Kutoheshimu bendera ya Taifa inaposhushwa

Sigara Kali

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2017
Posts
3,708
Reaction score
8,749
Nakumbuka siku za nyuma mida ya SAA 12 jioni inaposhushwa Bendera ya Taifa watu tukisimama kwa adabu na ukakamavu hadi bendera inaposhushwa na kupiga filimbi kuruhusu watu kutembea

Ila siku za hivi karibuni nimegundua watanzania wengi hawana muda tena wa kuheshimu Bendera inaposhushwa

Mgambo anapiga filimbi kuashiria muda wa kushusha Bendera ya Taifa lakini watu hawana time wala mpango wowote wa kusimama ndo kwanza wanaendelea kuchapa lapa

Je hii ni kiashiria kwamba sasa watanzania wamechoka kuziheshimu alama za Taifa
Wapo busy na mambo yao hivyo kusimama dakika 2 kusubiri Bendera ishushwe ni kupoteza muda tu

Au watu hawana uzalendo na nchi yao?
Nawasilisha
 
Mkuu Uzalendo wa nchi hii hakuna kabisa, na umeuliwa na viongozi wetu baada ya utawala wa Kambarage
 
Nakumbuka siku za nyuma mida ya SAA 12 jioni inaposhushwa Bendera ya Taifa watu tukisimama kwa adabu na ukakamavu hadi bendera inaposhushwa na kupiga filimbi kuruhusu watu kutembea

Ila siku za hivi karibuni nimegundua watanzania wengi hawana muda tena wa kuheshimu Bendera inaposhushwa

Mgambo anapiga filimbi kuashiria muda wa kushusha Bendera ya Taifa lakini watu hawana time wala mpango wowote wa kusimama ndo kwanza wanaendelea kuchapa lapa

Je hii ni kiashiria kwamba sasa watanzania wamechoka kuziheshimu alama za Taifa
Wapo busy na mambo yao hivyo kusimama dakika 2 kusubiri Bendera ishushwe ni kupoteza muda tu

Au watu hawana uzalendo na nchi yao?
Nawasilisha

Muda wa kuabudu vitambaa umeshapita,kama tuliowapa madaraka hawaviheshimu viapo vyao na wanaivunja katiba hadharani kwa kisingizio cha kunyoosha nchi,nani atapoteza muda wake akisubiri kitambaa kishushwe mtini?
 
Nadhani kwa mtizamo wangu huu utaratibu upo sana nchi za kikomunisti
BTW mtoto anajifunza kutoka kwa wakubwa, walioko juu hawaoneshi uzalendo huo tutegemee kizazi kuendelea na kuendelea
 
Tusipangiane mi sijala unanisimamisha kisa unashusha bendera
 
Back
Top Bottom