Elections 2015 Kutoka Iringa: Kampeni CCM uwanja wa Samora

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
557
500
Habari wakuu,

Leo ni muendelezo wa kampeni, mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli leo yupo uwanja wa Samora mjini Iringa. Tuwe pamoja kujuzana yanayojiri kutoka Iringa.
======
Front Magu.jpg
Anaeongea kwa sasa ni aliyekuwa waziri wa ardhi, ndugu William Lukuvi na anampigia chapuo mgombea anaewania ubunge jimbo la Iringa mjini ndugu Mwakalebela, pia anampigia chapuo mgombea urais kupitia chama cha mapinduzi ndugu Magufuli.

Nape: Siku moja UKAWA walikuwa wanazindua mkutano wao Dar, nikiwa pale wakaanza kubishana Magufuli ametumia muda mrefu sana kuongea, nikawaambia mgombea wa UKAWA akifikisha dakika kumi na tano natoa milioni tano na nikazitanguliza, nikaulizwa ulijuaje, nikawaambia tatizo Lowassa anadhani Ikulu ni wodi ya wagonjwa.

Watanzania hatutaki Rais wa majaribio, ambae tukimwambia akakague majeshi yetu hawezi, tumchague tingatinga. Watanzania wameshaamua, hawawezi kupeleka fisadi Ikulu. Nakumbuka nilikuwa nahangaika na magamba, gamba namba moja Lowassa kashaondoka na chama kiko safi.

Kuna watu walikuwa wanakifanya chama chaka la kujifichia, wanaharibu katika serikali na kukimbilia katika chama wakiongozwa na Lowassa, tunaamini mabadiliko tunayoyataka ndani ya serikali na CCM tutayapata kwa ndugu Magufuli, katika orodha hakuna mtu alienistua kama Edward Lowassa. Nikasema na huyu fisadi anataka kwenda ikulu? Akasema hamuwezi kuzuia mafuriko, nikamwambia mafuriko yanazuiwa hata kwa kidole.

Mimi ni msemaji wa chama, kwanini hatukumpa nafasi mwizi? Hiyo habari ya ugonjwa anaijua yeye mwenyewe na tumuombee mungu tarehe 25 ashuhudie tunavyorudi Ikulu kwa kishindo!

Tunataka watuambie hata kazi moja tu ambayo Lowassa amefanya hakuiba, tulimpa uwaziri mkuu na miaka miwili tu Richmond, kazi gani ambayo tumempa Lowassa hakutumia madaraka yake vibaya na hakuiba? Mtu mwenye historia ya namna hii hatuwezi kumpeleka Ikulu, weka mbali na Ikulu.

Upande wa pili tunae Magufuli, nitajieni doa moja la Magufuli! Mbowe siku moja anasema vibaka wanachomwa moto, kibaka mkubwa Edward Lowassa yuko mtaani, leo amefika bei ya CHADEMA, wote kawatia mfukoni. Mzee Mtei kapigwa bilioni mbili, Mtei bilioni tatu na Msigwa ambae alisema atakaemuunga mkono Lowassa akapimwe akili. Sasa Msigwa tangulia mwenyewe ukapime akili yako mwenyewe.

Wakati wanajadili bei ya kuuzwa chama chao, Slaa alikuwemo ndani, nayajua mengi lakini leo nasema yanayomuhusu Msigwa, akaambie aende kufuta kauli akasema hawezi, akaambiwa basi nyamaza, akasema nipeni uji nishindwe kuinua mdopo, milioni 340 zikawekwa mezani ndio maana akipita anashindwa kumsema Lowassa na Magufuli, anabaki kusema nipeni kura. Uchungaji amesahau mtumishi huyu, tapeli mkubwa. Msigwa alisema watu wa Iringa msitumie bidhaa za ASAS, anaajiri vijana zaidi 400 Iringa na ndiye mlipa kodi mkubwa hapa Iringa. Anataka wale vijana 400 waje mtaani kuja kuwaandamanisha.

Tarehe 25 lazima tumwadhibu kwa kuhahakisha kura zote zinaenda kwa Mwakalebelela, wakati wa ujenzi wa barabara Iringa kwenda Dodoma, kambi ya Ujenzi ilitaka kuwekwa Iringa lakini ikabidi ikawekwe Dodoma akitaka eneo , kwanini! Msingwa. Sina mashaka Iringa tumemaliza, mwambieni pesa ziko wapi, pesa kidogo zilizobaki akale na mkewe, ya ubunge imeshaharibika.

Watanzania muombeeni mzee afya aone tunavyochukua nchi kwa kishindo, wanasema Nape alituambia bao la mkono, kelele watapiga sana lakini Ikulu inaenda kwa rangi za kijani, wenzetu wanahubiri mabadiliko, madadiliko ya kumuacha muadilifu tumpeleke mwizi, mabadiliko ya kumuacha mzima na kumpeleka marehemu. Kwa leo inatosha.

Magufuli
Anaeongea kwa sasa ni Magufuli na anawakosoa wale wanaosema serikali haijafanya kitu akiwemo mchungaji wa Iringa ambae aliamini anafata amri kumi. Anasema hata amani hamna chochote kilichofanyika! Anasema ni serikali hii hii ilileta vyama vingi 1992.

Sasa anaelezea kwanini ameomba urais ikiwemo kudumisha amani iliyopo na la pili ni kuafanya kazi na hatakuwa na blabla, analinganisha lami iliyoacha na mkoloni kwa miaka 76 na lami aliyojenga Kikwete kwa miaka 10. Pia anaelezea mipango yake ujenzi wa barabara njini Iringa ili magari makubwa yasikatishe Iringa mjini.

Anasema anafahamu hela ziko wapi na mapato hayo yatashuka chini kwa wananchi na anaeleza vipi atagharamia elimu bure mpaka kidato cha nne.


 
Last edited by a moderator:

Idimulwa

JF-Expert Member
May 27, 2011
4,104
2,000
Ndiyo Maana Watu Wachache Uwanjani,watu Wamechoshwa Na Blablaa Za Akina Nape
 

Muyobhyo

JF-Expert Member
Oct 9, 2014
8,161
2,000
wamshitaki na wamfunge ndio dawa, sasa kubwabwaja ni kujishushia hadhi yao, mshamkamata fungeni, mnaogopa nini
 

Bandundu

Senior Member
Sep 6, 2015
125
225
hawa jamaa wajinga sana.yaani kajikita kumponda tuu lowasa anafkiri atatubadilisha.tushachukua maamuzi tayari asubri kunyongwa tuu
 

Utotole

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
6,590
2,000
Anasema Lowassa ni Mwizi, kila kitengo alichopewa aliiba, kuanzia Kwenye chama, wizarani Hadi alipokuwa waziri mkuu Lowassa ni Mwizi asilia.
Na kwa jinsi CCM kilivyokuwa chama cha wapuuzi, mijizi na mafisadi (according to Kinana and Magufuli), kila akiiba sekta hii wanamhamishia sekta nyingine, na nyingine, na nyingine ili aendelee kuiba. Kwao CCM lengo kubwa ni kuhakikisha viongozi wameiba kila mahali. Otherwise, sioni sababu ya kuendelea kum-promote mwizi wakati kila anapowekwa anaiba.

Hata wakurugenzi ambao walitajwa kuhusika na wizi na ubadhirifu kufuatia ripoi za ukaguzi za CAG, mheshimiwa sana Rais amekuwa na kawaida ya kuwahamishia kwenye halmashauri na taasisi nyingine ili wakaibe huko pia kwa maendeleo ya chama chetu.

Ni kawaida sana kwa CCM.
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,779
2,000
hawa jamaa wajinga sana.yaani kajikita kumponda tuu lowasa anafkiri atatubadilisha.tushachukua maamuzi tayari asubri kunyongwa tuu
Nafikiri ndio kazi aliyopewa kwa leo kutoa kashifa tu.!
 

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
8,795
2,000
Hawa CCM kwa kweli sio wazima hata kidogo..yaani kuna jamaa kapanda jukwaani kwenye mkutano unaoendelea Iringa hakuna anachoongea tangu ameanza. Anasiliba upinzani tu na kutisha wananchi badala ya kunadi sera zao kwa wananchi. Ajabu ni wananchi wanaoshangilia ndio hawajielewi hata robo.... hakyanani hii nchi inawajinga wengi
 

Tyta

JF-Expert Member
May 21, 2011
12,799
2,000
Anasema Lowassa ni Mwizi, kila kitengo alichopewa aliiba, kuanzia Kwenye chama, wizarani Hadi alipokuwa waziri mkuu Lowassa ni Mwizi asilia.
kuna kitu kimoja unajitia upofu....Kwa nini hawakumwadhibu(kwa kumshitaki mahakamani)muda wote mpaka alipoamua kuondoka mwenyewe..........Wananchi wanamchagua Lowasa si kwa kuwa ni kiongozi bora,bali kuiamsha na kuiadhibu CCM kwa kuwa kichaka cha kulea maovu kwa miaka yote hii.Kaa ukitambua hakuna kashfa yoyote mtakayozua sasa ionekane ni ''shocker''........
 

Emma.

JF-Expert Member
Jun 25, 2012
19,911
2,000
Nape na ccm wameshanganyikiwa kama alikuwa mwinzi bado wakaendelea kumpa madarakani ?Lowasa ndo raisi wetu mtarajiwa
 

ebaeban

JF-Expert Member
Jan 15, 2012
2,032
2,000
Naweza kusema Kikwete ndio rais wa hovyo kabisa kumwacha huyu jamaa mpaka anamaliza ninashindwa kuamini
 

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
12,125
2,000
Thanks kwa updates

Baadhi ya picha za mkutano wa Magufuli katika uwanja Samora Iringa,
Magufuli akihutubia wana Iringa katika Uwanja wa Samora.

Nape akitoa maneno mawili matatu.


Baadhi ya wasanii wa vikundi mbali mbali wakiwa na Magufuli huku wengine wakiongozwa na Nape Nnauye wakipiga push-up katika mtindo wa #Magufulika
 

Tyta

JF-Expert Member
May 21, 2011
12,799
2,000
Na kwa jinsi CCM kilivyokuwa chama cha wapuuzi, mijizi na mafisadi (according to Kinana and Magufuli), kila akiiba sekta hii wanamhamishia sekta nyingine, na nyingine, na nyingine ili aendelee kuiba. Kwao CCM lengo kubwa ni kuhakikisha viongozi wameiba kila mahali. Otherwise, sioni sababu ya kuendelea kum-promote mwizi wakati kila anapowekwa anaiba.

Hata wakurugenzi ambao walitajwa kuhusika na wizi na ubadhirifu kufuatia ripoi za ukaguzi za CAG, mheshimiwa sana Rais amekuwa na kawaida ya kuwahamishia kwenye halmashauri na taasisi nyingine ili wakaibe huko pia kwa maendeleo ya chama chetu.

Ni kawaida sana kwa CCM.
kampeni hizi ndio zinazidi kuuchisha tabia mbaya walizonazo CCM,ukiiba hapa,unahamishwa sehemu nyingine.Ndio maana nchi hakuna sekta yoyote yenye unafuu,maana mijizi inahamishwa tu...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom