?
Sio kila mtu alichagua kuwa single. Wengine wamepigwa character development za kutosha hadi wamefunga mlango wa moyo na kutupa funguo baharini.Unakuta mtu alikuwa romantic mbaya, sasa hata SMS ya hi inamkumbusha betrayal. Anaona mapenzi ni scam, watu wote ni waongo, na hakuna love ya kweli.
Kuwa single kwake si kwamba anapenda, ni self-defense. Ni kujilinda dhidi ya heartbreak ya pili au ya kumi.
Au Ni Sisi Tumeweka Vigezo Vikali Sana?
Siku hizi, ukiongea na watu wengi waliopo single, watakwambia wanangoja mtu “mature”, “mwenye vision”, “asiwe mchepukaji”, “mwenye fear of God”, “anajua kujielewa”, “not toxic”...Lakini vigezo hivyo vimekuwa vikali hadi mtu wa kawaida hawezi kuvipita.
Labda tatizo siyo kukosa mapenzi, bali ni kutoweka realistic expectations. Mapenzi ya ki-movie hayaishi Tanzania, jamani 😂
Hebu Tujiulize...
- Ni lini mwisho uliwahi kupenda bila hofu?
- Unajisikiaje unapowaona watu wako wakipost couples goals?
- Unaamini bado kuna mtu wa kukupenda real au ushawachoka?
Njoo utoe ya Moyoni hapa kwa Comments
Wewe ni mtu wa #TeamSingle by choice au umekula matukio hadi ukapewa kitambulisho cha uanachama?Kuwa single muda mrefu ni uhuru halisi au ni kivuli cha maumivu yaliyopita?
Drop maoni yako pale chini – tuchambue mapenzi bila presha, bila bias, kwa lugha ya mtaa!