Kutumia kifaa cha android kama decoder

Kutumia kifaa cha android kama decoder

Pole na majukumu wanaJF pamoja na ufisadi wa Escrow

Naomba kufahamisha nawezaje kutumia kifaa changu cha android kama decoder kwenye tv, nina app moja nimeinstall katika simu nacheki mpira live na movies kibao je, ku a kifaa au namna naweza tumia badala ya kuangalia kwa kukodelea kwenye simu nikahamishia kwenye screen ya tv ????

Natanguliza shukrani za dhati kwa wataalamu wote

Mkuu hapo una app gan...?
 
Nafikiri changanya ushauri wa Chief hapo juu alokupa wakutumia Mini USB to HDMI

Vinginevyo kama hauwezi basi kuna option tatu hapo nimekutajia

1.IPTV receivers e.g srt 4922 ina bein sports zote bei yake 150,000/=
2.Laptop + Modem au Smartphone as Modem
3.Android TV boxes

Kazi kwako sasa
Mkuu, hiyo decoder inahitaji dish size gani? Na ni inashika all over Tanzania! Ili kuona hzo za BeIN utahitaji account au ni FTA.
Asante
 
hapa hatuongelei madishi tena tunaongelea Internet protocol TV ni wewe na bundle lako tu hapa unakula vitu
 
kipindi cha zamani cha symbian simu nyingi zilikuwa zinakuja na av cable au micro hdmi ili kuweza kuona content zako za simu kwenye tv ila sasa hivi oem wanaongeza tu processor na ram na kusahau vitu vya maana.

angalia simu yako kama ina micro hdmi kanunue huo waya halafu unganisha na tv yako. ila tv nayo inabidi iwe na hdmi pia.

Nokia-808-PureView-13.jpg

ikiwa haina hdmi hapo itabidi utafute adapter toka micro usb kuja hdmi

41MJMzbTnwL._SY300_.jpg

adapter hio hapo juu na waya wa hdmi utaweza unganisha simu na tv

pia simu za kisasa na tv za kisasa zinakuja na technolojia mpya inaitwa miracast kama vyote viwili vinavyo unaweza kustream kitu cha simu kwenye tv bila waya,

Mkuu Mkwawa naweza fanya hii kitu nikiwa na Lumia 920 na Tv ya LG?
 
simu za lumia hutaweza kwa njia za waya ila utaweza kwa njia zisizotumia waya.

kuna lumia beamer ambayo unastream vitu vyako kwenye tv lakini inahitaji tv yako iwe na internet na vyote tv na simu viwe vinatumia network moja.

ipo pia app ya nokia play to ambayo inatumia dnla inabidi tv yako iwe inasupoort hiko kitu.

search store app hizi
-lumia beamer
-lumia play to
 
hapa hatuongelei madishi tena tunaongelea Internet protocol TV ni wewe na bundle lako tu hapa unakula vitu

Dah, cc wa mikoa ya pembezoni wengi kwenye Iptv ni shida. Voda sanasana ndo wanapatikana na vifurushi vyao ni vya kuruka isitoshe net sio stable!
Ooh, Tanzania yangu.
Mafisadi Bring Back our Money for our Development
 
fanya research ya mahali ulipo, kwa mwaka mimi natembea mikoa mingi sana na sijaona hata mmoja wenye speed ndogo unless unakaa wilayani
 
Mkuu, hiyo decoder inahitaji dish size gani? Na ni inashika all over Tanzania! Ili kuona hzo za BeIN utahitaji account au ni FTA.
Asante

IPTV inatumia internet so all you need is internet conn. with speed basi!
 
simu za lumia hutaweza kwa njia za waya ila utaweza kwa njia zisizotumia waya.

kuna lumia beamer ambayo unastream vitu vyako kwenye tv lakini inahitaji tv yako iwe na internet na vyote tv na simu viwe vinatumia network moja.

ipo pia app ya nokia play to ambayo inatumia dnla inabidi tv yako iwe inasupoort hiko kitu.

search store app hizi
-lumia beamer
-lumia play to

Chief - Mkwawa , heshima mbele,

Iptv receiver zinapatikana wapi dar? Nikiwa nayo naweza kuangalia tv kwa bundles za kawaida?
 
kifaa chochote kile cha android/windows/osx/ios/linux kinaweza kuwa iptv receiver ilimradi kiwe kinauwezo wa kuunganisha na tv.

mfano unaweza nunua desktop halafu ukatafuta gpu ya bei rahisi kwa ajili ya hdmi, then ukaconect na tv kama iptv receiver.

kuhusu bundle huwezi tumia za kawaida unatakiwa uwe na internet yenye gb nyingi ikiwezekana iwe unlimited kabisa na iwe na speed kubwa
 
Nyie mnatumia tv zikoje? ni hizi za kawaida?
 
Pole na majukumu wanaJF pamoja na ufisadi wa Escrow

Naomba kufahamisha nawezaje kutumia kifaa changu cha android kama decoder kwenye tv, nina app moja nimeinstall katika simu nacheki mpira live na movies kibao je, ku a kifaa au namna naweza tumia badala ya kuangalia kwa kukodelea kwenye simu nikahamishia kwenye screen ya tv ????

Natanguliza shukrani za dhati kwa wataalamu wote

Mkuu,
Hapo kwenye RED, ni app gani hiyo?
 
Back
Top Bottom