Kutoka ute mzito mweupe (usaha) kwenye uume

R

Ruth

Member
Joined
Jul 27, 2009
Messages
27
Points
0
R

Ruth

Member
Joined Jul 27, 2009
27 0
JF Dr. Naomba mnisaidie hili,
Mume wangu alianza kusikia maumivu kwenye kichwa cha uume anapokojoa baada ya siku kama nne maumivu yaliendelea kupanda juu, baada ya siku kama tatu maumivu yalikoma ukaanza kutoka ute mzito mweupe kama usaha wakati mwingine mpaka chupi aliyoivaa inachafuka, alipoenda hosipitali akarudi akaniambia wamemwambia ana UTI, akapewa antibiotics akaniambia amepona, tumekaa kama wiki, leo asubuhi nimeamka nikamwangalia yeye akiwa bado amelala nikaona ule ute mweupe umetoka tena, sasa nina wasiwasi kwamba anaweza kuwa na tatizo zaidi ya UTI aliyoniambia, Kuanzia alipoanza kusikia maumivu hatujafanya tendo la ndoa mpaka leo kwa sababu ya mimi kuwa na wasi wasi, sasa tatizo linaweza kuwa nini?
 
P

Paul S.S

Verified Member
Joined
Aug 27, 2009
Messages
6,029
Points
1,500
P

Paul S.S

Verified Member
Joined Aug 27, 2009
6,029 1,500
Subiri wataalamu watakusaidia zaidi
lakini kwa utaalamu wangu mdogo hilo linawezekana likawa gonjwa la zinaa linaitwa gonorea
Tabia ya gono linapo muingia mtu hasa wa kiume ni maumivu wakati wa kukojoa na kisha baada ya muda huanza kutokwa na maji maji meupe kama usaha fulani ambao hupelekea chupi kuwa na vidoa doa vya ute unaotoka kwenye uume.
ushauri:i usishiriki naye kabisa tendo la ndoa hadi ahakikishe amepona kabisa kwa kwenda hospitali na kupata tiba sahihi
 
W

WILSON MWIJAGE

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2011
Messages
276
Points
0
W

WILSON MWIJAGE

JF-Expert Member
Joined May 30, 2011
276 0
Ndugu,

Dada Ruth, mimi ningependa kununua ushauri nzuri wa Paulss kwamba "usishiriki naye kabisa tendo la ndoa hadi ahakikishe amepona kabisa kwa kwenda hospitali na kupata tiba sahihi" Tafadhali jizuie hata kama ni mwaka mmoja
 
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Messages
40,173
Points
2,000
MziziMkavu

MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined Feb 3, 2009
40,173 2,000
Kisonono

Kisonono ni maradhi ya zinaa ambayo husababishwa na bakteria zinazofahamika kisayansi kama Neisseria gonorrhoeae. Bakteria hizo hushambulia utandotelezi unaozunguka sehemu za siri.

Ingawa kwa makisio maambukizi 360,000 ya kisonono huripotiwa kila mwaka nchini Marekani, wataalamu wamekisia kuwa watu karibia 650,000 huambukizwa kwa mwaka.

Kama ilivyo klamidia, kisonono nayo huwa haionyeshi dalili. Kisonono ikiwepo huwa na dalili kama zile za klamidia ambazo huhusisha mauvimu wakati wa kukojoa na kutokwa kwa majiyanayonuka au usaha katika uke au uume.

Kisonono huonekana kwa urahisi kwa wanaume ambao hutoa usaha kutoka katika mfereji wa mkojo (urethra). Huanza kidogo, lakini huongezeka na huwa mwingi na kusababisha kusikia haja ya kukojoa mara kwa mara huku kukiwa na maumivu.

Kisonono ikisambaa na kufikia prostate, mfereji wa mkojo huziba kwa kiasi fulani. Kwa wanawake maambuki hutokea katika urethra, uke au mlango wa uzazi (cervix). Ingawa mwasho unaotokana na majimaji katika uke unaweza kuwa mkubwa, mara nyingi dalili hizi huwa ni chache au hamna kabisa katika hatua za awali.

Kisonono isiyotibiwa inaweza kusababisha PID kwa wanawake. Watoto wanaozaliwa na mama wenye kisonono huwa na hatari ya kuambukizwa wakati wa kuzaliwa; maambukizo haya yanaweza kusababisha magonjwa ya meno kwa wachanga.

Uchunguzi wa ugonjwa hufanywa kwa kuchungunza usaha kutoka katika uke au uume au mkojo kwa uwepo wa Neisseria gonorrhoeae.

Kisonono iliongezeka kwa kiasi kikubwa Marekani mnamo miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980, hadi kukaribia kufikia kiwango cha magonjwa ya mlipuko (epidemic proportions) kwa vijana wanaobalehe na watu wa umri wa kati.

Kisonono hutibiwa kwa antibaotiki kadhaa, ingawa maambukizi yamekuwa na ukinzani juu ya tiba ya baadhi ya madawa katika

miongo ya nyuma. Moja kati ya mambo magumu katika kupambana na kisonono ni kutafuta mahusiano yote ya kimapenzi ya nyuma ya aliyeambukizwa ili kuweza kuzuia usambaaji zaidi wa ugonjwa.

H

Hatipunguzo

Member
Joined
Dec 4, 2011
Messages
10
Points
20
H

Hatipunguzo

Member
Joined Dec 4, 2011
10 20
Kuna uwezekano mkubwa sana ikawa ni UTI,lakini pia inaweza ikawa ni gonorhea.haujatoa viashiria vya kutosha.
 
doctorz

doctorz

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2010
Messages
907
Points
195
doctorz

doctorz

JF-Expert Member
Joined Aug 10, 2010
907 195
Wote mnahitaji tiba ya haraka. Kama anapata tiba pekee basi kila akikuingilia utamambukiza tena.

Kwa mwanamke dalili zake huchelewa kuonekana. Labda baada ya cycles mbili au 3 na kama hujapata tiba waweza ukapata salpingitis which may lead to ectopic pregnancy. Vigorous treatment regime kwa wote ndiyo usalama wenu.

Siku hizi tiba ni rahisi. Nenda INFECTIOUS DESEASE CLINIC kwa ushauri na tiba.
 
M

mchajikobe

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Messages
2,530
Points
2,000
M

mchajikobe

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2009
2,530 2,000
JF Dr. Naomba mnisaidie hili,
Mume wangu alianza kusikia maumivu kwenye kichwa cha uume anapokojoa baada ya siku kama nne maumivu yaliendelea kupanda juu, baada ya siku kama tatu maumivu yalikoma ukaanza kutoka ute mzito mweupe kama usaha wakati mwingine mpaka chupi aliyoivaa inachafuka, alipoenda hosipitali akarudi akaniambia wamemwambia ana UTI, akapewa antibiotics akaniambia amepona, tumekaa kama wiki, leo asubuhi nimeamka nikamwangalia yeye akiwa bado amelala nikaona ule ute mweupe umetoka tena, sasa nina wasiwasi kwamba anaweza kuwa na tatizo zaidi ya UTI aliyoniambia, Kuanzia alipoanza kusikia maumivu hatujafanya tendo la ndoa mpaka leo kwa sababu ya mimi kuwa na wasi wasi, sasa tatizo linaweza kuwa nini?
Embu mkanunue dawa inaitwa ciprofloxacin alafu muangalie maendeleo yake!!!
 
King'asti

King'asti

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2009
Messages
27,689
Points
2,000
King'asti

King'asti

JF-Expert Member
Joined Nov 26, 2009
27,689 2,000
Cipro ni strong antibiotic na haitakiwi kutumia bila kuandikiwa na dr.
Bibie, nenda kwanza hosp wewe ukapimwe. Muambie dr bila chenga kuhusu mumeo, fanyiwa vipimo na upate matibabu. Rudi home muambie mumeo mficha maradhi kilio humuumbua. Aache ujanja wa porini, muende hosp na kupata tiba sahihi manake utapata ugumba kama sio kuzaa mtoto kipofu. Mkishapona mtamalizana huo mwanya ama ufa ulioleta ugonjwa. Na umuambie aache ushamba, ngono nzembe ni uzembe haswaa!
Embu mkanunue dawa inaitwa ciprofloxacin alafu muangalie maendeleo yake!!!
 
DASA

DASA

JF-Expert Member
Joined
Jan 6, 2011
Messages
1,031
Points
1,195
DASA

DASA

JF-Expert Member
Joined Jan 6, 2011
1,031 1,195
Dah! pole sana dadangu, lakini hapo lazima kuna mmoja wenu alitoka nje ya ndoa, inaweza ikawa ni wewe vile vile kwasababu kwa wanawake dalili huwa zinachelewa sana. kwahiyo na wewe wahi ukapime. Shaurina vizuri na mumeo, samehaneni, mtibiwe mpone kabisa, kabla madhara makubwa zaidi hayajawakuta.
 
K-killer

K-killer

Senior Member
Joined
Nov 14, 2011
Messages
143
Points
0
K-killer

K-killer

Senior Member
Joined Nov 14, 2011
143 0
Anakubaliana na DASA,huu ugwonja umempata mmoja wenu bada ya kutoka nnje ya ndoA na kufaanya ngono zembe,kama ni bwana wako basi atakua alitoka nnje ya ndoa tena baada ya kutumia dawa,akapona lakini kama alikutana tena na huyo mtu atakua aliambukizwa tenA..Kwa upande wa Pili inawezekana wewe dada yetu ndo ulitoka nnje ya ndoa nakufanya ngono zembe ivo kuambukizwa gonorhea,kwa wanawake huwa inajificha sana hivo ngumu kuonekama,kwaiyo kAma ulifanya na mume wako tendo la ndoa bada ya yeye kutumia dawa na kupona basi umemuambukiza tena..Ni vema wote mkapima alafu mwenye ugonjwa Atumie dawa mpaka apone,La mwisho kuweni wAminifu kwenye ndoa yenu,leo gono kesho itakua ngoma mamaaaa!
 
kibaa

kibaa

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2011
Messages
718
Points
225
kibaa

kibaa

JF-Expert Member
Joined Aug 29, 2011
718 225
hilo ni GONO aka KISONONO miaka ya 80 mpaka 90 mwishoni lilikuwa maarufu nenda hosp ww na mumeo mkapate matibabu
 
Butho Mtenzi

Butho Mtenzi

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2011
Messages
331
Points
195
Butho Mtenzi

Butho Mtenzi

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2011
331 195
Kapimen jaman itawasaidia saaana watu wangu ila ilo inshort ni Gono
 
chenngula

chenngula

Member
Joined
Apr 30, 2019
Messages
5
Points
20
chenngula

chenngula

Member
Joined Apr 30, 2019
5 20
Pole sana ila hilo ni gono ambalo jina lake limejumuishwa na magonjwa mengne yazinaa na kuitwa mkojo machafu UTI.mmoja kati yenu aliupata nje kisha akauleta ndani. hvyo yawezekana kuwa wewe pia unao ndo maana mumeo baada ya kutibiwa aliugua tena. Maana magonjwa meng ya zinaa yanachelewa kuonesha dalili kwa wanawake. Dalili kwa mwanaume huonekana ndani ya wiki moja wakati huo kwa mwanamke ni mpaka miez mitatu.
 
M

Mwasapi justin

New Member
Joined
Jul 3, 2019
Messages
1
Points
20
M

Mwasapi justin

New Member
Joined Jul 3, 2019
1 20
Kisonono

Kisonono ni maradhi ya zinaa ambayo husababishwa na bakteria zinazofahamika kisayansi kama Neisseria gonorrhoeae. Bakteria hizo hushambulia utandotelezi unaozunguka sehemu za siri.

Ingawa kwa makisio maambukizi 360,000 ya kisonono huripotiwa kila mwaka nchini Marekani, wataalamu wamekisia kuwa watu karibia 650,000 huambukizwa kwa mwaka.

Kama ilivyo klamidia, kisonono nayo huwa haionyeshi dalili. Kisonono ikiwepo huwa na dalili kama zile za klamidia ambazo huhusisha mauvimu wakati wa kukojoa na kutokwa kwa majiyanayonuka au usaha katika uke au uume.

Kisonono huonekana kwa urahisi kwa wanaume ambao hutoa usaha kutoka katika mfereji wa mkojo (urethra). Huanza kidogo, lakini huongezeka na huwa mwingi na kusababisha kusikia haja ya kukojoa mara kwa mara huku kukiwa na maumivu.

Kisonono ikisambaa na kufikia prostate, mfereji wa mkojo huziba kwa kiasi fulani. Kwa wanawake maambuki hutokea katika urethra, uke au mlango wa uzazi (cervix). Ingawa mwasho unaotokana na majimaji katika uke unaweza kuwa mkubwa, mara nyingi dalili hizi huwa ni chache au hamna kabisa katika hatua za awali.

Kisonono isiyotibiwa inaweza kusababisha PID kwa wanawake. Watoto wanaozaliwa na mama wenye kisonono huwa na hatari ya kuambukizwa wakati wa kuzaliwa; maambukizo haya yanaweza kusababisha magonjwa ya meno kwa wachanga.

Uchunguzi wa ugonjwa hufanywa kwa kuchungunza usaha kutoka katika uke au uume au mkojo kwa uwepo wa Neisseria gonorrhoeae.

Kisonono iliongezeka kwa kiasi kikubwa Marekani mnamo miaka ya 1970 na mwanzoni mwa miaka ya 1980, hadi kukaribia kufikia kiwango cha magonjwa ya mlipuko (epidemic proportions) kwa vijana wanaobalehe na watu wa umri wa kati.

Kisonono hutibiwa kwa antibaotiki kadhaa, ingawa maambukizi yamekuwa na ukinzani juu ya tiba ya baadhi ya madawa katika

miongo ya nyuma. Moja kati ya mambo magumu katika kupambana na kisonono ni kutafuta mahusiano yote ya kimapenzi ya nyuma ya aliyeambukizwa ili kuweza kuzuia usambaaji zaidi wa ugonjwa.
Mi nikajua unataka dawa
 
Forum statistics

Threads 1,315,265
Members 505,171
Posts 31,851,862
Top