Camilo Cienfuegos
JF-Expert Member
- Apr 23, 2015
- 18,849
- 67,285
Hivi Mugabe na Joshua Nkomo walikosana nini?, nawakumbuka Askofu Muzorewa na Sithole pia.namuona kulia joshua nkomo, nadhani ni hayati sasa hivi
he is so old, he can't recall ever being young.That is not me. I have always been old." - Robert Mugabe
Joshua Nkomo huyoHuyo mwingine eti nimemfananisha na Kenneth Kaunda!
Hivi Mugabe na Joshua Nkomo walikosana nini?, nawakumbuka Askofu Muzorewa na Sithole pia.
NKOMO alikuwa ZAPU na MUGABE ni ZANU-PF halafu NKOMO base yake ya kisiasa ilikuwa ni BULAWAYO kwa wa-NDEBELE wakati MUGABE ni m-SHONA . Upinzani mkubwa wa kisiasa kwa MUGABE uko BULAWAYO. Baada ya UHURU wa mwaka 1981 ZAPU chini ya NKOMO ilipambana vikali na jeshi la ZANU-PF chini ya MUGABE ambapo watu wengi walikufa na hasa wale wa ZAPU katika jimbo la Matabele yaani huko BULAWAYO na maeneo mengine. Hatimaye MUGABE alishinda lakini inasemekana watu kati ya 20,000 na 30,000 wengi wakiwa ni wanachama wa ZAPU walikufa katika vita hivi vya ndani baada tu ya uhuru....Miaka hiyo ya 80 nikiwa kijana mdogo nilikuwa naishi eneo moja jijini Dar es salaam na baadhi ya Wazimbabwe ambao walipokwenda kwao walikuwa viongozi wakubwa wa nchi, kwa hiyo nafahamu kidogo ugomvi kati ya Nkomo na Mugabe kupitia Wazimbabwe hao. Ugomvi wao nadhani ulikuwa katika misingi ya kikabila na tofauti za kiitikadi.
Mkuu Ahsante kwa historia nzuri sana, Je unaweza kujua MUGABE ALIKUWA NA CHEO GANI KIJESHI? Kwa kweli ukabila ni moja ya tatizo kubwa sana Afrika na limeuawatu wengi na kuzorotesha maendeleo yetu.
dah, natamani nikuone baba yangu unipe story nyingi zaidi ya hizi. nazipendaga sana.Mmmmmmmhhh, mimi sikuwahi kusikia kuwa MUGABE alikuwa na cheo cha kijeshi, nadhani alikuwa ni mwanasiasa zaidi kama alivyokuwa Edgar Tekere ambaye umaarufu wake wakati Fulani ulikuwa ni mkubwa kuliko MUGABE, na sina hakika huyo TEKERE yuko wapi sasa...ila katika majeshi ya wapigania uhuru wa Zimbabwe kulikuwa na jina moja maarufu la Jenerali Josiah Tongogara, ambaye alikuwa maarufu sana. nakumbuka huyu Tongogara alikufa katika kifo cha kutatanisha kwa ajali ya gari mwishoni mwa miaka ya 70 nadhani mwaka 1979 siku chache tu baada ya kushiriki mazungumzo ya suala la Zimbabwe huko London, Uingereza maarufu kama mazungumzo au makubaliano ya Lancaster...Nakumbuka rafiki yetu mmoja wakati wa ujana wetu alikuwa anajiita 'General Tongogara' yaani kifo kile kilimhuzunisha sana akawa anatoa machozi (Yalikuwa ni mambo ya utoto tu unajua miaka ile vijana tulikuwa tumepikwa sana kiitikadi na hasa za mapinduzi na vita, wengine walikuwa wanajiita Major castro; wengine sijui Montgomery; wengine sijui Field Marshal Rommel; General Paton, Zhukov wa vita vya pili vya dunia na kadhalika)
Lakini hili jambo sijui likoje, mbona Joshua Nkomo kama vile ndie alikuwa rais wa Zimbabwe kabla ya Mugabe!!NKOMO alikuwa ZAPU na MUGABE ni ZANU-PF halafu NKOMO base yake ya kisiasa ilikuwa ni BULAWAYO kwa wa-NDEBELE wakati MUGABE ni m-SHONA wa HARARE na maeneo mengine. Upinzani mkubwa wa kisiasa kwa MUGABE uko BULAWAYO. Baada ya UHURU wa mwaka 1981 ZAPU chini ya NKOMO ilipambana vikali na jeshi la ZANU-PF chini ya MUGABE ambapo watu wengi walikufa na hasa wale wa ZAPU katika jimbo la Matabele yaani huko BULAWAYO na maeneo mengine. Hatimaye MUGABE alishinda lakini inasemekana watu kati ya 20,000 na 30,000 wengi wakiwa ni wanachama wa ZAPU walikufa katika vita hivi vya ndani baada tu ya uhuru....Miaka hiyo ya 80 nikiwa kijana mdogo nilikuwa naishi eneo moja jijini Dar es salaam na baadhi ya Wazimbabwe ambao walipokwenda kwao walikuwa viongozi wakubwa wa nchi, kwa hiyo nafahamu kidogo ugomvi kati ya Nkomo na Mugabe kupitia Wazimbabwe hao. Ugomvi wao nadhani ulikuwa katika misingi ya kikabila na tofauti za kiitikadi.
Lakini hili jambo sijui likoje, mbona Joshua Nkomo kama vile ndie alikuwa rais wa Zimbabwe kabla ya Mugabe!!
Unaweza kuwa sahihi kuhusu uswaiba wa mwl.Nyerere na Joshua Nkomo vs Robert Mugabe, maana nakumbuka kwenye kitabu cha Historia darasa la 5, Joshua Nkomo alikuwa na coverage kubwa sana kuliko Robert Mugabe.Mmmmmmmmmmmmmmhhhhhhh kwa NKOMO kuwa Rais, hapana.... ingawa ni wazi kabla ya Mugabe Rais wa Zimbabwe alikuwa ni Canaan Banana, kwa mujibu wa katiba iliyokubaliwa baada ya uhuru na wakati huo Mugabe akiwa ni Waziri Mkuu.. Urais wa Banana ulikuwa hauna nguvu sana kwani nafasi ya Waziri Mkuu ilikuwa na nguvu kubwa. Baadaye nadhani katikati ya miaka ya 80 Mugabe akawa Rais (nadhani mwka 1987 kama sijakosea) yaani akawa Rais mwenye madaraka kamili kwa kiingereza EXECUTIVE PRESIDENT. Hii ilikuwa ni baada ya katiba kubadilishwa. Joshua Nkomo hajawahi kuwa Rais....Baada ya uhuru wa Zimbabwe Nkomo alipewa nafasi ya uwaziri katika serikali ya Mugabe kwa muda mfupi ingawa baadaye aliondolewa/au kukimbia kutokana na tofauti kati yake na Mugabe..Ikumbukwe kuwa kuna majina mengine yalikuwa maarufu huko Zimbabwe wakati wa mapambano ya uhuru haya ni Askofu Abel Muzorerwa na Padri Ndabaningi Sithole, lakini nadhani hawa wamepotea kwa umaarufu kwa kuwa hawakuwa 'wakali' sana kwa utawala wa wazungu wa Ian Smith...Kwa kumbukumbu zangu nadhani (sina hakika) Mwalimu Nyerere alikuwa karibu zaidi na Joshua Nkomo kuliko MUGABE wakati wa mapambano ya silaha dhidi ya wazungu. lakini baada ya NKOMO kukimbizwa na MUGABE nadhani MUGABE ndipo akapata 'ujiko' wa kukubalika na Tanzania...Nasema hivi kwa kuwa wakati wetu wa udogo jina la Joshua Nkomo hapa Tanzania lilikuwa linavuma kuliko la Robert Mugabe...lakini hii ya mwisho katika andiko langu sina hakika sana.
Old is gold maaaaannn
Duh! Jongwe sijui kama halitachinjwa this time naona wajeda wamekaza buti kwelikweli
Hakuna marefu yasiyo na ncha!Duh! Jongwe sijui kama halitachinjwa this time naona wajeda wamekaza buti kwelikweli
Kawapindua pindua sana naona kama nyakati zimeisha wadiaHakuna marefu yasiyo na ncha!