Boniphace Bembele Ng'wita
JF-Expert Member
- Dec 25, 2013
- 3,594
- 2,030
Mkuu tanganyika yetu, Bunge lilishavunjwa ile siku rais analihutubia bunge!, ila uhai wa bunge ambao ni statutory unamalizika rasmi leo tarehe 20/08/2015!.
statutory maana yake ni kwa mujibu wa sheria ambapo tangazo rasmi la kuisha kwa uhai wa bunge hili utatangazwa kwenye gazeti la serikali na Tume ya Uchaguzi itatangaza majina ya wagombea na kuanza rasmi kwa kampeni!.
Mfano mtu anaweza kuteuliwa kuwa balozi, uteuzi huo unaweza kutangazwa leo tarehe 20/08/2015 lakini uteuzi huo ukawa umeanza tangu tarehe 01/08/2015 au unaanza 01/09/2015, statutory maana yake ni kipindi rasmi cha kuanza au kumalizika rasmi kisheria ambao hutangazwa kwenye Government Gazette!.
Muda wa ukomo wa serikali yetu kukaa madarakani ni tarehe 30/11/2015, lakini uchaguzi unafanyika zaidi ya mwezi mmoja kabla, hivyo hata Lowasa akiishashinda ile October 25, sio lazima aapishwe fasta fasta, anaweza kuapishwa muda wowote mwezi November, kwa sababu serikali inakua bado ina uhai wa kufanya kazi hadi November 30!.
Pasco
Mkuu hapo kwa edo umevuruga