Kutokuridhishwa na hatua zilizochukuliwa na zinazochukuliwa na Serikali kuhusiana na Corona

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
27,931
35,936
Nina wasilisha hoja hii miye kama mtanzania mwingine yeyote mwenye haki ya kutoa mawazo yake kwa maslahi ya nchi yake.

Ninaandika haya kwa uchungu nikifahamu pia kuwa kumekuwa na kutishana kusiko kuwa sahihi kwa watoa maoni hata wale wa nia njema tu kuhusiana na huu ugonjwa.

Hata hivyo ni mawazo yangu ya dhati kabisa kuwa itakuwa haina maana yoyote "kutopaza sauti" hata kama ni dhahiri dereva wa gari tulilomo atakuwa anatuelekeza kwenda kutumbukia mtoni.

Ikumbukwe, tumekuwa tukihamasishana siku zote kwa mabango na matangazo: "paza sauti kuzuia ajali, ajali zinaepukika".

Waungwana wanasema "penye wengi hakuharibiki jambo". Maana halisi ya kuwa, pamoja na mawazo kuwa tofauti penye wengi, ni dhahiri kuwa yatapatikana mawazo yaliyo bora zaidi yakatuvusha.

Hivi sasa tunakabiliwa na janga. Janga hili si letu peke yetu kama watanzania (in isolation). Hili ni janga la dunia nzima. Mataifa mbalimbali makubwa na madogo, matajiri na maskini sote tumekumbwa.

Ni kweli kuwa kutokana na lini ugonjwa huu umefika katika nchi gani, kiwango cha kuathirika kutoka nchi moja hadi nyingine kimekuwa ni tofauti sana. Itakuwa ni kujidanganya kudhani kuwa tuko vizuri kuliko kwingine hali kwetu ugonjwa huu hauna hata wiki 2.

Kote (kasoro ya China ulikoanzia) walianza kwa kisa kimoja kimoja kama sisi na baada ya mwezi hali yao leo haisemeki wala haitazamiki.

Hatua walizopitia hawa ambao leo hali hazisemeki ni hizi hizi tunazozipitia sisi leo, kwa maana ya kuwa tutapata matokeo hayo hayo tusipogutuka na kufanya kivingine. Na hali yetu yaweza kuwa hata mbaya zaidi kulingana na WHO inavyoendelea kuonya.

Anasema Albert Einstein: "Insanity is repeating the same mistakes and expecting different results". Mwisho wa kumnukuu.

Tulikuwa tunafanya kama walivyokuwa wenzetu wakati wa maonyo kuwa ugonjwa unakuja. Hawakufunga mipaka, ndege ziliendelea kuruka, shughuli za uchumi waliziweka mbele, hawakuweka wageni quarantine, nk nk. Waliendelea hivyo hadi ugonjwa ukawafikia.

Sisi nasi ilikuwa hivyo hivyo huku tukionywa hadi nasi ugonjwa ukatufikia.

Kama vile haitoshi na hata sasa tena tunaendelea kufanya yale yale yaliyowafikisha hapa wenzetu ambapo leo wanapokufa watu kwa mamia kwa siku. Ugonjwa ulipoingia maisha yaliendelea kama kawaida wakihamasishana kutotaharuki, kunawa nawa mikono, uchumi ulikuwa muhimu sana, mikusanyiko haikusimamishwa yote. Mengine kama: ibada, usafiri wa umma nk viliendelea.

Kimsingi hawakuwaweka wananchi wao kusalia majumbani ili kuudhibiti ugonjwa kikamilifu wakati maambukizi yakiwa yangali kidogo. Leo kiwango cha maambukizi kimepindukia na kuudhibiti usiendelee kusambaa sasa ni shughuli pevu kweli kweli.

Sisi nasi tunapita humo humo na huu ugonjwa. Mbaya zaidi hata tuna na imani za kukanyaga mafuta ya upako. Bahati mbaya sana tena, hii hata ni kutokea katika ngazi za juu kabisa. Yale yale ya babu wa Loliondo na kikombe chake.

Na sisi ugonjwa huu utatupeleka huko huko wataliano waliko, pengine hata kubaya zaidi kuliko wao kama tusipobadilika sasa.

Kwa common sense ya kawaida mno: ni muhimu sasa kukawa na mbinu tofauti kabisa ikibidi hata kuwa na watendaji tofauti. Mbinu ambazo serikali imekuwa inazitumia kupambana na huu ugonjwa kwa namna hii ni wazi kuwa haziwezi kutuvusha!

Afrika kusini wagonjwa waliothibitika wameongezeka mara 6 tokea ya waliokuwapo wiki jana kufikia 426.

Uganda wamefika 9 tokea 1 wa juzi.

DRC wamefikia 33 tokea kwa 1 wa wiki iliyopita.

Nk.

Siyo siri tena, takwimu zetu ni zenye kutiliwa mashaka makubwa. Inaonesha kuna msukumo wa kutoa taarifa zenye kijifariji zaidi kuliko uhalisia. Tumefikia kudhani Mungu ana sisi zaidi kuliko wengine. Sisi sote ni viumbe wake.

Truly, we shouldn't be going that low.

Tumekuwa kituko katika dunia inayo ona hatari ya wazi ambayo sisi kwa makusudi, viongozi wetu wanataka kuchagua kutokuiona na eti kutuaminisha sote hivyo. Huu siyo upepo ambao eti utapita pasipo na kuchukua hatua chungu kabisa. "No gain without pain". "No sweet without sweat". Mbona yote yanajulikana? Maisha hayawezi kuendelea kama kawaida hata kwa muda huu tu.

Tusidanganyane!

Tumetanguliza siasa zaidi. Kutetea matumbo yetu binafsi juu ya maslahi ya wote kama taifa. Ushauri kwa mkuu ya nini kifanyike, unapaswa kuwa huru hata kama ni mchungu vipi. Tunataka kuvuka hapa salama hilo tu ndiyo hitajio na sala yetu. Tunayo sehemu ya kufanya katika kufanikisha hili.

Ni wazi kuwa ugonjwa huu utakoma kusambaa kama watu watabakia majumbani. China wameushinda kwa njia hiyo. Vivyo hivyo Korea kusini wanaelekea kufanikiwa.

Rwanda tayari wanabakia majumbani. sasa wamebakiwa na siku 11 katika walizojiwekea. Afrika kusini wataanza alhamisi kwa wiki 3. Ramaphosa anasema ni sasa au athari zitakuwa mbaya zaidi!

Sisi ni watazamaji tu?

Ni vyema serikali yetu ikatambua kuwa hatua inazochokua na ilizoishachukua kwa kuzingatia uzoefu wote ulio kwisha onekana kuwa, hazijibu matarajio ya kuushinda huu ugonjwa. Hatuko katika njia sahihi ya kuumaliza. Sisi kama taifa tuko hatarini sana.

Ni muhimu sana wigo wa ushauri kwa mamlaka ya juu upanuliwe. Hili ni letu sote. Serikali isikilize hata isiyopenda kuyasikia kibinafsi au katika ujumla wake kwa maslahi ya taifa. Siyo siri tena kunatakikana mawazo mbadala na kwa hali ya dharura sana.

Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.

Ni muhimu kutambua hatujachelewa Ila muda unayoyoma. "Better late than never". Tunayo nafasi ya kushinda tusiitupe.

Kufanya mabadiliko kwenye wizara ya afya kwa sasa inaweza kuwa ni njia sahihi zaidi ya kwenda. Ni vyema Ummy akasaidiwa.

Vita hii ni kubwa na hata akiazimwa jenerali mwingine tokea TPDF yaweza kuwa muda muafaka kabisa. Kwanini majenerali hawa waende magereza magereza tu?

Wakuu tuyaangalie haya kwa mawazo wazi na thabiti, vinginevyo twafa tukijiona.
 
Tuendelee kunawanawa mikono

Sent using Jamii Forums mobile app

Inasikitisha sana. Si utamaduni wetu kuitisha mtu kuwajibika au kujiuzulu.

Muda muafaka kwa Ummy Mwalimu akapata usaidizi thabiti.

Mtukufu rais anahitaji ushauri wenye kutuvusha kwenye hili dhahama. Kusaidiana sote tukavuka hapa mbona itakuwa la maana mno.
 
Bila hata ya mabandiko yaliyopo mitandaoni ni wazi kuwa haihitaji elimu yoyote kubwa kutambua ugonjwa huu ukishaingia ni suala la muda tu kwa watu wengi sana kama si wote kuambukizwa, kama hatua stahiki hazichukuliwi.

Idadi ya watu walioambukizwa inapokuwa kubwa, kasi ya maambukizi inakuwa kubwa isivyomithilika.

Ugonjwa wa namna hii unaweza kudhibitiwa kikamilifu kwa namna moja tu. Hii ni ya kuwa weka watu wote wakatulia majumbani ili kutumia muda huo kuwabaini wote wenye maambukizi.

Si kweli serikali ya Tanzania iliyo sheheni waasomi vilivyo: wakiwamo na ma PhD yote yale kuwa eti hawaujui ukweli huu.

Ukweli mchungu, yaonekana kuna ukweli tunaofichwa hapa. Kwa nini ujasiri huu wa kutuweka hatarini kiasi hiki?

Labda muda muafaka sasa badala ya kukumbuka umuhimu wa lockdown iwe kutafuta sababu ya kuficha ficha huku.

Ni kitu gani serikali inasubiri kabla ya kutangaza total lockdown? Nchi zingine zinafanya hivi sisi tu?

Fumbo mfumbie mjinga mwerevu atang'amua.
 
brazaj unajitahidi kuisihi serikali kwa hili la corona. Ila hebu tuiache serikali nayo ifanye kazi yake tukianza kufa mfululizo ndo tuilaumu.
 
Acha ujuaji wewe ungekuwa Raisi ungeweza kuizuia Corona isiuwe wananchi?pia tambua katika watanzania 5 watatu kati yao ni vichaa, Hivyo katika comments 5 tatu ni za Vichaa.

Aliyefanya huu utafiti mungu anamuona....katika members 5 wa Jf wa tatu wanaugua ukichaa na katika moods 5 watatu wanaakili zilizopitiliza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
brazaj unajitahidi kuisihi serikali kwa hili la corona. Ila hebu tuiache serikali nayo ifanye kazi yake tukianza kufa mfululizo ndo tuilaumu.

Well said. Thanks.

Ila wanasema: "asiyejua kufa, aangalie kaburi".

Acha tusubiri vifo badala ya kutambua makaburini kuna wafu ili kufahamu nini maana yake.
 
Sijui kwann nahisi Corona ilishakuja Tanzania kitambo. Kuna homa ilianzia Dar Dec 2019 watu wakaumwa kama dalili ya Corona. Mimi nipo mkoani ile homa ilinipitia tuliumwa nyumba nzima. Mtoto wangu mdogo mpaka alilazwa wk nzima na alipata mpaka nimonia. Kuchwa kinauma mfululizo hakisikii dawa, homa kali maumivu ya kifua na misuli. Yaani dalili zile zile za Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sijui kwann nahisi Corona ilishakuja Tanzania kitambo. Kuna homa ilianzia Dar Dec 2019 watu wakaumwa kama dalili ya Corona. Mimi nipo mkoani ile homa ilinipitia tuliumwa nyumba nzima. Mtoto wangu mdogo mpaka alilazwa wk nzima na alipata mpaka nimonia. Kuchwa kinauma mfululizo hakisikii dawa, homa kali maumivu ya kifua na misuli. Yaani dalili zile zile za Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hako bila shaka kalikuwa ka upepo tu ndiyo maana kalipita salama. Mataifa haya Italy, Spain, nk yameendelea mno.

Kupoteza watu kwenye zaidi 700 kwa siku na ni mfululizo itakuwa si sahihi kudhani kuwa itakuwa kwenye huo ugonjwa mliowahi kuugua, au vipi mkuu?:

Huko Spain watu 738 wameaga dunia kwa masaa ishirini na minne. Wakenya na Watanzania tuwe makini ili majanga haya yasitupate - JamiiForums
 
  • Thanks
Reactions: Ilu
Ni kweli mkuu ila unafanana dalili basi. Inatisha sana watu 700 kwa siku.
Mkuu hako bila shaka kalikuwa ka upepo tu ndiyo maana kalipita salama. Mataifa haya Italy, Spain, nk yameendelea mno.

Kupoteza watu kwenye zaidi 700 kwa siku na ni mfululizo itakuwa si sahihi kudhani kuwa itakuwa kwenye huo ugonjwa mliowahi kuugua, au vipi mkuu?:

Huko Spain watu 738 wameaga dunia kwa masaa ishirini na minne. Wakenya na Watanzania tuwe makini ili majanga haya yasitupate - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha ujuaji wewe ungekuwa Raisi ungeweza kuizuia Corona isiuwe wananchi?pia tambua katika watanzania 5 watatu kati yao ni vichaa, Hivyo katika comments 5 tatu ni za Vichaa.

Aliyefanya huu utafiti mungu anamuona....katika members 5 wa Jf wa tatu wanaugua ukichaa na katika moods 5 watatu wanaakili zilizopitiliza

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu wewe katika hao 5 uko upande upi?

Isije kuwa yale ya nyani asiyeona ku**ule.

Usisahau na zile tafiti za TWAWEZA zote zinatuhusu au siyo?
 
Bado hatujawa serious!

Minada/Magulio ya kila wiki bado yanaendelea.

Makanisa yenye ibada mara tatu kwa wiki bado wanaendelea hivyo hivyo tu na mazoezi ya kwaya kila siku.

Usafiri wa umma ndiyo kabisa.

Jana DC G.Gondwe kawaambia bodaboda wawe wanaosha helmets za abiria kabla ya kumpa abiria mwingine.😁
 
Back
Top Bottom