Kutoka NEC ya CCM: Mrithi wa Kinana ni Dr. Bashiru Ally. Apitishwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM

Chama cha mapinduzi kimempitisha De Bashiru Ally kuwa katibu mkuu kumrithi mwanasiasa machachari ndugu Abdurahman kinana.. Dr Bashiru si mtu mashuhuri (popular) kwani alikuja kujulikana zaidi baada ya kuteuliwa na Rais Magufuli kama mwenyekiti wa kamati ya kuchunguza mali za chama lakini zaidi ya hapo hana umaarufu wowote wala influence inayofahamika.
Chadema nao walimchagua Dr Mashinji katika mazingira ya aina hii. Tangu kuteuliwa kwa mashinji nafasi ya katibu mkuu IMEPWAYA.
Je wanaCCM wategemee kupwaya na mashinji mwingine huko CCM?
Nimchambuzi wa masuala ya kisiasa hasa kwa ngazi za kimataifa..

nimeanza kumsikia kitambo kidogo kwenye vyombo vya habar vya Magharibi hususa ni DW (Doch vere Ujeruman) na BBC..

ni muhadhiri wa kitengo cha elimu ya sayansi ya siasa chuo kikuu cha dsm
 
Miongoni mwa wachambuzi WA mambo ya siasa ni ndugu yetu Dr. Bashilu ambapo mwanzo alijinadi kuwa ni mtu huru, ghafla leo amekasimishwa madaraka makuu ya kiutendaji ndani ya chama ambacho alishawahi kusema hakitendi kwa haki.

Tumeona kwa kina PolePole na hata Professor Kabudi,je Dr Bashiru atanyamaza saa ya kula ama atadhuhutu kusema waombe kwanza kabla ya kuendelea kula?!!
mmmmmhhhhhhhh . . . . . .mi napita tu
 
Halafu jamaa alishakana kuwa mwanachama wa CCM mara mbili ila leo mle mle

Hahahaaaaaa . . . . .chezea appointment wewe . . . .
 
Kitwanga,Muhongo na wengine.
Kitwaga alitumbuliwa kwa ufisadi? Siyo alifukuzwa kwa ulevi? Muhongo alifanya ufisadi gani ambao naibu wake Kalemani akapona? Wengine kina nani?

Na lini yeye mwenyewe atajitumbua kwa ufisadi wa Dar Ferry?
 
Mtumishi wa umma anapotolewa kwenye utumishi wa umma kwenda kutumikia chama anastaafu utumishi wake wa umma au anaacha kazi kwa "Resignation"?

CCM hamuitendee Tanzania haki mnapowatotoa watu kwenye utumishi wa umma na kuwaingiza kwenye shughuli za siasa ambazo hawakuwahi kuzitaka

Hapo pana utata!
 
Back
Top Bottom