Napongeza kuvuliwa madaraka wakuu wa shule za sekondari zilizofanya vibaya hata kama zipo sababu zilizo nje wa uwezo wao. Napendekeza na Afisa elimu wa mkoa wa Dar es salaam na maafisa elimu sekondari wa wilaya Msalala, Kisarawe na Morogoro(V) pamoja na wilaya kumi za mwisho wavuliwa madaraka. Afisa elimu mkoa ashushwe awe wa wilaya na wale wa wilaya wakawe wakuu wa shule. Sababu wa Dar es Salaam shule zake nyingi kuwa za mwisho, maafisa elimu sekondari wilaya hizi, wilaya zao kufanya vibaya ukilinganisha na mwaka uliopita. Wilaya za kumi za mwisho (Rufiji, Mafia,Bahi, Korogwe, Ruagwa, Musoma, Liwale, Nanyumbu, Kusini na Nachingwea. Wafuatao wapate pongezi Afisa Elimu mkoa wa Njombe na maafisa elimu sekondari wilaya ya Wangingombe, Njombe na Ludewa zote za mkoa wa njombe wamepandisha ufaulu ukilinganisha na mwaka jana. Wengine wa kupongezwa ni wilaya kumi za kwanza.