Kuvunjika kwa U.S.S.R chini ya Mikhail Gorbachev.

roservelt

JF-Expert Member
Aug 31, 2016
1,418
1,510
Kuvujika kwa U.S.S.R chini ya Mikhail Gorbachev.

Habarini wanabodi!!

Mwaka 1922 umoja wa nchi za kijamaa uliundwa (Union of Soviet Socialist Republics). Umoja huo uliundwa na nchi kama Romania, Poland, Czechoslovakia, Russia, Serbia, Yugoslavia na Ujerumani Mashariki.Marekani alikataa kuunga mkono uundwaji umoja huo. Joseph Stalin aliiongoza USSR kuanzia mwaka 1929 hadi1953. Mwaka 1939 Stalin aliingia mkataba wa kutopigana na kulindana na dikteta Adolph Hitler wa Ujerumani. Baadae Hitler aliusaliti mkataba huo na kuandaa jeshi lake zidi ya USSR.

Mwanzoni mwa kipindi cha vita baridi 1940s, Joseph Stalin akiwa rais wa USSR aliwezesha muungano huo kuwa juu kiteknolojia, uzalishaji wa silaha na kiuchumi. Hii ilisaidia USSR kuweka upinzani mkubwa zidi ya Marekani katika vita baridi.

Mnamo mwaka 1980s Mikhail Gorbachev alitawazwa kuwa rais wa USSR. Chini ya utawala wa Gorbachev alifanikiwa kuleta mapinduzi makubwa ya sera za kigeni za USSR. Mnamo mwaka 1985 Gorbachev alifanikiwa kurudisha mahusiano baina ya USSR na Marekani chini ya rais wa Marekani wa kipindi hicho Ronald Reagan.

Mnamo mwaka 1980s dunia ilikumbwa na mtikisiko wa kiuchumi uliosababishwa na kushuka kwa bei ya mafuta.Hii ilipelekea Gorbachev na serikali yake kupunguza nguvu kubwa katika washirika wake wa Ulaya Mashariki na duniani kote.

Katika harakati za kuinusuru USSR zidi ya mtikisiko wa kiuchumi, Gorbachev aliamua kupunguza uwekezaji mkubwa kwenye uzalishaji wa silaha wakati wa vita baridi na kuhamishia uwekezaji kwenye maeneo yenye kuleta faida kiuchumi.

Kufikia mwaka 1980s hadi 1988s USSR ilifanikiwa kupunguza nguvu kubwa kwenye vita baridi zidi ya Marekani. Mnamo mwaka 1989 Gorbachev na George H. W. Bush walitangaza mwisho wa vita baridi.

Mnamo mwaka 1991 USSR ilivunjika , Russia na nchi nyingine zikawa nchi huru zinazojitegemea.

NOTE.

Inasemekana Gorbachev alikuwa pandikizi wa taifa la Marekani, hivyo aliihujumu Russia na kuipa nafasi Marekani kuwa juu hadi leo hii.
 
Warusi walijiangusha wenyewe walijiimarisha kutengeneza siraha kwa gharama kubwa mengine wakayaweka pale Cuba.

Wakasahau kujenga nchi.
Kipindi hicho iliwalazimu kufanya hivyo kwani baada ya vitaa ya pili ya dunia Russia na USA ndio walikua wana nguvu duniani.
Katika vita baridi Russia alihitaji kuonekana yuko juu katika technology ...uzalishaji wa silaha na kiuchumi.
 
USSR ilianza kuanguka hata kabla ya Gorbachev. Bahati mbaya sana aliyeuua ule umoja ni Boris Yeltsin na walevi wenzake wawili kwenye Msitu wa Belazheva.

Gorbachev alipunduliwa na KGB mwaka 1991 na walitangaza hali ya hatari nchi nzima kwa dhumuni la kuzuia nchi nyingine zisipate uhuru.

Boris Yeltsin ndiye aliyezuia ule uasi na kuusambaratisha umoja wa Kisovieti. Alikuwa na maamuzi ya kukurupuka sana na mihemko bila hata kufikiria.

Hizi Progaganda za Neo-Cons kama waliiangusha USSR ni za kipuuzi sana.
Gorbachev angekuwa pandikizi nakuhakikishia angekuwa kama Alexander Litvinienko leo hii.
 
Kuanguka kwa soviet kuna faina kwa Russia.
Japo ni aibu mkakati kufeli. Lakini kwa maslahi mapana ya wananchi wa Russia , kulihitajika umoja huo ufe.

Kama alivyosemaGorbachev, USSR Ni umoja uliokua hauna vision.

Gharama kubwa waliwekeza kwenye kutengeneza military pact na silaha za kivita.
Hali ya wananchi ikawa duni.
Vita waliowekeza ikawa haipiganwi.. Huku Muda unazidi kwenda.
 
Kwa kuweka sawa mambo ni kuwa hizo nchi ulizotaja hazikuwa sehemu ya utawala wa USSR Bali walikuwa washirika wake Mwenye mambo ya ulinzi ikijulikana kama WARSAW PACT napia zilikuwa na Sera ya kijamaa kama USSR. Na umoja huo ulikuwa ni kukabiliana na NATO ya Marekani na nchi za kibepari za magharibi kama zinavojulikana leo. Baadhi ya nchi zilizounda USSR ni Uzbekistan ,Kazakhstan, Byelorus , Ukraine, Georgia na zingine kaama name zote zinamzunguka Russia ya Leo .Gorbachev hakupandikizwa yeye alianzisha ya Uhuru na Uwazi akiita Perestroika na Glasnost. Wahafidhina wa chama chake wakachukia wakampindua wakati yuko Mwenye mapumziko Mwenye pwani moja nchi ni kwake .Walipompindua hao wahafidhina ilikuta wananchi wameonja kautamu ka Uhuru waliokosa muda mrefu. Ndipo aliyekuwa meya wa Moscow Yeltsin akakataa kuyatambua Mapinduzi ya Wahafidhina akasema yeye anaunda taiga la Russia ambayo Ndiyo ya Leo .Wanajeshi wakamuunga mkono tens alipanda juu ya kifaru cha jeshi kupinga mapinduzi ya kumng'oa Gorbachev na Mapombe akiwa amelewa chakari. Ilipotokea hivo na vile vinchi jumuishi vikaona navyo vijitenge na ukawa mwisho wa USSR kamailivojulikana maana Russia ya Leo Ndiyo sehemu kubwa ya iliyokuwa USSR. Wakagawna Mbao kila nchi ikajitangazia Uhuru.Lakini Gorbachev alikuwa na nia njema ya kukomboa Uhuru wa RAIA ila sasa matokeo take ndio hayo badala ya kukomboa ikawa ni kuvunja nchi. Nakumbuka wakati wabunge wa G 55 wanataka serikali 3 za jamhuri ya Tanzania MWL Nyerere aliwauliza kuwa mumeishaandaa Yeltsin wenu maana hakukuwa na uwezekano wa serikali tatu halafu Muungano wetu ukabaki kama ulivyo. Ndivo ninavoelewa kusambaratika kwa USSR. Na kwa kweli lilikuwa li nchi kubwa lenye mfumo kandamizi ikawa Politburo ya watu 13 wanaokaa Moscow ndio walichagua viongozi wa USSR yote. Kwa hali hiyo wananchi hawkuwa na mapenzi na Muungano huo ndio maana ilisambaratika wananchi wanashangilia. Na ukawa mwisho wa ukuta wa Berlin na Warsaw Pact maana zilishikiliwa na dude hill la USSR. ndivyo ninayoikumbuka hiyo mianzo ya 1990's
 
Mkuu ahsante sanaa kwa madini...
 
Naomba nichangie machache japo sio mtaalamu sana juu ya ufuatiliaji wa masuala ya historia.

Mkuu samaani kidogo naomba nikurekebishe katika historia hatutimii neno 'mnamo mwaka 1980s hadi 1980s' unaposema 1980s una maana ni mwaka 1980 hadi 1989 ni vyema ungesema mnamo mwa miaka ya 1980.

Pili mkuu umejikita zaidi kumzungumzia Joseph Stalin kama ndo mwanzilishi wa USSR na kuacha kabisa kumtaja Vladimir I Lenin ambaye ndiye aliyefanya mapinduzi ya mwaka 1917 chini ya chama chake cha bolshevik.

Tatu, haujaelezea kwa undani hizo sera za kigeni zilizoashishwa na Mikhael Gorbachev na zilijikita kwenye nini na nini sababu zilizomfanya Mikhael kuja na hizo sera.

Nne, mkuu umejikita zaidi katika kumuelezea Mikhael kuwa ndo kinara wa kuimaliza USSR na kuacha kuelezea sababu nyinginezo.
 
Pamoja na sababu hizo, Mfumo au sera ya Ujamaa na ukosefu wa Demokrasia ndani ya USSR vilichangia sana Yale Majimbo ya ndani ya USSR kujitangazia Uhuru!

USSR iliwekeza zaid kwny Siasa kuliko Uchumi, mfano Wao ndio walikuwa Wadhamini wakuu wa Vita kadhaa barani Africa wakitumia Kibaraka wao Julius Nyerere Mtawala wa Tanzania Miaka hiyo kupiganisha vita South Africa, Angola na Mozambique vita ambavyo sio tu vilichangia anguko lake bali pia la Kibaraka wao!
 
Kumwita Nyerere kuwa alikuwa kibaraka Wa mrusi ni matusi makubwa kwa mwanamapinduzi anayeheshimika dunia nzima. Nyerere alikuwa mjamaa kweli lakini ujamaa wake haukuwa kama urusi. Mrusi alikuwa na ujamaa wa scientific socialism lakini Nyerere hakuupenda aina hiyo ya ujamaa sababu alisema hakukuwa na Uhuru kwa wananchi wa nchi zenye scientific socialism hadi miaka hiyo waumini wakuu wa Sera ya mrusi walimwona Nyerere kuwa ni msalit Wa scientific socialism. Ieleweke Nyerere hakuwa mshabiki kabisa Wa Mrusi wala mchina na hata Silahaza ukombozi wa kusini mwa afrika alinunua huko kwa sababu asingeuziwa na nchi za magharibi halafu zikaue wazungu huko kusini. Kama unakumbuka wakati huo Tanzania alikuwa mwanachama Wa nchi zisizofungamana na nchi za magharibi au magharibi .Ni kweli kuwa Tanzania ilipata maumivu kwenye ukombozi lakini Ndiyo gharama ya MTU mwema anaweza kufa akienda kumsaidia Jirani aiyeingiliwa na majambazi. Wakati Fulani professor Mazrui alimsema Nyerere hivi, nanukuu ( On the question of liberation of Africa against foreign domination Nyerere has no equal but on the question of African unity he is a non performer). Hiyo ni statement ya msomi nguli aliyekuwa hasimu Wa Nyerere kisiasa maana Mazrui alikuwa muumini Wa ubepari mkamilifu. Hivi kweli kuzikomboa nchi hizo alifanya makosa hata kama tuliumia sana kiuchumi. Mbona baada ya Nyerere Hamna kiwanda kilichosimama licha ya kukumbatia ubepari kwa asilimia zote. Ubepari ni unyama tu hata tuupende vipi. Setback ya ujamaa kwa sasa ni sababu ya ubinafsi wa binadamu tu. Na usishangae miaka 100 ijayo ubepari utafutika maana mfumo ambao Leo matajiri kumi wa kumi wa kwanza wanamiliki nusu ya uchumi wa dunia so mfumo endelevu lazima binadamu ataukataa muda muafaka ukifika. Jiulize kwa nini matajiri sasa hivi wanahamasishana watoe nusu ya utajiri wao kusaidia maskini ili dunia iwe nafuu kuishi. Na hiyo ndiyo imani ya mwalimu kuchukia ubepari lakini hakuchukia matajiri kama tunavyoa minishwa Leo. Mbona akina sir Andy Chande walikuwa marafiki zake..Tena baadae MWL Nyerere alikiri kuwa approach ya ujamaa alikosea maeneo kadhaa kama kutaifisha madukaya nyama. Nadhani MWL kwa uzalendo, ubinadamu, upendo na mema mengine hana mfano , alikuwa wa kipekee kabisa.
 
USSR iliwekeza zaid kwny Siasa kuliko Uchumi, mfano Wao ndio walikuwa Wadhamini wakuu wa Vita kadhaa barani Africa wakitumia Kibaraka wao Julius Nyerere Mtawala wa Tanzania Miaka hiyo kupiganisha vita South Africa, Angola na Mozambique vita ambavyo sio tu vilichangia anguko lake bali pia la Kibaraka wao!
unaona hii haikuwa na manufaa? ulikuwa inafurahia wenzetu kule Mozambique, South Africa, Angola, Zimbabwe, Ushelisheli na kwingineko Afrika waendelee kutawaliwa na wazungu? Naona kaubinafsi katika andiko lako.
 
Back
Top Bottom