Waswahili wenzangu tuchukue tahadhari na mlipuko wa kipindupindu

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
7,177
7,750
Mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu upo kwenye mazingira yetu, hii imechangiwa na mvua nyingi kunyesha hivyo baadhi yetu tumeamua kwa maksudi kufungulia chemba za kinyesi kutiririka ovyo!! tunao kula magengeni haswa wakazi wa Jiji la DSM tuwe makini. Mama ntilie osheni vyombo vyenu na maji ya moto pia zingatieni usafi wa mazingira.

Kwa ujumla sisi sote kila mmoja kwenye eneo lake tunapaswa kusafisha mazingira yetu ili kuepuka na ugonjwa huu wa kipindupindu lakini pia maradhi mengine ya mlipuko.

Pamoja na hayo tuendelee kuelimishana juu ya sababu na jinsi ya kuepuka/kujikinga.

Jambo la msingi tuzingatie usafi, tunapo kula na tunapo kunywa.

Tuache kutiririsha kinyesi wakati huu wa mvua, haswa maeneo ya tandale, sinza,mbagala, n.k
 
Back
Top Bottom