Kutuko katika ukuaji wa kuku wangu

Mr JM

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
266
459
Kwanza niwe mkweli sijawahi kufuga chochote kile mwanzo na sina experience ndo nimeanza mwisho wa mwaka uliopita.

Iko hivi, mwezi Desemba mwanzoni tarehe 8 nilianza safari ya ufugaji wa kuku chotara. Nilikuwa nina mawazo ya kufuga kwa matumizi binafsi kupunguza kwenda sokoni kununua pale unapohitaji na nilikuwa motivated na kajamaa kanakouza vifaranga kuroiler wa 3 week akiwapromo wanakuwa wameiva after miezi miwili na siku chache tayar kwa matumizi.

Nikachukua wa kuanza navyo 100 akanambia chanjo fresh ila kuna moja akanambia niwape akanichukulia kwa 8,000 duka la dawa tukawawekea kwa jicho then nikachukua starter 40 kg ya harsho company.

Banda lilikuwa ni kichumba tu hakitumiki so niliwaweka tu mle safar ikaanza. Vyombo vya maji na chakula niliviandaa kabla, nikaanza ufugaji.

Bwana ulaji wao ulikuwa kawaida kwa kweli mana nliwawekea chakula cha kutosha na maji pia usafi kwa kweli sikuzingatia walikufa paka sasa 12 in series wamebaki 88 ndo nikaambiwa na jirani nizingatie usafi so nikawa nabadili maji na kuosha vyombo na banda kwa ujumla.

Tangu Desemba cha kunihuzunisha aisee hawa viumbe sijui vimedumaa yaani vimeongezeka kidogo yaani hawana tofauti na nilivyowanunua na miezi miwili imetimia jana. Kwa hesabu toka niwachukue kimsingi wana miezi mitatu kasoro siku 6 ila bado ni vifaranga.

Sasa kila nikiuliza majirani wanasema haiwezekani kuwe na kifaranga cha miezi hiyo. Mpaka ikafikia last week nikawa sinunui chakula maana nalisha locally chochote.

Aliyeniuzia nampigia simu yeye anasema mimi ndo nina tatizo kwenye chakula na huduma japo alinambia unaweza kuwatunza locally mara “ohhh maji ilitakiwa uchemshe daily” nikampotezea.

Hapa JFnajua kuna wajuvi wafugaji wenzangu waliobobea kwenye ufugaji wa kuku chotara. Je, ni kawaida huu ukuaji? Maana nilitegemea chotara anakuacharaka kiasi sababu anashare character na kuku wa kisasa.

Hebu nipeni mwangaza na msaada nakwama wapi ndugu zangu maana napata hasira kweli nikiwaona hawa viumbe natamani nivigawe ase ila nataka nione mwisho wao hata vikikua kwa miezi 8 sawa tu sasa nikiona kuku mkubwa namuheshimu mana najua amechukua process kufika alipo.

Nafugia Moshi natamani nishift hata kwa broiler wa wiki 5 sijui kama nao ni kweli au fix.

Msaada wenu
 
Hapo inaweza ikawa chakula

Au chanjo ya monyoo hawajapata



Maana minyoo inadumaza sana kuku
Chakula kipo sawa mkuu nanunua cha kampuni ya uhakika 1000/kg, kuhusu minyoo Inaweza ikawa sababu unaweza fafanua zaidi dalili za minyoo tofauti na udumavu.
 
Mkuu ninakushauri uwatembelee wafungaji angalau wa3 "waliofanikiwa" uwashawishi wawatembelee kuku wako ili hasa washauri tatizo litakuwa nini.

Kuna mambo makubwa mawili. Ubora wa chakula au ubora wa vifaranga ulionunua. Cross breeding isipofanywa na watu wenye maarifa ya kutosha huweza pelekea kupatikana vifaranga "visivyoeleweka".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Asante mkuu Nimewasiliana na Vet. Officer atanitembelea kesho kutwa du maana miez 3 just imagine still vifaranga si hasara tupu
 
Kama una eneo na limezungushiwa na lina majani wape chakula asubui tu halafu waachie wale kama kuku wa kawaida ila maji maji machafu yasiwepo nje.
 
Nitajaribu kuwaachia # Wakurochi mana wanakaa ndani daily
 
Nitajaribu kuwaachia # Wakurochi mana wanakaa ndani daily
Sasa vitamin zote utaweza kuwapa kwa kukaa ndani tu. Watakuwa wa kizungu hao ila wanaitwa wa kienyeji. Sababu ni mara ya kwanza endelea hivyo hivyo kwanza. Upate uzoefu.

Hayo matatizo uliyopata ni shule safi sana usione mbaya ili uki wekeza pakubwa tayari una nondo kichwani.

We huoni kuku wanaojifuga wenyewe wanatembea na vifaranga hawana usumbufu wowote.

Mi nafuga nawachia. Nawapa chakula asubui. Akija vetinary ongea nae sana pia kuhusu magonjwa ya virus kwa kuku ni usumbufu pia
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom