Kutoka NEC ya CCM: Mrithi wa Kinana ni Dr. Bashiru Ally. Apitishwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,395
Tukiwa tunaendelea na kikao, tayari jina la Dr. Bashiru Ally limepitishwa na kuwa mrithi wa Kinana kuanzia leo.

Dr. Bashiru ni Mwalimu Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia ndiyo alikuwa Mwenyekiti wa Tume maalum ya kuchunguza mali za CCM iliyoundwa na Rais Magufuli.

Dkt. Bashiru kama wengi tunavyomfahamu ni Mzalendo, Mjamaa na Mnyerere.

D0A8E741-FD4B-4F7F-B816-0E000E92A9E6.jpeg
Mwenyekiti wa Tume ya kuchunguza mali za CCM Dkt Bashiru Ally akipongezwa baada ya kuteuliwa kwa kauli moja na NEC kuwa Katibu Mkuu mpya wa Chama hicho ukumbi wa Kikwete jijini Dar leo
=====

1.jpg

2.jpg

3.jpg
 
Tukiwa tunaendelea na kikao, tayari jina la Dr. Bashiru Ally limepitishwa na kuwa mrithi wa Kinana kuanzia leo. Dr. Bashiru ni Mwalimu Mwandamizi kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, pia ndiyo alikuwa Mwenyekiti wa Tume maalum ya kuchunguza mali za CCM iliyoundwa na Rais Magufuli.

Dkt. Bashiru kama wengi tunavyomfahamu ni Mzalendo, Mjamaa na Mnyerere.
Mtumishi wa umma anapotolewa kwenye utumishi wa umma kwenda kutumikia chama anastaafu utumishi wake wa umma au anaacha kazi kwa "Resignation"?

CCM hamuitendee Tanzania haki mnapowatotoa watu kwenye utumishi wa umma na kuwaingiza kwenye shughuli za siasa ambazo hawakuwahi kuzitaka
 
Back
Top Bottom