Kutoka mke mtarajiwa hadi mchepuko

Kutoka mke mtarajiwa hadi mchepuko

Wana MMU, Umuofia kwenu.

Kuna kisa kimenikuta nimeona sehemu pekee ya kupata ushauri na mawazo mapana ni kwenu.

Nilikuwa na mchumba ambaye tulikuwa tunapendana sana na muda si muda tungefunga pingu za maisha. Ghafla mwenzangu alipata safari ya kwenda Marekani na kuniomba tuahirishe zoezi mpaka atakaporudi kwani asingechukua muda mrefu.

Nikamkubalia; akakwea zake pipa na alipokuwa huko mawasiliano kwa njia za mtandao yaliendelea. Siku moja akaniambia hawezi tena kuolewa na mimi kwa kuwa alikuwa anataka kufunga ndoa na mtu mwingine. Nilisononeka sana kwa namna nilivyompenda, lakini nikawa sina namna zaidi ya kumtakia kila la heri katika mahusiano yake hayo mapya. Baada ya kuuguza maumivu, nikapata" material wife" na tukafunga pingu za maisha. Sasa nina miaka kadhaa kwenye ndoa.

Hivi karibuni aliyekuwa mchumba wangu karejea kutoka America na akanitafuta kwa udi na uvumba na akafanikiwa kunipata. Ananiambia bado ananipenda na yuko tayari kutoa gharama yeyote ili nimwache mke wangu.

Kaweka "one billion" nikamtolea nje! Nikamweleza namna ambavyo tunaishi na mke wangu na watoto kwa amani na kwamba nampenda mke wangu na watoto sana. Hivyo pendo langu kwake limeshapata replacement.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu mrefu akarealize kwamba hawezi kunishawishi kwa namna yeyote kumwacha my beloved wife, akaingiza hoja nyingine ya kuwa second wife kwani hawezi kuishi bila mimi.

Na kwamba kama nikimkatalia na hilo basi hana haja ya kuendelea kuishi. Anasema kama pesa anazo lakini kakosa mwanamme aliyemwonyesha mapenzi ya kweli na aliyemfikisha kileleni kama mimi. Hilo ndo linanitisha nikaona niliweke kwenu wadau.

Karibuni kwa ushauri.

Hadithi njoo uwongo njoo utamu kolea.. Hii hadithi inatufundisha kwamba... Wewe ni mtaalamu wa kufikisha mwanamke kileleni so kama kuna mademu humu JF wakutafute. Pia una hela sana hadi ukakataa kuhongwa TSh. Bilioni moja. Hahahahahahahaaaaaaa
 
1bn ni wanaume wachache wanaweza kuchomoa. Nafikiri hapa kuna chai labda kama ana nia ya kukutoa roho
 
Naamini hii ni hadithi kama nyingine haina uhalisia hata chembe. Ndani ya muda mchache amemake Billions? ??????
 
Hizi dharau nyingine hizi!hivi kwa nini umeamua kutudanganya?hiyo 1b ya zimdollar au ?aaah huyu jamaa hafai kabisa.
 
Billion moja ndio thamani halisi ya amani na uaminifu katika familia.yako?kama ndivyo vuruga familia uje kulia hapa kama wenzio
 
ukitaka uvunje ndoa yako ruhusu huyo shetani
 
You can not be serious mkuu, bilion moja mtu akupe tu kisa unamfikisha sijui nin nin!?, sio kweli, vinginevyo kuna jambo zaidi ya unayoelezea kama sio kamba lkn.
 
kapatwa na nini huko marikani yake? si alikukatia mawasiliano nakukwambia kwamba hawezi tena olewa na mtu kama wewe leo anakuja na figisufigisu yako hiyo ya nini tena achana nae ni muuaji huyo hafai anataka akununue afu akufanye kuwa mtumwa wake wa ngono hafai
 
One billion kama unatumia kila siku lak 1 inaisha baada miaka 26. nahis itakua lak 1 ya Uganda au Zimbabwe! naanzaje kuacha?
 
1billion? huyo atakuwa anacheza picha za matusi America. ..how can she offer u one billion?
 
jiulize:;
1. kwanini alithubutu kukuacha?
2. je, kama angepata anayemfikisha na kumjali wewe thamani yako ingekuwepo?
huyo dada ni hatari kuliko Ebola.
 
Wana MMU, Umuofia kwenu.

Kuna kisa kimenikuta nimeona sehemu pekee ya kupata ushauri na mawazo mapana ni kwenu.

Nilikuwa na mchumba ambaye tulikuwa tunapendana sana na muda si muda tungefunga pingu za maisha. Ghafla mwenzangu alipata safari ya kwenda Marekani na kuniomba tuahirishe zoezi mpaka atakaporudi kwani asingechukua muda mrefu.

Nikamkubalia; akakwea zake pipa na alipokuwa huko mawasiliano kwa njia za mtandao yaliendelea. Siku moja akaniambia hawezi tena kuolewa na mimi kwa kuwa alikuwa anataka kufunga ndoa na mtu mwingine. Nilisononeka sana kwa namna nilivyompenda, lakini nikawa sina namna zaidi ya kumtakia kila la heri katika mahusiano yake hayo mapya. Baada ya kuuguza maumivu, nikapata" material wife" na tukafunga pingu za maisha. Sasa nina miaka kadhaa kwenye ndoa.

Hivi karibuni aliyekuwa mchumba wangu karejea kutoka America na akanitafuta kwa udi na uvumba na akafanikiwa kunipata. Ananiambia bado ananipenda na yuko tayari kutoa gharama yeyote ili nimwache mke wangu.

Kaweka "one billion" nikamtolea nje! Nikamweleza namna ambavyo tunaishi na mke wangu na watoto kwa amani na kwamba nampenda mke wangu na watoto sana. Hivyo pendo langu kwake limeshapata replacement.

Baada ya majadiliano ya muda mrefu mrefu akarealize kwamba hawezi kunishawishi kwa namna yeyote kumwacha my beloved wife, akaingiza hoja nyingine ya kuwa second wife kwani hawezi kuishi bila mimi.

Na kwamba kama nikimkatalia na hilo basi hana haja ya kuendelea kuishi. Anasema kama pesa anazo lakini kakosa mwanamme aliyemwonyesha mapenzi ya kweli na aliyemfikisha kileleni kama mimi. Hilo ndo linanitisha nikaona niliweke kwenu wadau.

Karibuni kwa ushauri.
basi hana haja ya kuendelea kuishi --hivi ni vitisho vya wanawake indirect.

hawezi tena kuolewa na mimi kwa kuwa alikuwa anataka kufunga ndoa na mtu mwingine
Ananiambia bado ananipenda na yuko tayari kutoa gharama yeyote ili nimwache mke wangu. - huu ni upuuzi

second wife kwani hawezi kuishi bila mimi. -- labda kama dini yako ya ruhusu.....

Muda wake ushapita alichezea bahati huyo asubiri wengine we una familia tayari...pesa hainunu upendo au mapenzi ya mume na mke na watoto
 
Uko sawa mkuu, baadhi ya wanawake wanafanya maisha kwa trial and error!
 
One billion🙄🙄 anataka kukununua!?? Hizo pesa kapata wapi😕😕 au typing ERROR!??😀😀
 
Back
Top Bottom