Kutoka jangwani jmosi, wananchi waporwa ardhi kinondoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kutoka jangwani jmosi, wananchi waporwa ardhi kinondoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WATANABE, Jun 14, 2012.

 1. W

  WATANABE JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 1,091
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 135
  Wananchi wengi wao wakiwa wazee na akina mama ambao walihudhuria mkutano wa CCM pale Jangwani Jumamosi ya tar 09 Juni 2012 kutoka Kata ya Kwembe, na kuhakikishiwa na Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Mhe Anne Tibaijuka kuwa hakuna mkazi yeyote wa Jiji la DSM atakayeporwa ardhi yake pasipo taratibu za kisheria kuzingatiwa na kulipwa fidia stahiki leo hii Alhamisi tar 14 Juni 2012 walipigwa na bubuwazi pale Mkuu wa Mkoa wa DSM Ndg Mecky Sadiky alipozuru eneo la Mtaa wa Kwembe na kuwataka zaidi ya wakazi 3000 wanaoishi na katika maeneo ya Kisopwa, King'azi n.k linalotarajiwa kujengwa Chuo kishiriki cha Muhimbili kubomoa nyumba zao na kuhama pasipo kulipwa fidia ya ardhi; eti kwa kisingizuio kuwa walivamia ardhi ya Serikali iliyokuwa ikimilikiwa na Kampuni ya Mifugo iliyokuwa ikiitwa Kampuni ya Biashara ya Mifugo Tanzania (KABIMITA) moja ya mashirika ya umma yalioanzishwa na enzi za Mwalimu Nyerere.

  Wazee na Wananchi waliotakiwa kubomoa nyumba zao leo hii na Mkuu wa Mkoa wa DSM chini ya Serikali ya CCM Ndg Mecky Sadick wengi wao walihamishiwa katika maeneo haya yaliyokuwa sehemu ya
  Kijiji cha Kwembe mwaka 1979 na Serikali ya awamu ya kwanza ya Mwalimu Nyerere, enzi hizo chama tawala kilikuwa ni "TANU" katika Operesheni iliyojulikana kama "Gezaulole" wakati huo Mkuu wa Mkoa akiwa Ndg Rwegasira.

  Wengi wao walikamatwa kutoka mitaa mbali mbali ya Jiji kwa tuhuma za uzururaji na kukosa ajira na Serikali kuwahamishia katika Vijiji mbali mbali vilivyolizunguka Jiji la DSM ikiwemo Kijijii cha Kwembe kilichokuwa na hati ya usajili na kuandikishwa kama Kijiji cha Ujamaa. Kijiji cha Kwembe kilikabidhiwa hati ya usajili na aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais Hayati Rashidi Mfaume Kawawa.

  Hivyo walipofikishwa kijijini Kwembe na malori ya Serikali walipokelewa na kugawiwa ardhi kihalali na hivyo kuanza maisha mapya na uongozi halali wa Kijiji kilichokuwa na hati kamili ya usajili na kuandikishwa kama Kijiji cha ujamaa
  kwa lengo kuanza maisha ya kushiriki ajira ya kilimio chini ya kampeni ya "Kilimo ni Uti wa Mgongo" ambayo ilikuwa na hadhi sawa na Kilimo Kwanza ya CCM ya sasa.

  Vijiji vya ujamaa katika Jiji la DSM vilifutwa mwaka 2003, lakini haki za wananchi waliokuwa wakiishi katika vijiji hivyo zinalindwa na sheria
  Sheria mpya za Ardhi namba 4 na 5 mwaka 1999, Kifungu cha 15 cha Sheria ya Ardhi ya Vijiji namba 5 ya 1999 kinatamka kuwa “Ugawaji wa ardhi uliofanywa kwa mtu au kundi la watu waishio au waliotakiwa kuhamia na kuishi katika kijiji wakati wowote kati ya 01 Jan 1970 hadi 31 Des 1977 , kama ugawaji huo ulifanywa kwa mujibu wa sheria au kinyume cha sheria au bila kuzingatia sheria yoyote, sasa inathibitishwa kuwa ugawaji huo ni halali na kwamba daima ni wenye nguvu ya kutoa haki na wajibu wa kisheria kwa kundi la watu waliogawiwa ardhi hiyo....." Aidh kifungu cha 16 kinatamka .......... masharti ya kifungu 15 yatatumika kila mara ugawaji wa ardhi ya kijiji ulipofanywa na halmashauri ya kijiji au mamlaka nyingine yoyote mnamo na baada ya 01 jan 1978 hadi tarehe ya kuanza kutumika kwa sheria hii.

  Utaratibu wa kuwapora wananchi waliokuwa wakiishi katika vilivyokuwa vijiji vinavyolizunguka Jiji la DSM uliasisiwa na FISADU MKUU WA ARDHI aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Ndg Salome Sijaona, ambaye sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Japan, nafasi aliyopatiwa baada ya kutimiza umri wa kustaafu utumishi wa umma ilihali nchi hii ikitengeneza mamilioni ya vijana wenye elimu ya juu kushika nyadhifa mbali mbali lakini wasio na ajira.

  Sasa wananchi hawa wamekosea wapi katika kuendeleza makazi na kilimo katika ardhi waliyogawiwa kihalali zaidi ya miaka 30 iliyopita tena kwa kuhamishiwa katika ardhi hiyo kwa mabavu na Serikali ya awamu ya kwanza?

  Tunaomba viongozi wa CCM, chama kinachojidai kurithi mazuri ya TANU waliopo katika jamvi la JF hususan Nape Nnauye wajitokeze kujibu tuhuma hizi za ubabaishaji na kuwadharau wazee waasisi wa taifa hili waliopasisi mfumo wa watanzania kuishi katika vijiji vya ujamaa na kuiruhusu Serikali ya CCM chama kilichozaliwa na TANU kuwapora wananchi ardhi yao kwa kukiuka Sheria na haki za binadamu kiasi hiki.

  Kwani kuna ulazima gani chuo cha Muhimbili kuwapora wananchi ardhi yao takribani hekta 3000 ilihali Kilomita 9 tu kutoka eneo la Kwembe Mloganzila ipo ardhi ya Serikali yenye ukubwa huo huo wa hekta 3000 inayomilikiwa na Serikali chini ya liitwalo Shirika la Elimu Kibaha lenye miundo mbinu yote inayohitajika kwa chuo kama cha utabibu ikiwemo Hospitali ya hadhi ya Mkoa Tumbi kwa ajii ya wananfuzi kufanya mazoezi, Chuo cha uuguzi, barabara za lami, miundo mbinu ya maji na umeme, Shule za Msingi na Sekondari, Kituo cha Polisi, Maktaba, Viwanja vya Michezo mbali mbali na nyongeza mashamba ya mifugo kwa ajili ya kuwapatia wanachuo maziwa na mayai na mboga mboga.

  Ni dhahiri kuwa Serikali ya CCM ilikosa umakini katika kutafuta eneo la kujenga chuo hiki na watendaji wa Serikali ya CCM waliokosa usimamizi makini wenye kuwatetea wanyonge walizingatia ufisadi watakaoufanya kupitia zoezi ya ulipwaji wa fidia tu ndio maana ya kuiacha ardhi ya Serikali yenye miundo mbinu lukuki kwa chuo hiki. Ni dhahiri kuwa miundo mbinu hii iliyotekelezwa huko Kibaha itaendelea kuoza na watanzania tutalazmika kulipa mkopo wa kujenga miunombinu mipya katika eneo la Mloganzila kwa mkopo ambao watanzania tutalazimika kuulipa kwa riba kubwa.
   
 2. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,728
  Likes Received: 12,797
  Trophy Points: 280
  Tisheti na khanga ,wali maharage vime waponza.
   
 3. n

  nyabhera JF-Expert Member

  #3
  Jun 12, 2014
  Joined: Nov 25, 2011
  Messages: 425
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 60
  Soma kisa hiki cha mlinganyo wa Bunda na Dar es Salamu.

  Zamani miaka ya sabini. Shirika la Tanganyika Packers lilimiliki maeneo ya kupumuzishia wanyama maeneo haya yalijulikana kwa Jina la eneo la Kabimita. Hapa Bunda Tanganyika Packers walikua na eneo katika kijiji cha Mekomalilo. Huko Dar es Salamu Tanganyika Packers walikua na eneo kijiji cha iloganzala.

  Maeneo yote haya yalihamiwa na wanavijiji baada ya Shirika kufilisika Mwaka 1978.

  Hivyo wananchi wamekalia na kuendeleza maeneo haya kwa miaka 36.

  Ufisadi umetokea bunda ambapo halmashauri kwa maslahi yao wachache imeagiza wanavijiji waliokaa maeneo haya wahame. Wakati kwa Sasa maeneo hayo ni vitongoji viwili ktk kijiji cha Mekomalilo.

  Wakati wanakiji hawa wakitakiwa kupisha maeneo haya. Wenzao walioishi katika eneo kama hili huko Dar es Salam wamepimiwa rejea gazeti la Nipashe.
  Mwaka 2013 August 17.

  Hii ndo tofauti ya kujua haki na kutojua haki.
   
Loading...