Kutwa nzima wanashinda baa wakicheza pool na kukata maji, Je wanatoa wapi pesa?

K 4 LIFE

JF-Expert Member
Jul 21, 2015
2,567
416
Wakuu,

Kuna hawa jamaa ambao kuanzia asubuhi mpaka jioni utawakuta baa wakinywa pombe na kucheza pool mpaka jioni.

Swali;- Hawa watu wanafanyakazi muda gani na wanapata wapi hizo pesa za kutumbulia mapombe na kuchezea pool?

Anayejua zaidi kuhusu hawa jamaa atujuze hapa.
 
wakuu embu njooni huku kuna hawa jamaa ambao kuanzia asubuhi mpaka jioni utawakuta bar wakinywa pombe na kucheza pool mpaka jioni, swali hawa watu wanafanyakazi muda gani? na wanapata wapi hizo pesa za kutumbulia mapombe na kuchezea pool? anayejua zaidi kuhusu hawa jamaa atujuze hapa.
Sana akiba zao Na hela za urithi, get busy man hii dunia hii kila mtu Na life lake
 
Tanzania kubwa ukifuatilia sana maisha ya watu yako utachelewesha!!! Mjini hapa oohh!! shauri zako
 
wakuu embu njooni huku kuna hawa jamaa ambao kuanzia asubuhi mpaka jioni utawakuta bar wakinywa pombe na kucheza pool mpaka jioni, swali hawa watu wanafanyakazi muda gani? na wanapata wapi hizo pesa za kutumbulia mapombe na kuchezea pool? anayejua zaidi kuhusu hawa jamaa atujuze hapa.
Wanafanya Kazi usiku wewe ukiwa umelala.
 
wakuu embu njooni huku kuna hawa jamaa ambao kuanzia asubuhi mpaka jioni utawakuta bar wakinywa pombe na kucheza pool mpaka jioni, swali hawa watu wanafanyakazi muda gani? na wanapata wapi hizo pesa za kutumbulia mapombe na kuchezea pool? anayejua zaidi kuhusu hawa jamaa atujuze hapa.
Umefuatilia usiku kucha wanafanya nini? labda ndio muda wa kutafuta pesa huo kwao. Pia yawezekana michongo yao ya kutafuta pesa haihitaji uwepo wao physically. Au pia inawezekana hapo wanapocheza pool na kunya bia ndio wanakuwa kwenye harakati za kutafuta pesa. You never know. There are endless possibilities. Anyways, najiwazia tu.
 
Mwaka juzi nilipita Mwanza pale mjini kati. Nilikuta watu wamelala pale kwenye garden ya stand ya kemondo na kwenye ile garden ya ofisi ya mkuu wa wilaya nyamagana, ilikua ni majira ya saa tano asubuhi. ha ha ha ha ha
 
labda wanafanya kazi shift za usiku, au wameachishwa kazi wanatumia pesa zao za akiba na za kubangaiza, yaani majibu ni mengi sana kwa hili swali lako maana unakuta mtu mwingine anafanya kazi siku 3 za wiki halafu zile 4 anakua bar, au ana duka au mradi mwingine ameajiri yeye anafunga hesabu usiku, au ni mtoto wa tajiri anakula na kupewa pocket money
vp kwani wewe ni mpelelezi au unawachunguza kwa sababu zako binafsi?
 
kuna jamaa mtaani kwetu alikua hana kazi lakini alikua anatoa ofa za bia na kila mwezi utakuta anabadilisha gari la kupigia misele
watu wakaanza kuzusha mara eti ni shoga
 
Watu wamekaa huko wakisubiria mikela yao itiki.
We endelea shangaa tu utashangaaa sana ila wao ni watu wazima wanajua kile wanafanya
 
real G. jaribu kufuatilia huyo shoga anafanya kazi gani,then urudi hapa
 
Back
Top Bottom