Nafikiri cha kuangalia kwanza ni wakati gani wa kuvaa kifaa cha kujikinga na ajali au kuokoa maisha.
Kwa gari ni sahihi kufunga ukanda ukiwa safarini, kwa baiskeli na pikipiki ni kuvaa helmet.
Kwenye anga na majini kunavaliwa maboya ya kuokoa maisha. Katika baadhi ya boti za kasi, maboya hayo huwekwa chini ya kiti na abiria na kabla ya boti kuondoka mnafahamishwa namna ya kuvaa na kuoneshwa njia gani muelekee inapotokea ajali, yaani kuelekea kwenye vihori (boti ndogo) zilizomo ndani ya boti au meli. Kwenye boti na ndege abiria havai maboya hayo hadi pale tu inapotokea ajali.
Tatizo lipo katika hizi feri zetu (tunzoziita meli) ambazo mara nyingi huwa ni za abiria na mizigo, wakati meli hasa (za cruise), utaratibu nikama nilioueleza kwa boti za kasi; lakini katika feri zetu mambo ni shaghalabghala kwa sababu kadhaa zifuatazo:
1. Kupakia abiria (na mizigo kupita kiasi), kiasi kwamba inapotokea ajali, hakuna maboya ya kutosha kwa abiria wote.
2. Feri nyingi ni chakavu lakini huruhusiwa kufanyakazi bila ya kujali usalama wa abiria.
3. Pamoja na uchakavu wa chombo, kunakuwa na uchakavu na uchovu wa mabaharia ambao ni mabaharia jina tu, wengi wao hawana elimu ya kuwaruhusu kufanyakazi humo, bali ni marafiki na jamaa wa wamiliki au waliojiriwa kwa kujuana na rushwa.
4. Hakuna ukaguzi wa mara kwa mara wa kitaalamu wa feri hizo, badala yake rushwa ndio cheti pekee cha kuonesha kila kitukiko sawa.
USHAURI: Ikiwa huna ulazima wa kupanda vyombo vya aina hiyo, usipande kwa sababu tu ya kutaka kujaribu.