Nakumbuka mwaka 1997 kule Iringa kuna demu nilimtongoza akakubali, tukakubaliana kesho tukutane kwa mgegedo, ilipofika kesho akaniambia hawara yake wa zamani waliepotezana nae kaja, atakuwepo kwa siku tatu hivyo akaniomba amuhudumie huyo hawara kwa siku hizo halafu akiondoka ndio tuendelee na mipango yetu. Nilimjibu sawa ila sikumtaka tena. Baada ya siku tano hivi akaanza kunitafuta na kusema nahisi nimekukosea nisamehe. Kwa kifupi sikumhitaji tena. Kilikuwa kisa cha ajabu na vurugu nyingi zilifuata kwani kila alipoona nina demu mwingine hata kwa salamu tu ilikuwa ugomvi. Ilikuwa kituko. Nakumbuka!