Kuwa na kiongozi wa nchi vuguvugu kunahatarisha amani na maisha ya wanasiasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuwa na kiongozi wa nchi vuguvugu kunahatarisha amani na maisha ya wanasiasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Determinant, Nov 17, 2011.

 1. D

  Determinant Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa muda mrefu sana Rais Kikwete amekuwa vuguvugu, kuna wakati anaonyesha kupiga vita ufisadi na mafisadi lakini haonyeshi kuwashughulikia marafiki zake wanaohusishwa na ufisadi. Najiuliza hivi nae ni fisadi? Kitendo hiki kimeleta uadui kati ya wanaopinga ufisadi na wanaohusika na ufisadi. Ndio maana kuna watu wanatishiwa kuuwawa na wengine kuwekewa sumu. Lakini tunajua mafisadi wote ni rafiki zake Rais na wanaopinga ufisadi si marafiki wa kikwete hivyo anashindwa kutoa maamuzi magumu.

  Lakini akae akijua wanaopinga ufisadi ni marafiki sana wa wananchi wa kawaida na masikini ambao vilevile ni asilimia kubwa ya nchi. Siku wananchi watakapochoka na kuungana na wapinga ufisadi wakitumia nguvu ya umma sijui atajificha caravat gani na maswahiba wake.
   
Loading...