Kutoka James Ngugi Hadi Ngugi Wa Thiong'o

Kutoka James Ngugi Hadi Ngugi Wa Thiong'o

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
22,454
Reaction score
32,980
KUTOKA JAMES NGUGI HADI NGUGI WA THIONG’O
TOFAUTI YA ‘’JAMES’’ NA ‘’THIONG’O’’


1748666536956.png

Wengi wa kizazi kile ambacho Ngugi alianza kuandika tulimfahamu kwa jina la James Ngugi. Inawezekana sana wengi kati yetu kila wakisikia jina hili Ngugi linawakumbusha siku zao miaka mingi iliyopita walipokuwa shule na pengine hata chuo kikuu. Wengi tulisoma kitabu chake cha kwanza, ‘’Weep Not Child,’’ alichoandika akiwa James Ngugi kisha tukasoma ‘’A Grain of Wheat,’’ alichoandika sasa akiwa Ngugi wa Thiong’o. Vitabu vyote hivi Ngugi aliandika akiwa na kusudio maalum. Jina la kitabu hiki, ‘’A Grain of Wheat,’’ ni nukuu kutoka Biblia (John: 12:24). Ngugi amekipa jina kitabu chake kutoka mfano wa punje ya ngano ambayo kama haijapandwa ardhini haitaweza kuzaa punje nyingine nyingi na si moja. Ikipandwa punje hii moja inazaa mashuke. Huu ni muujiza wa Mungu. Kwa jina la kitabu na nukuu hiyo ni wazi kuwa Ngugi ni mwandishi aliyekuwa anaijua vyema Biblia, kuipenda na kuiamini.

Haya ni matokeo ya mafaniko ya Wamishionari walioingia Afrika na kujipa jukumu la kuwaelimisha Waafrika kupitia shule zao maarufu zikijulikana kama shule za Misheni. Hizi ndizo shule zilizojenga Ukristo Afrika ya Mashariki. Ngugi alinufaika na elimu hii ambayo ilijiakisi katika maisha yake ya udogoni na katika jina lake la ‘’Jmaes,’’ hadi pale alipolibadili na kuwa Ngugi wa Thiong’o. Kwa nini Ngugi alilikana jina lale la ubatizo? James ni jina maarufu katika majina ya Kiingereza. Majina haya mawili ‘’Ngugi Wa Thiong’o,’’ haya ni majina ya Kikikuyu. William Shakespeare ameuliza katika mchezo wake maarufu ‘’Romeo and Juliet,’’ kauliza, ‘’What’s in a name…’’ yaani kuna nini katika jina? Kisha akatoa jibu na kusema kuwa waridi katika jina lolote utakaloliita harufu yake itakuwa ni ile ile haitabadilika. Si kama Ngugi bingwa wa fasihi hakulijua hili. Alilijua fika lakini kuna kitu alikuwa anataka kukionyesha. Ngugi alikuwa anaiarifu jamii yake na wale waliokuwa wamemzunguka kuwa yeye anahama nyumba na akataka ijulikane kuwa kahama nyumba ile.

Ngugi kuanzia hapa akiwa na jina jipya akaanza kuandika kwa Kikikuyu, lugha ya mama yake akitumia jina lake jipya la ‘’Ngugi wa Thiong’o.’’ Hakuna mwandishi aliyepata kufanya kitu kama hiki Afrika kabla yake wala hajatokea mwingine kuiga mfano wake. Kuanzia hapa kalamu ya Ngugi wa Thiong’o ikawa si tu inaandika bali pia inasema maneno. Kalamu yake Ngugi wa Thiong’o ikazidi ukali ikawa sasa inakata na kujeruhi. Ngugi wa Thiong’o akawa mwandishi ambae kalamu yake inasomwa na kusikilizwa – kalamu inayokamata macho na masikio. Vitu viwili muhimu kupita kiasi katika hisia ya binadamu. Kalamu ya James Ngugi ikawa inakujulisha huyu aliyeishika ni nani na nini kinamchochea kuisukuma kalamu hii kiasi inamwaga wino wake kama damu ilivyomwagika katika watu kabila lake la Wakikuyu walipokuwa wakipambana na Waingereza kwa silaha kudai ardhi yao iliyoporwa. Si wengi wanajua kuwa kaka zake wawili Ngugi walikuwa wakati wa Mau Mau na mama yake alipata alipata kuteswa.

Hebu tusimame kidogo hapa tuvute pumzi.

‘’Mwanangu Mwanasiti, kijino kama chikikichi alitokea chanjagaa akajenga nyuma akakaa, vya kujengea vikuta na vilango vya kupita.’’

Maneno haya yalikuwa yanasemwa na mpiga hadithi na akimaliza kuyatamka maneno haya ndipo anapoanza hadithi yake kwa kusema: ‘’Hapo zamani za kale…’’

Huu ndiyo ulikuwa utangulizi bibi zetu walipokuwa wanatupigia hadithi. Hapa pazia linakuwa limefunguliwa hadithi inaanza.

Ngugi wa Thiong’o alianza historia yake ya uandishi kwa kurejea nyuma katika zama za kale. Kalamu ya Ngugi ikawaleta Mau Mau mbele ya ulimwengu wafahamike kama wanavyostahili kufahamika kwani waliowaandika waliwaandika sivyo wakawapa jina silo, wakawaita magaidi wauaji. Hakika Ngugi aliandika riwaya lakini vitabu vyake si riwaya kama riwaya zilivyozoeleka. Ngugi aliandika riwaya riwaya zilizokuwa na ukweli ndani yake. Ngugi anaeleza historia ya uhuru wa Kenya na wale waliojitolea kuupigania uhuru huo. Majina yote msomaji atakayokutananayo ni majina ya Wakikuyu, viongozi wa harakati hawa utawasoma wakiwa katika mapambano ya silaha na utawasoma mashujaa hawa wakining’inia katika vitanzi wakinyongwa na Waingereza kwa kosa la kunyanyua silaha dhidi ya majeshi Malkia kuidai ardhi yao.

Vitabu hivyo viwili nilivyovitaja hapo juu, ‘’Weep Not Child,’’ na ‘’ A Grain of Wheat,’’ ndiyo vilikuwa ‘’Mwanangu Mwanasiti’’ ya Ngugi, yaani utangulizi wake kwa hayo atakayokuja kuandika baadae. Mabadiliko ya jina lake na kuandika kwa Kikikuyu ilikuwa kuitaka dunia imfahamu yeye ni muandishi na mtu wa aina gani. Vitabu vyote vya Ngugi vilikuwa vitabu vyenye kuhangaisha na kufikirisha. Mpiga hadithi yeyote hakosi wasikilizaji. Kila atakapoonekana yupo mahali wasikilizaji watamzunguka kumsikiliza. Serikali ya Kenya ikawa sasa inakaa na yeye kwa tahadhari kubwa. Haukupita muda baada ya ‘’Grain of Wheat,’’ Ngugi wa Thiong’o akaja na kitabu kingine – ‘’Petals of Blood.’’ Katika kitabu hiki Ngugi anaeleza kwa staili yake ile ile ya mpiga hadithi, dhuluma na ubadhirifu nchini kwake baada ya uhuru kupatikana. Mengi aliyoeleza ndani ya kitabu hiki kama ilivyokuwa katika vitabu vyake vingine, yalikuwa mambo yaliyopo ndani ya jamii ya Kenya.

Lakini kulikuwa na kitu hakijaonekana katika vitabu vyake hadi pale alipofika katikati ya miaka ya 1970. Miaka hii Kenya ilikuwa katika siasa za kutisha kwa viongozi kuuliwa na ikiaminika na serikali yenyewe. Mauji ya Tom Mboya, Gama Pinto, Ronald Ngala na Josiah Mwangi Kariuki yalitingisha nchi. Mauaji ya viongozi wa wananchi likageuka kuwa jambo la kawaida. Ndani ya Chuo Kikuu cha Nairobi kulikuwa na mjadala wa kisomo nini kisomeshwe chuoni hapo kitakachokuwa na manufaa kwa wahitimu wa chuo hicho. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam tayari kilishakuwa kinajulikana kama ‘’Marxist School.’’Huu ulikuwa wakati wa waandishi mfano wa Walter Rodney, Franz Fanon, Samir Amir kwa kuwataja wachache, waandishi hawa waliokuwa wanataka kuleta mabadiliko Afrika. Uhuru ulikuja na fikra mpya na fikra hizi mpya zilikinzana na fikra zilizokuwapo na kurithiwa kutoka kwa wakoloni. Siasa za Mashariki zilikuwa zimeshapiga hodi Kenya toka enzi za kupigania uhuru. Watawala wa Kenya wakawa wanaiogopa historia yao wenyewe ya kupigania uhuru wao. Ukiiogopa historia hii ni wazi kuwa utaiogopa pia historia ya Dedan Kimathi na Mau Mau.

Ilkuwa msomaji hatoliona jina la Dedan Kimathi kwa maandishi ndani ya kitabu chochote cha Ngugi Wathiong’o lakini akiwa ni mtambuzi atawasoma na atawasikia Mau Mau; na atawasona na atawasikia wasaliti vilevile. Halikadhalika atasoma, atawasikia na kuwaona viongozi wa uhuru wa Kenya pamoja na ‘’Home Guards’’ jeshi la Waafrika wasaliti lilioundwa kulinda maslahi ya Waingereza ndani ya Kenya wakipokea uhuru. Lakini juu ya Ngugi kueleza haya yote Ngugi alikuwa na donge limemkwama rohoni, halishuki halitoki nje. Ngugi akihangaishwa ndani ya moyo wake kwa yeye kutotoka ndani ya shimo alilojichimbia mwenyewe kwa mikono yake kwa kuwa kimya bila kumtaja shujaa katika mashujaa wa uhuru wa Kenya, kiongozi wa Mau Mau, Dedan Kimathi katika kitabu chake chochote alichopata kuandika. Ndani ya Kenya muongo mmoja baada ya uhuru akiangalia kila upande uhuru haukuwa umeleta mabadiliko ya maana kwa wananchi. Ardhi iliyochukua roho nyingi za Mau Mau kutaka kuikomboa zilikuwa badi iko mikononi kwa Wazungu. Inawezekana sana kuwa hali hii ndiyo iliyomfanya Ngugi kusimami kumuadhimisha Dedan Kimathi katika kitabu alichoandika akishirikiana na Mithere Githae Mugo, ‘’The Trial of Dedan Kimathi.’’ Ndani ya kitabu hiki Ngugi anamtambulisha Dedan Kimathi dunia imafahamu na halikadhalika dunia iwafahamu pia Waingereza.

Kipindi hiki ni muhimu kwa Ngugi kwani ni kipindi cha kuchimbua makaburi ya mashujaa. Wakati huu Ngugi aliingia katika sanaa ya maigizo. Maonyesho haya hayakuwa katika majukwaa ndani ya kumbi za mijini bali katika majukwaa yaliyojengwa kwa miti maeneo ya wazi vijijini watazamaji wakikaa chini ya vivuli vya miti na kuangalia tamithlia ya mambo yanayowahusu wao katika maisha yao ya kila siku. Ngugi alikuwa kahama kutoka vyumba vya kuhadhiri (Lecture Theatre) ndani ya Chuo Kikuu Cha Nairobi amehamia vijijini kusomesha wananchi, wengi wao wajukuu na watoto wa Mau Mau na wapigania uhuru wa Kenya na yeye akiwa mmoja wao. Kitabu kwa asili yake kina kizingiti kinachomzuia mwananchi wa kawaida kukisoma na kujifunza kile kilichokuwa ndani yake. Kitabu kinahitaji kujua kusoma na fedha za kukinunua. Tatizo hili halikuwapo katika tamithlia hii ya kijijini iliyomfuata mwanakijiji, mkulima masikini kijijini alipo tena ikija kwa njia ya burudani ya bure isiyo na gharama yoyote kwake. Hii ilikuwa fursa ya kipekee sana kwa Ngugi na wale aliokuwanao katika mradi huu mpya wa kusomesha kupitia jukwaa la maonyesho. Uovu wa watawala sasa ukawa unawekwa wazi hadharani vijijini kwa kila jicho kuuona.

Katikia jukwaa hili wananchi wakawa wanaona mambo ambayo kama si kwa ubongo kujaliwa kuwa na uwezo wa utambuzi ingekuwa tabu kutambua ukatili na ufisadi huo unaoonyeshwa jukwaani ni wa wakoloni au wa serikali iliyochaguliwa kwa kura za wananchi? Jukwaa hili la kijijini likawa sasa linakumbusha historia ya Mau Mau na kile walichopigania kwa jasho na damu yao kukomboa nchi yao kutoka kwa wakoloni. Ngugi alikuwa anatonesha vidonda. Serikali ikaiona hatari hii na mara moja ikapiga marufuku jukwaa hili na Ngugi akakamatwa.

Kuanzia hapa Ngugi akawa adui mkubwa wa serikali ya Kenya hasa katika utawala wa Rais Moi. Kitu gani kilimsukuma Ngugi kunyanyua kalamu? Swali hili unaweza ukalipatia jibu kwa ukamilifu wake endapo utapitia maisha yake hatua kwa hatua toka akiwa mwanafunzi Makerere na ndipo alipoanza kuandika na kisha uangalie yote aliyopitia katika maisha yake akiwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu Nairobi, akiwa jela kama mfungwa wa siasa na mwishowe akiwa uhamishoni. Ni kitu gani kilimpambanua Ngugi Wathiong’o ukimweka jamvini pamoja na waandishi wengine si wa Kenya tu bali Afrika nzima?

Waandishi wanachongwa na jamii wanayoishi. Mlolongo wa vitabu alivyoandika Ngugi vitakuonyesha ile hali ya Kenya ya baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1963. Hii ni Kenya aliyoishi Ngugi Wa Thing’o. Kama vile Kenya inamuunga mkono Ngugi wa Thiong’o na yale aliyopigania na kuishi nayo umri wake wote wa kutafuta mabadiliko, yale aliyotuandikia Ngugi na kutueleza katika karatasi na katika jukwaa la wazi Kamiirithu zaidi ya nusu karne bado yanasikika, Tofauti ni kuwa wanayoyapigania yale aliyokuwa akipigania Ngugi ni hivi sasa katika karne ya 21 ni kizazi kingine. Mungu amemjaalia Ngugi wa Thiong’o kuyashuhudia hayo yote kwa macho yake.

Huyu ndiye Ngugi wa Thiong’o na hii ndiyo kalamu yake ilivyokuwa ikisomesha hadi umauti ulipomfika akiwa uhamishoni mbali na kwao.
 
Baada ya kuandika kitabu chake The petals of blood kilimletea shida mwaka 1977 akafungwa kwa mwaka mmoja.Mwaka 1982 akaamua kutoroka na kuishi ughaibuni.Hata hivyo miaka22 baadae alirudi Kenya baada ya wiki majambazi yakamvamia yakamjeruhi na kumbaka mkewe someni hukumu hapo chini.

Kenyan writer's assailants sentenced to death

A Kenyan court has sentenced three security guards to death for attacking and robbing renowned writer Ngugi wa Thiong'o and his wife.

During a homecoming after a 22-year self-imposed exile, Thiong'o was brutally beaten by four men in his apartment in Nairobi. His wife Njeeri was raped and burnt with cigarettes on the night of the attack in August 2004.

"The offence of robbery with violence is notorious in Nairobi and must be discouraged by imposing stiffer penalties," principal magistrate Julie Oseko said when passing sentence.

The three attackers - Richard Kayago Maeta, Elias Sikuku Wanjala and Peter Mulati Wafula - were convicted on Wednesday.

Wafula was additionally sentenced to 21 years in prison for rape. They said they would appeal.

The death sentence remains on Kenya's statutes, but has not been used since perpetrators of a 1980s coup attempt were hanged.

Four men attacked Thiong'o at the high-security apartment complex of a city-centre hotel. His nephew, John Kiragu Chege, was cleared of charges this week.

The magistrate said the 2004 attack was a normal case of robbery with violence, with no political overtones as Thiong'o had alleged. A laptop computer and jewellery were stolen.

Thiong'o said he did not agree with the death sentence but welcomed the convictions, although he took issue with the magistrate's statement that there were no other responsible parties at large.

"She (the magistrate) had no right to say that, she had no basis to say that. It is wrong," he told a news conference.

"The court's astonishing ruling and opinion may well have given, however unintentionally, comfort to those forces that had orchestrated the attack. It amounted to an unfounded exoneration of all forces connected with the attack."

Thiong'o, a professor of English and comparative literature at the University of California-Irvine, was jailed for a year without charge in 1977, then fled Kenya in 1982 after troops razed a theatre where one of his plays was being performed.

The novelist and playwright's works have been critical of British colonial rule and also, implicitly, of

Kenya's post-independence governments for corruption and exploitation of the poor.

His best works include Weep Not Child, A Grain Of Wheat, The trial of Dedan Kimath, Petals Of Blood,The river between and Devil On The Cross.
 
Shukrani sana mkuu kwa kutuletea hii historia hapa jukwaani...
 
Back
Top Bottom