ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
Habari wanajamvi wenzangu,
natumai mko fiti kabla sijamaliza mwaka huu nimekuja na kitu kingine leo ambacho kitawafanya wadada na wamama zetu kuwa makini na watu wa aina hii ninaowaelezea hapa. Kuna WANAUME ambao mara ya kwanza wakikutana na wadada watajichetua na kusema maneno mengi yasiyo na maana tena wengine watajichetua kwa kusema kuwa nikupeleke lunch ama dinner twende hoteli gani wewe chagua usiwe na wasiswasi hapa ni BOT hapaishiwi kitu na kumbe ana lolote ni magilini na mpita njia tu anataka kukuaharibia tu ili uingie line na akishakuweka katika timeline yake basi umebugi womeeen. Wanaume wengine utawasikia kuwa ohoo nitakujengea nyumba ya ghorofa wakati yeye mwenyewe anaishi banda la uani manzese B, hana hata godoro sasa hilo ghorofa hatalimuduje wakati maisha yake tu kwa siku yanamshinda. Nataka kuwataadharisha wadada na wamama acheni tabia ya kumzoea mtu kwa siku na kufanya urafiki wa nguvu naye si busara wala sio vyema kabisa wanawadanganya hao ni matapeli wa mapenzi wana jipya ndani yao wamebaki kujishaua tu kuwa makini na watu wa aina hiyo, na ni vyema ukajifunza kutokana na maneno yao ya mara ya kwanza. Natumai mtanielewa na kuchukua hatua za kutokujianika bure kwa mabazazi wabaya na waharibifu kama hao
Happy new year 2013