Kutoka Washington, USA: President Magufuli, Stop That Dam

Kutoka Washington, USA: President Magufuli, Stop That Dam

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
52,672
Reaction score
103,598
Bado dunia inaomba, inambembeleza Mh. Rais Magufuli asimamishe/aachane kabisa na ujenzi wa bwawa la Stieglers Gorge. Wanasema athali zake ni kubwa kuliko matumaini yaliyowekwa kwenye huo mradi.

Quote:
Maritta Koch-Weser "If construction of Stiegler’s Gorge Dam in Tanzania goes ahead, it would squander the nation’s tremendous natural endowment and its finances for years to come".

My take: Tuwasikilize hawa, tukae nao meza moja, tusikie maoni yao na sisi wasikie ya kwetu. Tuondoe dhana ya "mabeberu" angalau kwa hili. Tukitoka hapo tunakuwa na hoja za kufanya tunaloliamini. Tuepuke "lawama za wabia wetu wa maendeleo ulimwenguni" kwenye mradi huu maana tutakuwa na hoja za msingi kujibu madai yao akina WWF, UNESCO na wengine.

Sitatafusiri kwa Kiswahili, mwenye kujua Kizungu asome. Naweka Link. Interesting to read.

President Magufuli: Stop That Dam - The Globalist
 
Tungeanza kwanza kufunga viwanda vyao vikubwa.

Tukitoka hapo, wasitishe urutubishaji wa uranium na utengenezaji wa nuclear based warfare.

Wangepunguza na upelekaji wa vifaa mbalimbali angani ambapo sasa mabaki yamebaki just beyond the exosphere yakijazana mbele ya uso wa dunia.

Uchimbaji wa mafuta ungesitishwa ili kuzuia matumizi yake kupitia uchomaji wake unaoharibu mazingira.

Halafu sasa, baadae wakimaliza hayo, waje tuongee na sisi tuchukue hatua kwa upande wetu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waache ujinga,, wao watuonyeshe walivyoprotect mazingira yao, wanajua kabisa hamna maendelo bila umeme wa uhakika, kwa hiyo wakitubana kwenye hilo tutaendelea kuwa tegemezi.

Tuunge mkono asilimia mia ujenje wa Bwawa hili. Ni kwa maendeleo yetu. Mbona huwa hatujifunzi? Mara ngapi tumekuwa tukilalamila mgao wa umeme?

Tuunge mkono basi ujenzi huu maana ndo utaondoa adha hii. Tutakuwa na umeme wa uhakika, viwanda vitakuwa na umeme wa uhakika na kwa bei nafuu. Means hata production cost itakuwa chini tutakuwa competitive.

Wawekezaji watakuja maana wanauhakika wa energy for production..

Tusikubali kushikiwa akili,, au kupinga kila kitu. Mazuri tuunge mkono mabaya tuyapinge kwa nguvu zote..

Kama mbuga tunazo nyingi tuu,, nyingine kubwa karibiana nchi zao..
 
Si tuzalishe hata umeme wa upepo na solar bila kuharibu mazingira.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanini nini maana ya kuwa na nchi na kuwa na kiongozi pia kuweka mipaka na sisi tunahaki ya kufanya tunayoyataka kuna MTU aliwapigia kelele kuhusu vinu vya nuklia mbona sisi wanatupigia kelele waachane tujikwamue umeme ukiwepo mzuri hata viwanda vitakuja tena vya maana maana malighafi tunayo shida inatoka wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusikubali kushikiwa akili,, au kupinga kila kitu. Mazuri tuunge mkono mabaya tuyapinge kwa nguvu zote..
Hakuna anayepinga, nimeleta muone what they say about us! basi, si kwa nia ya kupinga!
 
Stigliers Gorge lazima ijengwe..!! Nyie wake za mabeberu mkome, and the area for construction is just less than 1% ya Selous Game Reserve..!! Sisi na USA in comparison nani anaharibu sana mazingira ya dunia hii? Nuclear tests zao na mabomu lukuki, they don't have guts za kutusema sisi kwa utunzaji wa mazingira. Acheni ku exaggerate vitu msivyovijua kisa nyie wapinzani wa Mh. Rais..!! Tunahitaji umeme cheap, na hilo haturudi nyuma, pumbaf
 
Hawa mabeberu ni hatari sana wanaona tukifanikiwa huu mradi hawataweza tena kutuuzia magenerata na mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi wanataka tuendelee kuwa tegemezi ili waendelea kunufaika na kutuuzia magenerata na mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi. Wajerumani walianza kupinga huu mradi kwa sababu wao ndio watengenezaji wa mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi, mitambo yote ya Kinyerezi 1 hadi 4 yote ni mitambo kutoka Ujerumani, tukianza kutumia umeme wa maji hawataweza tena kutuuzia hii mitambo ya gesi. Aggreko na Symbion yote ni magenerata ya kuzalisha umeme kutoka Marekani na wao watapata hasara tukianza kutumia umeme wa maji. Hii ni vita ya kiuchumi si ya kimazingira na kama wanapenda mazingira wangepinga uchimbaji wa dhahabu ambao umeacha uharibifu wa mazingira kupita kiasi.
 
Soma link utafakari. kuna sense kwa wanachokisema. Nani hapendi umeme?
Nimerudia tena kusoma hiyo article lakini bado mkuu wanazunguka pale pale!
Sijui tembo Mara mto hauna uhakika wa kuzalisha umeme KAMA vyanzo vya huo mto vitaendelea kukauka!

Ila hawapo tayari kutoa pesa kwa hizo vyanzo mbadala wanavyotaka wao!
 
Uzuri US huwa hachezewi hovyo na hawa viongozi uchwara wa Afrika akiamua hujengi na unatakiwa ufuate maana mnajua kabisa Jiwe atakuwa mstaafu muda si mrefu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la umeme namuunga mkono jpm!
Hawa Watu nao tukiwaendekeza sana hatutafanya chochote!
Kama wanapinga basi walete njia mbadala wajenge mradi utakao kuwa mbadala
Naungana na wewe,maana inasemekana
hata reli ya TAZARA walikuwa wanapinga
ikabidi kukimbilia kwa wachina
sasa angalia jinsi reli hii ilivyomuhimu
kwa usafirishaji wa abilia na mizigo.
 
Soma link utafakari. kuna sense kwa wanachokisema. Nani hapendi umeme?
Sikia kaka hata ukisoma hiyo link haina maana,binadamu kama hakitaki kitu anatafuta formular ili kionekane kibaya tu hiyo ni human nature lakini mbona wao wanarusha rocket kila siku makobora mazito kila siku pia nyuklia wanayo na wanatumia uliwasikia tumekaa tukasema waache wanaharibu mazingira lakini umeme wetu wanapiga kelele " wanataka tuwategee kila siku ndio maana wanapinga na idea zao za ajabu ajabu it doesn't make sense" hata Leo tukisema tujinge kinu cha kurutubisha nyuklia watapinga tu huko kwao vipo lakini kwetu hawataki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili la umeme namuunga mkono jpm!
Hawa Watu nao tukiwaendekeza sana hatutafanya chochote!
Kama wanapinga basi walete njia mbadala wajenge mradi utakao kuwa mbadala
Umeelewa alichokisema huyo jamaa hapo?
Shida sio kuzalisha umeme Bali matatizo yatakayotokea baadaye ni makubwa mno kuliko faida ya huo umeme unataka kuzalishwa hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom