Kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Deo Filikunjombe amuumbua Stella Manyanya

ane kilango kalala kama kigwangala sendeka ndo hana mpango kabsaaa njaa hiz

Ester Bulaya wapi,nilimsikia anajinyenyea siku ya Alhamisi, kumbe mnafiki mkubwa tu, heko Deo komaa hukohuko CCM unakisaidia chama
 
Safi sana mkuu nimeipenda. Filikunjombe hataishi muda mrefu CCM nyie sikilizeni.....ataachia jimbo arudi kwao agombee kwa tiketi ya CDM alafu arudi bungeni!
 
hizi post nyengine jamani, huku si kutaka kufitinishana na kuchochea ugomvi jamani ?
Mkuu unataka kulipeleka wapi taifa hili? kama kila anayesema ukweli tunamuita mfitini,anayetaja mambo ya kifisadi yanayotendeka ni mvunjifu wa amani wakati mwenye macho aambiwi tazama.Enzi za watz vipofu zimepitwa na wakati.Kila mtanzania mwenye uchungu na nchi hii achukie uovu na Biblia inasema hivi "HAKUNA AMANI KWA WATENDA MABAYA'' kwa nini tunawatakia amani wasiotaka kutenda mema? Hivi hivyo vitisho vya Stella manyanya vinayo tija kwa taifa? Nimpongeze Mh. Filikunjombe kwa kazi nzuri na ni mmojawapo wa wabunge wa watanzania wote bila kujali itikadi za kisiasa.
 
Mwaka jana kwenye bunge la bajeti siku Waziri Kaghasheki alipohitimisha bajeti ya Wizara yake kulikuwa na wachangiaji wengi. Siku hiyo neno "maandamano" lilitawala mijadala.

Mnakumbuka hadi Attorney-General akasema uangaliwe uwezekano wa ku-regulate maandamano.
Mmoja wa wachangiaji wa asubuhi ya siku hiyo alikuwa ni Mheshimiwa Deo Filikunjombe. Filikunjombe alichangia kwa hisia na hadi akalitangazia Bunge kuwa matakwa ya jimbo lake yasipotimizwa basi licha ya yeye kuwa mwana-CCM atawahimiza wananchi wa jimbo lake kufanya maandamano.

Mchangiaji wa mwisho kabla ya lunch break alikuwa Stella Manyanya. Alipoinuka tukadhani kuwa Manyanya ana mengi ya kuchangia kuhusu hoja iliyo mezani. Kumbe yeye hoja yake ilikuwa ni sentensi moja tu nayo ni kuhusu kauli aliyotoa Filikunjombe asubuhi.

Namnukuu Manyanya aliposema hivi "Huyu Deo Filikunjombe akumbuke kuwa maandamano siyo sera ya CCM, lakini akikaidi na kuendelea na hayo maandamano yake, basi asisahau kuwa mimi ni kiongozi wake katika NEC"

Kwa kauli kama ile ni kama Stella Manyanya alikuwa kama amemkata kilomolomo Filikunjombe kwa mambo kama haya. Ungetegemea kwamba Filikunjombe asingeibuka tena kwenye jambo lolote kubwa kwani NEC aliyomo Manyanya ni ileile yenye maamuzi mengi ndani ya CCM ikiwemo kuchagua wagombea ubunge wapya.

Lakini naamini kwa mshangao wa Manyanya na wengine wengi, sasa Deo Filikunjombe kaja na gia kubwa zaidi. Kubwa zaidi kwa maana ya kwamba maandamo aliyodhamiri kule jimboni ni kitu kidogo sanakuliko kitendo alichofanya sasa hivi.
Filikunjombe amenukuliwa akikiri kwamba ni mmoja wa wabunge waliohisiwa kuwa watasaini kwenye list ya Zitto ya kuleta hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu.

Yeye alivyoitwa alijua atashawishiwa ili asisaini. Ili kuwamaliza nguvu na kuwaonyesha kuwa sasa hajali litakalotokea basi akaamua kwanza aweke saini ndipo aende huko walikomwita.

Maana yake ni nini? Maana yake anaitwa ofisini mwa mawaziri huku tayari saini yake imeshaanguka karatasini.
Kingine ni kwamba ni mmoja wa wabunge wachache ambao wameamua kusaini huku wakipigwa picha ziende gazetini. Sasa, hapo utasema nini kwa mtu kama huyu Filikunjombe ambaye mlimkataza maandamano lakini sasa ameamua kushiriki kitu kikubwa zaidi tena ulimwengu ukimshuhudia.

Maana yake ni nini? Maana yake ni kwamba sasa hivi huwezi kumtisha kwamba NEC-CCM ndiyo inayochagua wabunge mwaka 2015. Analijua hilo na inaelekea yuko tayari kwa lolote. Labda tu sasa atishiwe uhai wake na kama itafanyika hivyo.

Kwa maana hiyo, enzi za mbinu kama za Stella Manyanya za kutishiana kuwa "utanitambua kwenye NEC" si tishio tena, kwani sasa hivi NEC si yao tu, nchi sasa ina NEC nyingi tu na zina nguvu kubwa kwa umma.

Pole sana Stella Manyanya na pole wote waliozoea kudhani tishio la rungu la chama ni dawa ya kuwa-discpline wabunge hata kwa kinachoonekana dhahiri ni maslahi ya taifa.

Taifa linahitaji watu kama Deo Filikunjombe, ujasiri wako unahitajika popote ama hukohuko CCM lakini ikishindikana uko milango ya dunia iko wazia kwako.

Weldone nikupateje for good presentation. Manyanya aliniconvince sana ya kuwa ni mtetezi wa wanyonge aliposaidiana na timu yake kumpiga chini mamvi lakini hii ya Filikunjombe imeonyesha rangi yake halisi. She cannot be trusted anymore.
 
Back
Top Bottom