G COY naikumbuka, wao walipigwa bogi Chita, hata mm ilikuwa nipigwe bogi hilo nikajongo. Nasikia Chita MP ni simba na chui ni kweli au vipi? Medard namkumbuka sana alitupokea F COY ikiwa combania ya mapokezi 30/6/89, alitupiga cadebra hadi saa 5 usiku ndio akatupatia chakula yaani ugali wa mchana na maharage meupe kumbuka ndio tumetoka nyumbani siku ya kwanza hatuna mess tin wala chochote na baada ya hapo akatulaza ktk vitanga bila magodoro. Hakika kuna mengi ya kusimulia kuhusu msjeshi.
Mkuu COPPER,Malela anaendelea kutafutwa kila depo Tz nzima.
Umenifurahisha sana!Bwana wee mimi nilikuwa D COY hapo ruvu jkt op programe ya chama kweli enzi zile lilikuwa jeshi kweli sio hili la wabunge nakumbuka hemedi msangi na makele waliingia mitini wakatimkia ccp polisi moshi bila taarifa hasa makele tulimtafuta vibwende mpaka tukazani ameliwa na simba na walitoka kwenye order mara nyingi ,kwakweli makele tulijua ameliwa na simba kama malela it's true story kwa watu wa ruvu najua mtakumbuka .
Je hawa Wabunge watashiriki mkutano wa Bunge la bajeti? Kama sivyo, itakuwa ni hujuma ili kupitisha uozo kiurahisi. Pia, Wapiga kura tutakuwa tumekosa haki ya kuwakilishwa.Hii ya JKT kuna agenda imejificha,
tusubiri lipo litakalodhihirika bayana!
Hawa ni wazee unadhani wataweza kula chakula
halafu wakimbie. Kichurachira,kukroo nani ataweza.
Hizo pit short&T shirt watavaa ama Kombati moja kwa moja. Watapigwa Nuwa kweli.
Miili yao imekomaa pia wiki 3 kwa Kuruta anatakiwa kukimbia smart area zote maana kijeshi wanasema hajui kutembea.
Naona kama kwa kuwa wanakwenda kama Waheshimiwa lazima Maafande watawanyenyekea.
Huyu Faustine ndiye yule aliyekuwa kipa wa timu? Nakumbuka jina la kwanza, mara ya mwisho nilimuona Muhimbili akisomea medicine. Dr Omar alifarika.