Kuvunja poverty circle sio kitu rahisi

Mimi sikubaliani na TIBIM kuwa eti mtu ukipanda miti ekari100 baada ya miaka15 mkivuna miti mnakuwa matajiri kuliko kupoteza miaka yako 15 ukisoma.Ataniwia radhi ni maoni tu.Elimu ni ufunguo wa maisha.Hakuna kitu kibaya ukiwa masikini halafu tena na elimu uwe huna.Hiyo habari ya kupanda miti ni mawazo tu unaweza kuta hata hiyo ekari100 huna na au ukapanda miti yote ikafa.Namnukuu mhe Flani raisi wetu awamu ya flani alipataga kusema ''Wazazi wa Maradhi ni Ujinga na Umasiki,Ujinga ni baba yao na Umasikini ni mama yao''(Mwisho wa kunukuu).

Ukiwa huna elimu kabisa kila kitu unafikiria umelogwa na unaendesha mambo yako kama meli isiyo na usukani matokeo yake maradhi na umasikini juu.Hivi unafikiri matajiri tulio nao Mfano Mzee wa IPP na kijana MOD hawana elimu?.Mzee wa IPP ana shahada ya udakitari na ni moja ya watu wachache wenye cheti cha charter cha wingereza hapa nchini.Kijana MODi ana shahada ya pili ya uchumi amesomea Marekani,Mzee wa watu wa Juice,Unga n.k anaweza kuwa hana elimu kubwa lakini amesomesha wanawe kwa elimu za juu sana kwa kuona umri wake mkubwa na wanawe wanamsaidia kupanua biashara na nyie mnaona.

Ni kweli wako matajiri walio na utajiri bila elimu ila ukiona wanavyoendesha mambo yao utasikitika sana.Unakuta mtu anaungulia ndani na pese kwenye magunia.Eleweni kuwa hata matajiri wakubwa wasio na elimu kuendesha mambo yao wanatafuta wasomi.Na walio wajanja wanaanza kusoma baada ya kugundua walichokosa maishani na wengine siwataji wameshafikia hata ngazi ya udaktari wa falsafa.Unakuta mtu ana ng'ombe 5000 lakini analala kwenye ngozi ya ngombe na hali nyama anachinja siku ngombe akifa au kukiwa na msiba.

Eleweni haiwezekani watu wote tukawa matajiri nani atamtuma mwenzake na nani atamuajiri mwenzake?.Matajiri mnao waona Marekani msije dhani hawana Elimu kama kina Trump na huyu tajiri wa Africa Aliko Dangote.Niwieni radhi kidogo nitataja mikoa yenye maendeleo mkoa flani wa kaskazini,mkoa flani wa kusini magharibe na na mkoa flani wa magharibi maendeleo yao japo hawana rasilimali yeyote ya kuwekeza au ardhi kubwa sana lakini wameendelea kutokana na Elimu sio maisha ya kubahatisha bahatisha.

Ili kuvunja CIRCLE ya umasikini kitu cha kwanza kabisa ni kutoa UJINGA kwa elimu mambo ya bahati yatafuatia hiyo ni mipango ya mungu sio kusema mbona fulani hajasoma lakini ana mali ni kujidanganya bahati ya mwenzio usilalie mlango wazi.

Kinachosababisha CIRCLE ya umasikini isikatike ni UJINGA(kukosa elimu) baba akiwa hajasoma kabisa akizaa mtoto naye anajiwa na ujinga wakusema mbona baba hajasoma mimi nisome nini sasa.Mtoto ana pass ujinga huo kwa wanawe na wanawe kisa mtasingizia laana au shetani SHETANI wetu ni ujinga wa kukosa elimu.Kwa ujinga mtu alio nao mtu anaoa wake wanne huku akijua ni masikini unategemea nini watoto wanazaliwa kwenye lindi la umasikini.Bahati mbaya baba akiondoka bado anaacha watoto kwenye lindi la umasikini kizazi na kizazi wanapasiana ujinga.

ELIMU inamkomboa mtu kutokuwa masikini wa kutupwa(ABJECT POVERTY) pia inamfanya mtu awe na uwezo wa kati sio chini sana wala juu sana.Sasa usiende shule kabisa utegee utakua kama flani utasubiri mpaka jua linazama.

Kitu kingine niwaase watanzania wenzangu.Kuna dhana imejengeka kuwa mtu anasoma ili aajiriwe.Hii pia ndio inachangia kuwafanya wasomi wasipige hatua kimaendele.Mtu unasoma ili uelimike upambane na hali yako serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu wa kila sekta na hata sekta binafsi imefikia hapo.Hiyvo chonde msikate tamaa kutokusoma kisa sitaajariwa afterall kuajiriwa ni utumwa.Tumia elimu na maarifa uliyopata kujiajiri mwenyewe.

Naomba kutoa hoja
 
Last edited by a moderator:
Kwangu mimi nacho amin kipaji pekee alicho nacho mwanangu ndo kitamfanya atoboe maisha, jukumu langu ni kumuendeleza tu. na kumfanya aishi kwenye ndoto zake.
Hakikisha unainvest sana ktk hilo maana vipaji kwa Tanzania bado sana, miundombinu si rafiki, bila kusahau elimu pia maana kipaji bila elimu in changamoto!
 
Hii iko applicable sana katika dunia ya tatu ambapo fursa kwa mtoto wa masikini zimebanwa mno lkn kwa dunia ya kwanza opportunities za kujikwamua hata kwa mtoto wa masikini ni nyingi tu.
Noted
 
Thanks for visionary thought
 
Tuendelee tu kupambana tu mkuu
 
Kwangu mimi nacho amin kipaji pekee alicho nacho mwanangu ndo kitamfanya atoboe maisha, jukumu langu ni kumuendeleza tu. na kumfanya aishi kwenye ndoto zake.
Endelea kumuandaa dogo
 
Of coarse, watu husema ukitaka kuwahi kimbia mwenyewe
 
True lkn kusoma ni Pesa,elimu sio bure ni ghali,nachomaanisha kwamba upate MAARIFA ya kuzalisha kwamba,then ukipata kipato ndo uwekeze kizazi kwenye elimu,ukipata kipato watoto watasoma vizuri. Tungekuwa na mfumo wa elimu bure kama wenzetu,ingeaaidia kupunguza umasikini.
 
Kuvunja mfumo huu wa kijamaa ni maamuzi magumu, kwani itakulazimu uonekane kichaa Kwanzaa kwa ndg na jamaa.
True hio nayo ni mbinu, unaweza ukajinyima na kuonekana mbaya kwa ndugu Kuwa utoi msaada, then mbeleni ukishasimama ndo uanze kuwasidia
 
MAARIFA yapo mengi sana ya kujikwamua na umasikini, shida unaweza ukawa na MAARIFA ukakosa Pesa ya kuligeuza Wazo kuwa Pesa. Mfano Kilimo kinataka zana na vitendea kazi ambavo lazima uwe na Pesa ili uvipate.
 
Hapo ni ishu za energy...... Like attracts..
 
MAARIFA yapo mengi sana ya kujikwamua na umasikini, shida unaweza ukawa na MAARIFA ukakosa Pesa ya kuligeuza Wazo kuwa Pesa. Mfano Kilimo kinataka zana na vitendea kazi ambavo lazima uwe na Pesa ili uvipate.
Sure
 
Familia nzima ikiwa inamtegemea mtu 1, ikitokea huyo mtu akadondoka, basi familia nzima inadondoka.... Distribution of wealth ni nzuri katika familia na capitalism ni nzuri kwenye familia kuliko socialism
 
Sasa nimekupata TIBM wazo lako zuri tuendelee tu kuelimishana kiungwana
 
Hua siamin sana kwamba elimu yaweza kuvunja poverty cycle,binafsi nimewai kujikuta kwenye hilo janga tena nikiwa na umri Mdogo (sio kama uliemtolea mfano maana yangu hayakua makubwa ivyo)
mm nilikataa shule tena kwa herufi kubwa baada tu ya elimu ya msingi na kuamua kuzamia dunian kukombua kile kilichokua kinaangamua..ya Mungu ni mengi kwa msaada wake nimefanikiwa kuvunja hyo poverty cycle

Sio kazi rais kabisa kuvunja mkataba na umasikin unaitaji kuagana na nafsi, kupamba na umasikini ni sawa kabisa na kupambana na shetani unatakiwa kupambana kiroho(kumuomba MUNGU) na kimwili!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…