Kuwa msema kweli kwa wanawake

Kuwa msema kweli kwa wanawake

Habari wakuu,

Hiki ni kisa kilichomtokea rafiki yangu na nilijifunza mengi kutokana na kisa chake cha mahusiano na naona ni vyema tuka share wengine pia wajifunze.

Ilikua ni siku yenye kunyesha mvua na David alikua anatoka kwa bibi yake na wakati huo alikua anarudi nyumbani kwao, baada ya kushuka kwenye daladala alianza kukimbia kutafuta sehemu ya kujihifadhi na mvua na kwa bahati mbaya akagongana na mdada aliyekua ameshika mwamvuli kwa kua alikua akitazama chini, anamuomba msamaha yule dada huku akijifuta maji yaliyokua yakichirizika usoni mwake lakini moyo ukaanza kudunda kwa haraka alipomuangalia huyo mwanamke aliyegongana nae, "alijibu yule dada" usijali ila uwe unaangalia mbele unapokimbia.

David aliendelea kumshangaa yule dada mpaka yule mwanamke alipoanza kuondoka na kuelekea kupanda daladala, David anamuangalia hadi yule mwanamke anapanda daladala hadi gari inaondoka na hapo anasikitika na kuanza kuondoka lakin safar alikua akitembea taratibu na ghafla akisikia akiitwa kwa sauti "wewe kijana umedondosha simu yako hii" anapokea simu ndogo ya nokia kutoka kwa mzee wa makamo akiambiwa aingalie kama haijaingia maji. Hadi anapokea simu anafahamu si simu yake lakini anaipokea na kuweka mfukoni na kuelekea nyumbani.

Njiani simu ilianza kuita na akafahamu hiyo si simu yake ni ile simu nyingine na anapokea kwakua simu haikua na nywila yoyote na kuanza kusikiliza masikioni, " Samahani nakuomba unisikilize kwa dakika chache" ilisikika sauti ya kike, David alijibu sawa dada angu nakusikiliza "

Naomba unirudishie hiyo simu kaka yangu kuna namba muhimu au hata laini peke nikiipata kwa kua kuna jambo muhimu na mtu nitahitaji kuwasiliana nae kupitia namba hii.." simu inakata na David anapoingalia anaona simu imezima na anapojaribu kuiwasha inaonyesha haina chaji na kujizima tena, anairudisha mfukoni na kuelekea nyumbani na anafika nyumbani na kubadilisha nguo na kukaa kitandani na kuanza kuitazama simu ile ambayo si yake na anatoa laini na...
Stry gan inaishia njian mapema hv
 
Back
Top Bottom