Kutoka Bungeni - Jumamosi 21, Aprili 2012 (Videos)

ameongea kwa utani tuu tusije tukalikuza kiivyo.

Wanataniana? Bungeni ambako Tanzania nzima tunaangalia, anamwita JAMBAZI?. Kuna kitu nyuma ya pazia.
Mama Makinda lazima aombe msamaha yeye mwenyewe aseme alikuwa anatania. JAMBAZI NI NENO BAYA SANA KAMA UNALIELLEWA
 
Ni lugha tu; ni kama kusema zitto kafanya matusi bungeni
Sio hawa hata ukiwaita mawaziri kwa majina yao wanakuja juu wanataka uwaite waheshiniwa... (basi kwa heshima si angesema muheshimiwa Jambazi...) au?

In short huyu mama kauli zake zinapelekea kufikiri mara mbili kama anawaza katika same wavelength na watu wenye busara.
 
Ulimi uliteleza alitaka kusema JEMBE LAKO. Nadhani jana usiku atakuwa alisikia wenzake wakisema yule Kijana ni Jembe la Chadema, kwa hiyo Madam Speaker na yeye asivyopenda kupitwa na wakati akafiriaaaa akaona hapo ndio mahala pa kuchomekea pia. Na yuko sahihi Mnyika ni Jembe.

Swali
Alimuokoaje Mbowe?
 
Yaani huyu Anna makinda anajisikia sana anamwita mbunge Jambazi. Anajua bunge linaangaliwa na wangapi analeta hisia zake.
 
Waziri Nundu anajaribu kuruka kesi ya Gati 13&14, anasema MoU wanazo nyingi tu. Ameruka tuhuma zote dhidi yake!

My Take: Utetezi wa Mh. Omar Rashid Nundu haumfanyi awe kiongozi mzuri vinginevyo haya yasingefika hapa. Hivi kwa nini hawataki kujiuzulu?
 
unaangalia na mazingira nanii acha kuwa kama sio muelewa.
Uelewa wangu ni kwamba huyu mama hafai kukalia hicho kiti.., chochote anachofanya naona kama anatuharibia Bunge (bora naibu wake).., huku kuteleza ulimi kumekuwa kunazidi...

Once is Coincidence.., Twice is a Trend... (huyu mama should go..)
 
sasa anaongea omary Nundu wa uchukuzi anakanusha tuhuma dhidi yake na kusema kuwa ni upotoshaji mkubwa

tuendelee kufuatilia na kujuzana.

my take.tumechoka ufisadi
 
Hata hivyo inabidi Spika atolee ufafanuzi wa lugha aliyotumia na kuomba radhi kama imemkwaza au kuwakwaza Wabunge wa CDM.
Hapana hapa Chadema wachume tu (waonyeshe ukubwa wa kisiasa na busara) ila siku wakikasirika na kumuita kibaraka au mwizi; warejee hii statement na kusema ni Utani tu, au kuteleza ulimi
 
Hakudhamiria tumsamehe tu bibi wa watu.


Simpendi Bi Kiroboto, lakini kwa hili naomba asamehewe, hakukusudia ulimi ulimteleza. Alitaka kusema "Jamaa yako" akajikuta anasema "Jambazi wako" ndio maana baada ya hapo alirekebisha kauli yake haraka sana ila hakuomba radhi! Kiungwana alitakiwa kuomba radhi kwa kukosea huko!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom