Kuwa makini ununuapo kiwanja Bagamoyo

blackeye

JF-Expert Member
Mar 28, 2016
300
95
Chukua hii

Ukija Bagamoyo kununua kiwanja au shamba usikumbuke kuja na hela peke yake bali pia kumbuka kuja na akili zako bila hivyo UTABAMBIKIWA vifuatavyo:-

Shamba au Kiwanja Feki

Mwenyekiti wa Kijiji Feki

Mtendaji wa Kijiji Feki

Muuzaji wa kiwanja /shamba Feki

Shahidi Feki

Jirani Feki anayejifanya ndio anapakana na kiwanja au shamba unalouziwa

Watoto Feki wataitwa kucheza ili muuzaji aonekane ana familia na si mhuni

Mke Feki wa muuzaji kwamba ataitwa kukusalimia

Nyaraka Feki

Mihuri Feki

Ofisi ya Kijiji Feki, bendera ya taifa itawekwa nje ya ofisi kama boshen.

Siku ukigundua umeuziwa kiwanja cha mtu au shamba lililoko katika mradi wa EPZA hao wahusika wote huwaoni na ndipo utagundua kuwa hata namba zao za simu ni Feki.

Kuweni makini, ukishapigwa hela zako za mkopo wa CRDB fahamu kuwa vitisho vya Polisi au kuroga havitasaidia hawa jamaa hutawapata kwa polisi na wala hawarogeki.
 
Back
Top Bottom