Kuua upinzani hakuwezi kuisaidia CCM, Zanzibar ni CCM tu tangu 2015 , lakini matajiri wa kipemba ndio wanaiokoa kwa kuikopesha hela kulipa mishahara

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,854
218,579
Hili ni angalizo kwa wachovu wa akili na mawazo kutoka ccm , ni kwamba hizi kampeni mnazozifanya za kuua vyama vya upinzani kwa kutumia Bunge , ofisi ya Msajili wa vyama , RITA , Uhamiaji , Polisi pamoja na vyombo vingine vya dola haitaokoa ccm wala wapambe wake , ccm imekataliwa na Mungu , waganga na wachawi hawawezi kuiokoa .

Kwa mfano , Baada ya dhuluma ya 2015 kule Zanzibar na baada ya Jabali Maalim Seif kujiondoa kwenye kilichoitwa uchaguzi wa marudio , ccm ilijitangazia ushindi wa jumla wa 100% japo waliojitokeza kupiga kura za marudio hayo walikuwa 57 , 850 , hii ni baada ya Wazanzibar wenye haki ya kupiga kura KUTII agizo la chaguo na kipenzi chao Maalim Seif la kususia uchaguzi ule feki ambao mmoja wa waangalizi wa ndani alikuwa Ali Karume.

Lengo langu si kurudia yaliyopita bali nilikuwa najaribu kuweka kumbukumbu sawa , hoja yangu ni kuwajulisha mamluki na wanafiki wa ccm kwamba pamoja na ccm kuachiwa Zanzibar kwa 100% lakini imeishia kushindwa hata kulipa wafanyakazi wake mishahara , kiasi cha kuombaomba hela kwa wafanyabiashara wa Kipemba , wale wale wanaoitwa Hizbu ! hili ni jambo la kujifunza , kwamba kumbe hata tukikazana kuuwa vyama vingine na kubakisha ccm pekee bado hatutafanikiwa chochote , hii ni kwa sababu ccm imepigwa laana na Mungu mwenyewe , hii mipango mnayofanya ya kuuwa upinzani kwa uchawi na kwa kutumia dola haitaibadili laana mliyopigwa na Mungu , iangalieni Zanzibar kama darsa la kujifunzia , hamuwezi kufanikiwa hata kama mmejaa Kibri .

Nakala : JABIRI IDRISA
 
Duh...!, hoja nyingine jameni tuwe wakweli!, yaani SMZ iishiwe hadi ishindwe kulipa mishahara halafu ikakope kwa wafanyabiashara wa Kipemba?!. Ya kweli haya?!.

Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye serikali mbili, serikali ya JMT na SMZ, ZMZ iishiwe mtu wa kwanza kuambiwa ni JMT, na kama ni kukopa serikali huwa zinakopa kwenye mabenki, leo ndio kwa mara ya kwanza kusikia eti serikali imeishiwa hadi imeshindwa kulipa mishahara!, halafu inakwenda kukopa kwa wafanyabiashara!, please uongo mwingine, jaribu basi hata angalau kutumia uongo unaotaka kufanana na ukweli!.

Kitu kingine, kumbe siasa za Zanzibar ni territorial, kwa vile Pemba ilikuwa ngome ya CUF, hivyo Wapemba wote ni CUF?.
Hizo kura za CCM kule Pemba zilipigwa na nani?.

Mambo mengine jameni tuwe wakweli!.

P
 
Serikali ya JPM na CCM zikiwa inakazania ujenzi wa Tanzania ya viwanda vya uzalishaji bidhaa na huduma huko CHADEMA sasa wapo mbioni kukamilisha ujenzi wa kiwanda kikubwa sana duniani kitakachokuwa kinachakata na kuzalisha uwongo, uzushi na upotoshaji na mwezi huu kitazinduliwa na mwenyekiti wao taifa.

mada yako ilikuwa na lengo na kueneza chuki kwa serikali ya JMT dhidi ya SMZ kwamba hatuna msaada wowote kwao na muungano hauwasaidii, Hapo umeonesha udhaifu mkubwa kichwani kwako na huku ccm tunasema hiyo ni propanganda ya kipuuzi sana
 
JPM baba jitahidi ukomboe ndugu zetu wa damu! Fanya chemistry zako Wazanzibar waunge juhudi kisha kura ya maoni rasmi,tuwe nchi moja , uwe mkoa rasmi wa Bara. , toa tu ahadi daraja Tanga hadi Pemba, Dar hadi Unguja, umeme Wa Nyerere Rufiji bure.....
Utakumbukwa daima
 
Ww naye una kihelehele cha kuwashwa,kwani ww ni smz au ww ni mpemba au mzanzibar?umeshupaza shingo kbsa kwenye keyboard unaandika kujibu eti mwenzako muongo,toka umekuwamfuasi wa shetani umeshakuwa shetani kazi yako kubwa sasa ni kuitetea ccm umemzidi hadi polepole.
Duh...!, hoja nyingine jameni tuwe wakweli!, yaani SMZ iishiwe hadi ishindwe kulipa mishahara halafu ikakope kwa wafanyabiashara wa Kipemba?!. Ya kweli haya?!.

Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye serikali mbili, serikali ya JMT na SMZ, ZMZ iishiwe mtu wa kwanza kuambiwa ni JMT, na kama ni kukopa serikali huwa zinakopa kwenye mabenki, leo ndio kwa mara ya kwanza kusikia eti serikali imeishiwa hadi imeshindwa kulipa mishahara!, halafu inakwenda kukopa kwa wafanyabiashara!, please uongo mwingine, jaribu basi hata angalau kutumia uongo unaotaka kufanana na ukweli!.

Kitu kingine, kumbe siasa za Zanzibar ni territorial, kwa vile Pemba ilikuwa ngome ya CUF, hivyo Wapemba wote ni CUF?.
Hizo kura za CCM kule Pemba zilipigwa na nani?.

Mambo mengine jameni tuwe wakweli!.

P
 
Wanataka kuua upinzani? Kwa hiyo kupingana maovu na kushindwa kwa serikali hawataki kuwe kwa mdomo sio?
Nyerere na chama kimoja ali survive majaribio takribani manane kwa vile waliopinga hawakuwa na pakusemea.
Jee hawa wa sasa yakiwa mambo ni hivyo uwezo wa Ku survive hata jaribio moja wanao?
Au kipigo cha mbwa koko na kuchakazwa kina weza kwenda hata kwa wajeda wakiamua ku legalize Zimbabwe au Sudan style?
Waache huo mpango wa kidhalimu
 
Serikali ya JPM na CCM zikiwa inakazania ujenzi wa Tanzania ya viwanda vya uzalishaji bidhaa na huduma huko CHADEMA sasa wapo mbioni kukamilisha ujenzi wa kiwanda kikubwa sana duniani kitakachokuwa kinachakata na kuzalisha uwongo, uzushi na upotoshaji na mwezi huu kitazinduliwa na mwenyekiti wao taifa.

mada yako ilikuwa na lengo na kueneza chuki kwa serikali ya JMT dhidi ya SMZ kwamba hatuna msaada wowote kwao na muungano hauwasaidii, Hapo umeonesha udhaifu mkubwa kichwani kwako na huku ccm tunasema hiyo ni propanganda ya kipuuzi sana
Mkielezwa ukweli mnaingiza upumbavu
 
Ww naye una kihelehele cha kuwashwa,kwani ww ni smz au ww ni mpemba au mzanzibar?umeshupaza shingo kbsa kwenye keyboard unaandika kujibu eti mwenzako muongo,toka umekuwamfuasi wa shetani umeshakuwa shetani kazi yako kubwa sasa ni kuitetea ccm umemzidi hadi polepole.
Mkuu Swelana, Mtanzania Mzalendo wa kweli wa taifa hili akisikia SMZ inazushiwa urongo, hatuwezi kunyamaza kwasababu Pemba ni sehemu ya JMT. SMZ ni miongoni mwa serikali mbili za JMT, haiwezi kuishiwa
Hadi kukopa kwa Wapemba wakati Benki la Baba la Baba pale BOT, lipo pale Zanzibar na limejaa minoti.
P
 
Duh...!, hoja nyingine jameni tuwe wakweli!, yaani SMZ iishiwe hadi ishindwe kulipa mishahara halafu ikakope kwa wafanyabiashara wa Kipemba?!. Ya kweli haya?!.

Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye serikali mbili, serikali ya JMT na SMZ, ZMZ iishiwe mtu wa kwanza kuambiwa ni JMT, na kama ni kukopa serikali huwa zinakopa kwenye mabenki, leo ndio kwa mara ya kwanza kusikia eti serikali imeishiwa hadi imeshindwa kulipa mishahara!, halafu inakwenda kukopa kwa wafanyabiashara!, please uongo mwingine, jaribu basi hata angalau kutumia uongo unaotaka kufanana na ukweli!.

Kitu kingine, kumbe siasa za Zanzibar ni territorial, kwa vile Pemba ilikuwa ngome ya CUF, hivyo Wapemba wote ni CUF?.
Hizo kura za CCM kule Pemba zilipigwa na nani?.

Mambo mengine jameni tuwe wakweli!.

P
Tulianza kusoma habari za THOMASO kabla hata hujazaliwa
 
Serikali ya JPM na CCM zikiwa inakazania ujenzi wa Tanzania ya viwanda vya uzalishaji bidhaa na huduma huko CHADEMA sasa wapo mbioni kukamilisha ujenzi wa kiwanda kikubwa sana duniani kitakachokuwa kinachakata na kuzalisha uwongo, uzushi na upotoshaji na mwezi huu kitazinduliwa na mwenyekiti wao taifa.

mada yako ilikuwa na lengo na kueneza chuki kwa serikali ya JMT dhidi ya SMZ kwamba hatuna msaada wowote kwao na muungano hauwasaidii, Hapo umeonesha udhaifu mkubwa kichwani kwako na huku ccm tunasema hiyo ni propanganda ya kipuuzi sana
Huna hoja na wala hujui chochote
 
Mkuu Swelana, Mtanzania Mzalendo wa kweli wa taifa hili akisikia SMZ inazushiwa urongo, hatuwezi kunyamaza kwasababu Pemba ni sehemu ya JMT. SMZ ni miongoni mwa serikali mbili za JMT, haiwezi kuishiwa
Hadi kukopa kwa Wapemba wakati Benki la Baba la Baba pale BOT, lipo pale Zanzibar na limejaa minoti.
P unauchungu na Zanzibar kuliko Tanganyika,.. Kila uzi unaohusu Zanzibar lazima uchangie..

Kaka Zanzibar ni ya Wazanzibari, ukweli mchungu, kweli hizi nchi zimeungana lakini utamaduni na mila za watu hazifanani..

Wazanzibari wanawaita Watanganyika "washenzi", tunayaona yanayotokea Upande wa Tanganyika ni ushenzi mtupu
 
Duh...!, hoja nyingine jameni tuwe wakweli!, yaani SMZ iishiwe hadi ishindwe kulipa mishahara halafu ikakope kwa wafanyabiashara wa Kipemba?!. Ya kweli haya?!.

Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye serikali mbili, serikali ya JMT na SMZ, ZMZ iishiwe mtu wa kwanza kuambiwa ni JMT, na kama ni kukopa serikali huwa zinakopa kwenye mabenki, leo ndio kwa mara ya kwanza kusikia eti serikali imeishiwa hadi imeshindwa kulipa mishahara!, halafu inakwenda kukopa kwa wafanyabiashara!, please uongo mwingine, jaribu basi hata angalau kutumia uongo unaotaka kufanana na ukweli!.

Kitu kingine, kumbe siasa za Zanzibar ni territorial, kwa vile Pemba ilikuwa ngome ya CUF, hivyo Wapemba wote ni CUF?.
Hizo kura za CCM kule Pemba zilipigwa na nani?.

Mambo mengine jameni tuwe wakweli!.

P
Wewe unapinga, una research yoyote uliyofanya ukaona alichokiandika ni uongo... Au ni mwendo wa kusifia sifia tu.?
P. Jielewe....
 
Duh...!, hoja nyingine jameni tuwe wakweli!, yaani SMZ iishiwe hadi ishindwe kulipa mishahara halafu ikakope kwa wafanyabiashara wa Kipemba?!. Ya kweli haya?!.

Tanzania ni nchi moja ya JMT yenye serikali mbili, serikali ya JMT na SMZ, ZMZ iishiwe mtu wa kwanza kuambiwa ni JMT, na kama ni kukopa serikali huwa zinakopa kwenye mabenki, leo ndio kwa mara ya kwanza kusikia eti serikali imeishiwa hadi imeshindwa kulipa mishahara!, halafu inakwenda kukopa kwa wafanyabiashara!, please uongo mwingine, jaribu basi hata angalau kutumia uongo unaotaka kufanana na ukweli!.

Kitu kingine, kumbe siasa za Zanzibar ni territorial, kwa vile Pemba ilikuwa ngome ya CUF, hivyo Wapemba wote ni CUF?.
Hizo kura za CCM kule Pemba zilipigwa na nani?.

Mambo mengine jameni tuwe wakweli!.

P
Standard accent
 
Japo umempinga ila kuna mahala ana Hoja na siyo Siri yupo Mpemba ( Mzanzibari ) Mmoja Tajiri sana si tu Tanzania bali hata Afrika ambapo Serikali yako ( hasa ile ya Awamu iliyopita ) ilipokuwa imeishiwa Pesa kabisa Hazina walikuwa wakimpigia Magoti kumuomba awakopeshe ili angalau Kwanza waanze Kuwalipa wale wa Makao Makuu ya Upanga ( ambao huwa hawana Masihara ) katika Kukinukisha nchini hasa pale wakicheleweshewa Mishahara yao wakifuatiwa na wale wa Makao Makuu ya Oysterbay ( ambao nao ni Moto ) vile vile kisha Watu wengine ( Kada zingine ) Malipo yao hufanywa taratibu kwakuwa wengi wao hawana Madhara kivile kama hayo Makundi mawili tajwa. Sijajua kama kwa Awamu hii bado huyo Mzanzibari Mpemba Tajiri bado huwa anafuatwa kuombwa akopeshe Pesa Serikalini kwani najua Serikali ya awamu hii inakusanya vizuri kabisa Kodi zake.
 
Back
Top Bottom