Guus
JF-Expert Member
- Jul 16, 2013
- 1,167
- 904
Wana JF,
Kama nilivyoandika katika "Heading", nina kama miezi mitano nimekuwa na shida ya kutoka jasho usiku nikiwa usingizini. Muda wote wa mchana na hadi pale ninapoenda kulala huwa sijisikii shida wala tatizo lolote. Lakini nikiwa usingizini basi ni kuhesabu masaa 3 hadi 4 lazima nishtuke, maana huwa nakuwa nimelowanisha shuka kwa kiwango cha kutia shaka (linakuwa halitamaniki tena). Kwa sasa nimeamua kulala na taulo pembeni, maana ninaposhtuka mwili huwa bado unajasho, kwa hiyo natumia taulo kujifuta. Kwa sasa siku zinazotokea kuwa sijatoa jasho usiku katika wiki ni za kuhesabika. Nimekwisha enda hospitali, na daktari alishauri nifanye check-up ya TB ambapo "Chest X-ray ikaonesha "normal", vipimo vingine ni HIV, Full blood count, Renal, Liver, Bone profile ambavyo vyote vipo "normal". Pia niliambiwa "thyroid function" ni "normal" na hakuna evidence yeyote ya kuonesha "Autoimmune disease". Hapa daktari ameniambia niwe na amani, kwa kuwa amejiridhisha na hayo yote basi kama kutakuwa na tatizo lingine litakalojitokeza nimfahamishe. Lakini aliniambia nisiwe na wasiwasi, ni vitu vinavyoweza kutokea kwa sababu ya mabadiriko ya mwili. Sasa shida yangu mimi ni kukosa "Comfortability"; kitendo cha kuingia kitandani na taulo na kushtuka usiku vinanikwaza sana.
Sasa madaktari humu mnisaidie ni nini laweza kuwa tatizo? Msaada wenu ni muhimu. Huyu daktari wangu ni muelewa sana, naweza shauriana naye kwa kutumia majibu yenu na akayafanyia kazi. Msaada wanajamvi.