Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 4,042
- 16,872
Habari za mchana.
Hii nimeitoa kwenye familia moja kanda ya ziwa.
Hivi ulishawahi kuona familia fulani ina watoto wengi lakini mmoja haolewi,au haoi na akioa anaacha ndoa haidumu.
Au kama ni mwanamke anaachika ili tu arudi Kwa wazazi?
Unakuta kijana anapambana lakini hatulii,anajikuta anaacha nyumba yake na kurudi Kwa wazazi?
Au binti anazalishwa mpaka watoto wanne na wanaume tofauti lakini ndoa zake zote hazidumu?
Hebu fuatilia kisa hiki cha mwanaume wa miaka 40,akinisimulia kisa chake baada ya kusoma mikasa yangu hapa Jamii forum.............
Naitwa Moses (siyo jina halisi) nimezaliwa moja ya mkoa maarufu kanda ya ziwa,nimezaliwa mwaka 1985 katika familia ya watoto wanane,watano wakiwa wa kiume na watatu ni wa kike. Huku Mimi nikiwa ni mtoto wa mwisho kuzaliwa.
Nilibahatika kumaliza shule ya msingi mwaka 2001 ,huku nikifaulu vizuri Sana kiasi cha wazazi wangu pamoja na Kaka na dada zangu kunisaidia ili niendelee na masomo ya pili ,nilisoma hadi kidato cha nne nikashindwa kufaulu vizuri kwenda advance hivyo nikarudi nyumbani nikajiunga na moja ya Kaka zangu kwenye biashara yake ya samaki.
Kifupi nimedumu kwenye biashara hiyo miaka mingi nikiwa na Mtaji wangu,hadi kufikia hatua ya kujenga kibanda changu (nyumba) hatua ambayo iliniweka kwenye mazingira mazuri kwani niliaminiwa,nilipendwa kijijini kwetu,lakini hata wanawake walinipenda nadhani ni kwasababu ya maendeleo niliyokuwa nayo.
Na ilipofika mwaka 2012 niliweza kutangaza ndoa na moja ya mchumba wangu wa muda mrefu Aitwaye zawadi, taratibu za kuoana zilifuata na ndoa ikapata baraka Kwa wazazi wote wanne.
Zawadi ni mwanamke ambaye tulipendana sana,Kwanza tulifanana vitu vingi ikiwemo wote kuwa ni malast born,hii ni moja cha pili familia Yao nao wapo wengi kama Sisi huku wao wakiwa tisa na mwanaume ni mmoja tu ya Yule first born ,waliofuata wote ni jinsia Ke.
Lingine ni heshima na maadili ya familia ile kuanzia dada zake namna wote walivyotulia kwenye ndoa zao lakini pia namna walivyo wazuri,zawadi ni moja ya wanawake weupe na Mimi mtu mweupe mrefu ulikuwa ni ugonjwa wangu kiukweli.
anasimulia Moses.
Mimi: siyo wewe tu Mimi mwenyewe Kwa mwanamke mweupe sipindui meza na nikiwekewa mtego ni rahisi kunasa (tunapeana tano na kucheka)
Moses:Ni kweli bro lakini sisi kabila letu tumezidi,yaani tangu zamani mwanamke mweupe alipewa thamani kubwa.(Huku akicheka zaidi)
Mimi:hebu nambie maisha yalikuwaje baada ya kuoana.
Anaendelea kusimulia..................
Bro we acha tu,Kwanza maisha yalianza vizuri kama tupo kwenye beach ya kimataifa vyakula vizuri,pesa nilizochangiwa,zilitosha Mimi kukaa mwezi mzima bila kujihusisha na kazi yeyote,fungate ilikuwa fungate kweli .
Na baada ya miezi minne ya ndoa yetu mke wangu kipenzi ilionekana ana ujauzito,hili lilinifurahisha sana pamoja na yeye mwenyewe alifurahi mno muda mwingi tuliangaliana na kutabasamu,licha ya ujauzito wake bado alifanya kazi Kwa bidii pamoja na kunionesha kunijali kama mume,nilipotoka kazini alinipokea Kwa shangwe,alinipa pole alinihurumia lakini niendapo kazini hakusita kunihusia kuwa makini.
Nilivimba nilijiona mwanaume mwenye bahati kana kwamba hakuna mwanaume mwingine aliwahi kuoa.
Hata baadhi ya washikaji walinionea wivu kimtindo hakika nilikuwa mfano wa kuigwa kama mtu anayeifaidi ndoa yake.lakini baada ya muda fulani mimba ilivyokuwa kubwa mke wangu alianza kubadilika, uvivu,kunijibu akijisikia,kutokuwajibika kwenye majukumu yake ndani ya familia pamoja na hujiamini,yaani ule uoga ulimtoka aliweza nijibu atakavyo.
anaweka kituo moses
Inaendelea........👇