Kuwa makini: Hawa ndio wanaoharibu haiba ya biashara ya electronics Zanzibar

abmzanzibar

Member
Jun 9, 2022
23
20
Ni muhimu kusoma:

Siku za hivi karibuni, nimekua nikipokea simu za watu wengi kutoka Tanzania bara hususan mikoani.

Hii imetokea baada ya kupost makala moja inayoelezea kuhusu bei za bidhaa za ELECTRONICS pamoja na gharama za usafiri kutoka ZANZIBAR kwenda BARA.

Licha kutoa ufafanuzi wa kina, ila bado watu wengi wanaendelea kupiga simu kuniuliza mambo mbali mbali yanayohusu bidhaa pamoja na mchakato wa usafirishaji!

Wengi huonesha kuvutiwa kwa UNAFUU wa bei uliopo, ila ni wachache tu kati ya hao, ndio ambao huchukua maamuzi ya kuagiza bidhaa kutoka hapa ZANZIBAR.

Hii inatokea kwasababu ya uwepo wa idadi kubwa ya WADANGANYIFU MITANDAONI!

Watu ambao huvaa vinyago vyenye haiba ya ZANZIBAR ili kuficha dhamira zao mbaya (kuwaibia watu).

Mbinu yao ya kujifanya wapo Zanzibar, kwa ku-deal na uuzaji wa ELECTRONICS bila shaka inawapa matokeo mazuri!

Hutumia mitandao kuonesha bidhaa ambazo ki-uhalisia hawana!
Huweka bei za kuvutia ili kuwanasa wale wasio na uelewa!
Ukiwapigia simu watakwambia "tuma pesa nusu ili tukutumie mzigo, nyengine utamalizia mpaka ukipokea mzigo wako"

Kwa kweli inasikitisha sana kuona watu wengi wananasa kwenye mitego hiyo!

Hayo yanatokea kutokana na MATAPELI hao kujivisha kinyago cha ZANZIBAR, jambo ambalo ni kinyume na uhalisia wao!

Unafuu wa bei pamoja na sifa ya UAMINIFU kwa WAZANZIBARI ndio sababu ya matapeli wengi kujivisha kinyago hicho!

Kwa hiyo, wengi wao wanaotumia mbinu hizo ili kulaghai watu, kiuhalisia huwa hawapo ZANZIBAR.
Binafsi nimefanya tafiti za kutosha kuthibitisha hilo!

Mfano:
Instagram: @babuu_electronic
Na @zanzibar_electronics_og

Hizo ni account mbili tofauti za Instagram, Hao jamaa wanajifanya wapo zanzibar, na ukiangalia accounts zao kwa kiasi fulani zinashawishi, ila kwa 100% ni MATAPELI.

Kwa hiyo, watu kama hao ndio wanao haribu HAIBA ya ZANZIBAR na kupelekea mambo kuwa magumu kibiashara!

Kinacho-sikitisha zaidi ni kwamba idadi ya wadanganyifu hao, bado inaendelea kukua kwa kasi mno!

Ni vyema kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwekeza nguvu na kuonesha ari ya kudhibiti na kutokomeza janga hilo!

Kinyume na hivyo, hali inaweza kuwa mbaya zaidi kwa siku zijazo.

Bali sio tu jukumu la POLISI, pia ni wajibu wako kuwa makini kujilinda kabla ya kulindwa. Unatakiwa kutumia sana akili kufikiri na kuchanganua ili kujinasua kwenye mitego wanayoitumia kukunasa.

Epuka PUPA na TAMAA! Hawa jamaa ni wabaya sana kwa kucheza na akili za watu! | KUWA MAKINI.

Mahabey | Based in Zanzibar.
EPUKA UDANGANYIFU: Ikiwa unahitaji msaada wowote kuhusu Electronics Nitakusaidia!

KARIBU | 0673563323
 
Mmmmmmhmn we jamaa mjanja hapa hapa umetangaza biashara.
Kama nililiona kuwa ni tatizo linalo athiri maisha ya wengi, kwanini nisiwe mtatuzi kaka!?

Nawakaribisha wale wote ambao wanahisi nitaweza kuwasaidia!
 
kuna mmoja enzi hizo tumechat vizuri sana instagram akanipa namba yake nimtumie hela sasa nika i copy ili nikibonyeza ile menu yakutuma pesa ni paste pale
la haula walakuwata true caller ikaji search (watumiaji wa true caller mnaelewa) ikaniletea jina tapeli zanzibar na biashara ikafia hapo
 
Hata wewe unaweza kuwa tapeli pia kwa kuwaponda matapeli wenzako ,,(ni mtazamo wangu tu ),,
Sawa akhy.. lengo langu sio kubadilisha mitazamo ya mtu.
Bali ni kuwafahamisha wale wasio na uelewa!
Na nitaendelea kufanya hivo kila nitakapo-jiskia kufanya.
I don't care.
 
Back
Top Bottom