Kutoka kwangu niwaonavyo watanzania. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka kwangu niwaonavyo watanzania.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by The Native Son, Jul 23, 2009.

 1. The Native Son

  The Native Son Member

  #1
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ndugu zangu,
  Hii ni jinsi nionavyo mimi kuhusu watanzania na maisha yao ya kila siku. Nimewatazama watanzania wenzangu kama watu wanaoishi kwa matukio yaani leo wamesikia hili kabla hawajalikamilisha kesho wamesikia lingine wakalikimbilia nalo halijaisha kesho kutwa lingine wanalirukia ili mradi matumizi ya hewa ya oksijeni na uchafu unaoandamananayo vinatumika na siku na maisha duni na ya shida yanakwenda.

  Tafakari:
  1. Je ni kweli ni jinsi tulivyo?
  2. Au tunamalengo mengi yasiyotekelezeka?
   
 2. E

  Evy Member

  #2
  Jul 23, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  i have to admit i dont know what are trying to say.
   
 3. The Native Son

  The Native Son Member

  #3
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Mfano siku fulani mtanzania aliletewa hoja ya ufisadi kuhusu manunuzi ya rada na ndege vyote vya serikali, sina shaka mimi, wewe na watanzania wengi hatujui hili limekwishaje, ikafika siku tukaletewa hoja ya mikataba mibovu ya migodi mfano ule wa Buzwagi, tukaiacha ile ya ndege na rada tukakimbilia uko hilo nalo hatujui limeishia wapi, likaja tukio la Richmond na Dowans, pia si shaka linakwendaje na limeishia wapi wengi wetu hatujui. Nimetaja machache ila kuna matukio mengi na kwa sasa watanzania wengi tuko kwenye tukio la Bungeni na mambo ya bajeti.
   
  Last edited: Jul 23, 2009
 4. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sielewi maana ya hiyo sentensi nyekundu. Hata hivyo tabia uliyoieleza naamini ni hulka ya binadamu, na sio kwamba ni tabia ya watu fulani, au wa eneo fulani.
   
 5. The Native Son

  The Native Son Member

  #5
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Naukubali mtazamo wako, ila tukumbuke ulimwengu huu una watu wengi wakiwepo wanaosababisha matukio kutokea na wale wanaoishi kwa matukio yaliyosababishwa na wengine. Sasa je sisi tuko wapi kama kishi kwa matukio ndio hulka ya kila mwanadamu?
   
 6. Timor

  Timor Member

  #6
  Jul 23, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 49
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 15
  Kamwe hatupo hivyo nadhani ndivyo unavyojifikiria ulivyo!!!
   
 7. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Sisi?
  Umewahi kusikia kuhusu 80/20 rule? (Tizama Pareto principle )
  Wewe ambaye jambo hili linakuumiza kichwa, nikupe hongera, maana pengine umo kwenye kundi la hao 20.
   
 8. The Native Son

  The Native Son Member

  #8
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Kwa hiyo tuseme nini, tuna malengo mengi tu kwa wakati mmoja na tena yasiyotekelezeka?
   
 9. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  The Native Son,
  Mwandishi mmoja aliandika kitabu akasema 80% of work-done kazini kwenu inafanywa na 20% ya employees. I would advice you to pay more attention to the 20% and not 80% ya watanzania; fanya kinyume chake pale tu unapokwenda kuwaomba watanzania wakupigie kura.
   
 10. The Native Son

  The Native Son Member

  #10
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Uko sawa katika nukuu, ila nadhani sisi ni kwa maana nikiwa kati ya watanzania. Nadhani tungelitazama na hili katika mapana kidogo wala lisilete mitazamo ya kihisia tu, wengine husema kuwa "emotional". Maana utawaona watanzania, mara mikataba mibovu kabla hatma haijajulikana linaanza la EPA wanasahau mikataba wanarukia hili nalo haliishi inaanza hoja nyingine mwisho wa yoye hakuna kinachotatuliwa. Hii iko hivyo hata kwenye kupanga mambo mengine ya nchi ya kimaendeleo
   
 11. The Native Son

  The Native Son Member

  #11
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Uko sawa ndugu, sasa naona hilo tatizo lipo ila ni matokeo ya namna siasa na wanasiasa wafanyavyo kazi. Ila usipotazama wengi ni sahihi? Japo nakumbuka bwana Plato yule mwanafunzi wa Socrates, anayesadikika kuwa mwanafilosofia nguli aliyewahi kuwepo uko ugiriki, aliasema, ashakum si matusi nanukuu, "The Majority Is always Stupid". Huo ni mtazamo wake na mazingira yake. Hawa watanzania wengi wanasaidiwaje?
   
 12. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #12
  Jul 23, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Taasisi zisizo za kiserikali zinaweza kusaidia. Ndiyo maana hata taasisi za kidini imebidi kutoa msimamo majuzi.
  Hizi taasisi ni sehemu ya 20% (japo not all of them). He-he-he-heh! :)


  Kwa hiyo no more "sisi" bwana - kumaanisha "watanzania" (in another words 100%)! Maana there will always be 80% and another group will be 20%.
   
  Last edited: Jul 23, 2009
 13. The Native Son

  The Native Son Member

  #13
  Jul 23, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ila tukumbuke "80-20 rule" ile ya Bwana Vilfredo Pareto wa Italia iliyokubaliwa vema na Bwana Joseph M. Juran, hawa jamaa ni wachumi na wachambuzi wa mambo y a biashara, naamini kuwa wote hatuwezi kufanya biashara moja lazima wengine wawe wanunuzi ndio maana waaiita "the law of the vital few". Sasa tukija kwenye maslahi ya kijamii unadhani si ni ubinafsi tu unaowafanya watanzania siku zote kukumbwa na kufuata upepo wa kimatukio bila kushika lolote? Kama ni hivyo tuhalalishe UBINAFSI?
   
 14. m

  mgiriki Member

  #14
  Jul 23, 2009
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Unaju sisihapa tunaweza tukaliendekeza ila haisadii pasipo wabunge wetu kulizungumzia huko vikaoni
   
 15. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #15
  Jul 23, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Watanzania hawa ni wepi? Wale wa Tumbatu au Tandahimba? Au kutoka Tumbatu mpaka Tandahimba? Mafia mpaka Mpanda?

  Kama ni wote ulitumia research method gani? Ulikaa nao muda gani? Uliona nini kilichokushawishi kufikia hitimisho lako? Ulifanya peer review au ndiyo unaibia hapa? Ulikuwa na control gani?

  Ulihusisha wa nje au wa ndani tu? Unaweza kutoa anecdote gani? Umepata muongozo wa publication gani?

  Una hakika gani kwamba hizi tabia ni za Watanzania tu na wala si za watu wa Afrika Mashariki, au Waafrika kwa ujumla, au watu wote? au hata viumbe wote? Unaweza kutoa ushahidi wowote unaoonyesha kwamba haya mambo ni hususan kwa watanzania? Na kama si hususan kwa nini uyaseme kama ya watanzania?

  Una hakika gani kwamba Watanzania wanasikia unayofikiri wanasikia? Au ni wewe na wachache mnaosikia na kuwapa mzigo "Watanzania" kwamba wanasikia? Ikiwa unakusudia habari unajua idadi ya Watanzania wanaosoma magazeti kila siiku ni ngapi? redio?

  Vipi ikiwa katika Watanzania kuna wasio na hizi sifa, bado utaweza kusema kwamba watanzania wana hizi sifa? Kama ndiyo utachora wapi mstari wa kutenganisha baina ya Watanzania kuwa na hizi sifa na kutokuwa nazo
   
 16. The Native Son

  The Native Son Member

  #16
  Jul 24, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 87
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Ngugu Bluray kwanza nianze kwa kukikubali vema kipande cha hoja yako nilicho "bold, italicise and colour it maloon". Tukumbuke wao waliwahi kusema, "practice makes more perfect", na kwa kuwa kwa siku nilizo bahatika kuishi nimeona na nimewazungumzia watanzania wenzangu ambao mambo haya yamekuwa yakitokea utaona wanashabikia kabla halijaisha hilo linatokea jingine wanaanza ushabiki kwenye hili, na hili wamelifanyia mazoezi kwa kulirudia kila mara matukio yatokeapo hapo nikajijengea uwezo kuwa hawa watakua wameshakomaa katika kuishi kwa matukio. Nimewazungumzia watanazia wandani ambao ndio ninao kila siku walio wengi na wenye nguvu ya kufanya mabadiliko kwani walio mbali ni sawa na fimbo ya mbali isiyouwa nyoka.
  Labda hoja iwe, Je Watanzania wanayafikiri ninayoyafikiri, na je wanayasikia ninayoyasema au yanayosemwa?
  Kutoka kwangu sina shaka na kusikia kwao japo si kwa kiwango kikubwa, ila labda tujiulize, Je wanakielewa wanachokisikia? Hii itawawezesha wajenge fikra sahihi na maamuzi sahihi. Ni hayo kwa sasa.
   
 17. F

  Froida JF-Expert Member

  #17
  Jul 24, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ukisema Watanzania wanaishi kwa matukio una maana gani
  Mimi nadhani tatizo hapa nikuridhika au kukata tamaa kufuatilia maovu yanayoibuliwa likitolewa jibu hata kama haliridhishi basi uandishi wa utafiti uankuwa haufanyiki,wananchi wenyewe kulivalia bango jambo hilo inakuwa shida na hata vyombo vya usimamizi wanatumia janja nyingi kufunika jambo hilo bado tunasafari ndefu kuweza kuyapembua haya
   
Loading...