Kuvunjwa kwa Bunge Tarehe 20 August 2015

Kuvunjwa kwa Bunge Tarehe 20 August 2015

Nakumbuka JK alivyokuwa anahutubia Bunge alisema atavunja Bunge leo tarehe 20.08.2015, naomba kujuzwa kama JK ameshalivunja Bunge na kama bado ni saa ngapi analivunja bunge.

Kwanza likizo yake anaianza lini manake namwona bado anazindua miradi kweli Urais mtamu.
 
atalivunja sangapi wakati wabunge wake wanavunjana mbavu na miguu , ndicho kilichobaki ccm.
 
Kikwete hawezi kwenda Dodoma kuvunja bunge,wanaogopa nguvu ya Lowassa na UKAWA maana hawataweza kumzuia kama kule Mwanga kwenye Mazishi,bunge limekufa kibudu!!!
 
Kiswahili somo zuri tena ni lugha ya taifa
 
Nakumbuka JK alivyokuwa anahutubia Bunge alisema atavunja Bunge leo tarehe 20.08.2015, naomba kujuzwa kama JK ameshalivunja Bunge na kama bado ni saa ngapi analivunja bunge.

Mmmmmh! Kuna nini tena mpaka wanaamua kulivunja Bunge letu lililojengwa kwa gharama kubwa hivyo, au wamegundua nalo liko barabarani tena?
 
Tupekue magazeti ya leo ya serikali kujiridhisha kama ametekeleza ahadi yake hiyo.

mkuu ni Government Gazette ambalo hupatikana kwa mpiga chapa wa serikali au government bookshop, lakini kamwe huwa halipo mtaani.
 
Kwlei sikujua kuna mtu anaamini maneno ya kikwete na ccm yake.

Ninaashindwa kabisa kuelewa huyu mtu hata huo uwaziri aliupataje.

Kwa muda huu ulioongezwa, nini mustakabali wa malipo na huduma zingine kwa hao wabunge?

Nani atalipa hizo gharama zote zikiwemo zakuitisha bunge ili livunjwe?

Ni lini marekebisho ya katiba yalifanyika ili kuwaongezea wabunge muda wa ziada?

Budget hiyo ya ziada ilipitishwa lini na chombo gani?

Ccm ni mauti kwa taifa.

Mkuu taarifa ya kuvunjwa bunge itatolewa kwenye gazeti la serikali na sio kukusanya wabunge kule mjengoni! Acha munkari, chapa kazi
 
Kikwete wala hastahili kuitwa JK... Hilo jina libaki kwa wenye busara ambazo hazina mashaka...

Kikwete hajawai kutoa kauli na ikatekelezwa na yeyote hata yeye mwenyewe mara kadhaa anashindwa kutekeleza kauli zake...

Kikwete akiendelea kuzunguka na Magufuli atatia aibu...!!
 
kama JUMA KASEJA
 
we jamaa sijui unatoka pori gani; alichosema siku ile ni kua ukomo wa bunge ni leo; alichofanya yeye sikuile kwa ile hotuba yake ni kutangaza hilo; hati ashasaini; sasa siku nyingine fikiri kabla ya kupost
 
Ungewaacha wamalize kwanza kuonyesha ushamba wao ndio uwaelimishe manake kuna wengine wengi umewastua hawatapost utumbo. Jaman Mwinyi Mpya wa Wazaramo yuko wapi siku hizi.

Bunge halivunjwi kwa kikao maalum cha bunge bali kwa waraka wa rais ambao utatangazwa katika Government Gazette!

Hivyo litafute hilo gazeti!

tanganyika yetu
 
Bunge halivunjwi kwa kikao maalum cha bunge bali kwa waraka wa rais ambao utatangazwa katika Government Gazette!

Hivyo litafute hilo gazeti!

tanganyika yetu

Bunge linavunjwa kwa kuhutubia taifa,asisahau kuweka na hotuba kwenye gazeti
 
Last edited by a moderator:
Nakumbuka JK alivyokuwa anahutubia Bunge alisema atavunja Bunge leo tarehe 20.08.2015, naomba kujuzwa kama JK ameshalivunja Bunge na kama bado ni saa ngapi analivunja bunge.
Mkuu tanganyika yetu, Bunge lilishavunjwa ile siku rais analihutubia bunge!, ila uhai wa bunge ambao ni statutory unamalizika rasmi leo tarehe 20/08/2015!.

statutory maana yake ni kwa mujibu wa sheria ambapo tangazo ra
smi la kuisha kwa uhai wa bunge hili utatangazwa kwenye gazeti la serikali na Tume ya Uchaguzi itatangaza majina ya wagombea na kuanza rasmi kwa kampeni!.

Mfano mtu anaweza kuteuliwa kuwa balozi, uteuzi huo unaweza kutangazwa leo tarehe 20/08/2015 lakini uteuzi huo ukawa umeanza tangu tarehe 01/08/2015 au unaanza 01/09/2015, statutory maana yake ni kipindi rasmi cha kuanza au kumalizika rasmi kisheria ambao hutangaz
wa kwenye Government Gazette!.

Muda wa ukomo wa serikali yetu kukaa madarakani ni tarehe 30/11/2015, lakini uchaguzi unafanyika zaidi ya mwezi mmoja kabla, hivyo hata Lowasa akiishashinda ile October 25, sio lazima aapishwe fasta fasta, anaweza kuapishwa muda wowote mwezi November, kwa sababu serikali inakua bado ina uhai wa kufanya kazi hadi November 30!.

Pasco
 
Nikirejea hotuba ya mwisho ya Rais kulihutubia Bunge alisema kwamba Bunge la 10 litafikia ukomo wake tarehe 20 Agosti 2015. Hii ina maana kwamba serikali yetu kuanzia kesho kukipambazuka haitakuwa na mawaziri. Tunawataka warudishe magari yetu na mali zote za wananchi ili tufanye maandalizi ya kuzikabidhi kwa serikali mpya.
 
Labda Wanaendelea mpaka wakabidhi kijiti kwa wale wapya
 
Back
Top Bottom