Kuwa dalali au mtu wa madini

Kuwa dalali au mtu wa madini

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
23,621
Reaction score
56,937
Ipo kazi nzuri kati ya hiyo kwa mtu ambaye ana ari ya kupambana kutoboa kirahisi.changamoto ninayoijua Mimi kwenye madini ni kwamba lazima uyajue madini lazima uyajue aidha uyasomee au uzoefu.na hata udalali uwe mzoefu na mwenye NGUVU ya ushawishi MPAka kuachiwa kuendesha mchongo.

All in all sekta hizi mbili zimewapa watu fedha nyingi bila kutumia nguvu sana .Hata hivyo mafanikio ya mtu yanabaki kuwa kwenye mawazo yako..Hela zio Tanzania michongo ya kukupatia millions 50 io ni uwoga wako tu kutojiingiza kwenye madini au udalali wa viwanja na majumba na mali.

Usiseme kwamba hizo kazi ni ngumu ila wewe ndo huja penetrate kwenye minara hiyo miwili kiundani.Maarifa tayari unayo mengi na hapa jf tahadhari za watu na nondo zao kuhusu hizo sekta ni tosha kwa wewe kuwa na maarifa..ingia field sasa tafuta network ya wauzaji mali kubwa na watafutaji mali kubwa.
 
Udalali, udalali,udalali, udalali

Pesa ni rahisi Tatizo ni kaushawishi Ka dhuluma.

Kuna mstari mdogo sana unaotenganisha Udalali na dhuluma.

Kesi ni nyingi,
Malalamiko mengi,
Pamoja na migongano kadhaa.

Unamuachia dalali auze nyumba Kwa bei fulani ,yeye anatamka bei kubwa kiasi cha wateja kushindwa,lakini na wewe mambo yanachelewa.

Unamuachia Eneo auze Kwa milioni 25 yeye anatafuta mteja wa milioni 50 na anapata 25 mbele yako,halafu bado anataka percent kwenye 25 ya kwanza.

Lakini pia kughushi nyaraka feki,na kujipatia pesa kiudanganyifu Kwa kuuza vitu visio vyao kisha kuwaachia misala wanunuzi.

Zipo faida nyingi za madalali ikiwa ni pamoja na kupata vitu Kwa wakati na usahihi
 
Madalali ni wasenge wasenge wamezoea kuuza vitu vya watu wenye shida au wasiojua mteja...sasa ukikutana na mtu anayefanya biashara halisi na anauza kitu anachojua dhamani yake dalali anakuwa mzigo na usumbufu wa biashara.

Siku hizi kwenye madini hakuna udalali labda uwe broker ni dalali mwenye mtaji na leseni ya kununua madini au vibali hivyo unakuwa na mtaji wako na ujuzi..unachukua kwa wachimbaji wadogo unapeleka town kwenye soko la madini.

Hapa hasara inakuwepo na faida inakuwepo ni kutuliza ninembe ukicheza na hisia za kutoboa chap inakula kwako mazima na mpaka uuziwe hayo madini na wachimbaji wadogo lazima uwe umeshawalisha au kukupiga vibomu hatariukija kwenye kalculator unakuta madini ni madogo kuliko huduma na usipowapa wanamuuzia bosi aliyewawezesha..
 
Ifike mahali madalali wadhibitiwe,uhuni umekua mwingi sana.
Misala mikubwa sana wametuachia iliyokuja kutucost mamilioni ya fedha mpaka kuyumba ktk biashara zetu
 
Back
Top Bottom