Kuwa makini na kuondoa uchafu masikioni kwa kupigwa bomba

Mwanapropaganda

JF-Expert Member
Aug 19, 2014
4,235
2,505
Kuna jamaa nilikutana naye akaniambia sikio lake moja halisikii vizuri tangu alipopigwa bomba hospitali ili kuondoa uchafu sikioni miaka ya nyuma kidogo. Kwahiyo upigaji bomba unaweza usiwe mzuri na hakuna njia nyingine inayotumiwa na madaktari kusafisha sikio zaidi ya hiyo ya kuchomekwa bomba na kusukumiziwa maji ya moto.

Pamoja na hayo sisemi kwamba usiende hospitali kusafishwa sikio kwa njia hiyo.
 
Sijakuelewa mkuu.
Nina maanisha kuwa kama nako kutumia bomba ni risk wakati ndio njia ya kitaalamu....si watu wataacha kusafisha masikio....na matokeo yake si masikio yataziba kwa tope la uchafu......maana mtu kwa uoga anaweza akaacha moja kwa moja kutoa uchafu kwa kuhofia kusababishiwa uziwi wa ukubwani.....
 
Mkuu KikulachoChako kupigwa bomba sio njia inayotumiwa kuondoa uchafu kwa vijiti vya pamba kama tulivyozea, bali ni kutoa uchafu kwa kusafishwa na daktari kwa kuingizwa tube maalum sikioni ambayo inatumika kuingizwa maji ya moto na kusukumwa ndani na kupitishia uchafu huo baada ya maji kuingizwa sikioni. Huduma hiyo inatolewa mahospitalini. Mzizi mkavu anaweza kutoa ufafanuzi zaidi.
 
Sasa mkuu kama nayo ni risk watu wataogopa kupata hiyo huduma...
 
Wanaoishi maeneo ya joto wana nafuu maana uchafu huo (Ear Wax) hulainika na kutoka kirahisi, ila sisi wa kwenye baridi hurundikana na inafika wakati sikio halisikii vema.

Yote kwa yote kupigwa bomba ni hatari sana kwa vile sehemu ya ndani ya sikio ni laini sana. Unaweza kuwa KIZIWI kabisa!
 
Usafi mzuri wa sikio ni kuchokoa sikio kwa kutumia kidole cha kidogo (little finger) hadi pale kinapoishia. Usitumie pamba wala vijiti kama wengine wanavyotumia njiti za kiberiti.Pamba na njiti ni hatari kwa usalama wa sikio lako. Ule utando (ear wax) unaouona sikioni ni muhimu sana ukiutoa wote unahatarisha sikio lako. Kazi ya ear wax ni kuzuia foreign bodies kuingia kupitia sikio. Foreign bodies zinazoweza kuingia kupitia sikio ni kama wadudu, mfano sisimizi, vumbi na maji. Usafishaji wa sikio na kuondoa ear wax ambao wengi wanadhani ni uchafu ni hatari sana kwa afya yako. Kupigwa bomba kama kulivyoelezwa kunatakufanyike tu pale ambapo imelazimika kufanyika hivyo. Yaani kufanyike kwa ajili ya kuondoa foreign bodies zilingia sikioni. Isifanyike kama desturi kwamba baada ya miezi kadhaa unaenda hospitali kusafishwa sikio kwa kupigwa bomba.
 
Hivi ni kila unapopiga bomba ni lazima madhara yatokee au inakuaje? Halafu kwani hadi sasa hospital zimeshindwa kubuni njia nyingine ya kusafisha sikio? Maana nasikia wanapitisha maji ya moto na kuya-pressure kuelekea ndani ya sikio na nasikia mgonjwa atasikia maumivu makali sana.
 
Back
Top Bottom