Kutoa Taarifa NMB kwa Maslahi ya Umma

Kutoa Taarifa NMB kwa Maslahi ya Umma

NMB Tanzania

Official Account
Joined
Sep 13, 2014
Posts
94
Reaction score
232
Habari JF,

NMB inapenda kuwafahamisha njia tofauti za kutoa ripoti au taarifa inayohusiana na wizi, udanganyifu, hongo, rushwa na makosa ya mtandaoni( Kama kushirikisana password), kupeana kazi kwa kujuana na makosa mengine yanayohusiana na NMB

Toa taarifa kupitia Deloitte Tip Offs (Kwa Walio nje)

TTCL (Bure) No - 0808110088,
Ujumbe Mfupi +27 11 929 3413
Barua pepe: nmb@tip-offs.com.

Pia kwa kutembelea www.tip-offs.com


Unaweza kuripoti NMB moja kwa moja kwa utaratibu huu;

Piga simu namba;
0658 751 000
Tigo
0779 751 000 Zantel
0685 751 000 Airtel
0800 751 000 Vodacom

Au tembelea tovuti yetu: Home - NMB Bank Plc.

Kwa Wafanyakazi wa NMB: http://internalweb.nmbtz.com/Pages/Default.aspx

Barua pepe maalum: Whistleblowing@nmbtz.com

Pia unaweza kuandika barua kwenda:
Mkurugenzi Mkuu (Bahasha iandikwe "SIRI") NMB Makao Makuu, Sanduku la Barua 9213, DSM, Tanzania.
 
Master card zenu hovyo sana,mnatutesa sana
 
hongera kwa kuanzisha huduma za whistle blowing.......hakikisheni mnatunza siri
 
Hizo master Card tokea niuchukue sijawahi fanikiwa kutoa hela kwenye ATM. Mpaka niingie foleni ya ndani, hovyo sana kwa kweli
 
mnaongelea mambo ya kutoa taarifa sijui za wizi sijui password alafu matatizo ambayo ni current kama jipu la mastakadi sijui mmekaa kimya aiseeee
 
Hivi kwanini mnacost sana watu na master card zenu...
Na sijaona popote mkiomba msamaha kwa kero mlitusababishia wananchi[emoji32][emoji32][emoji32]

Sio ustaarabu..
 
Nipo katika hatua za mwisho kuwahama, Huduma mbovu

Sent From My Nokia Ya Tochi
Mnooooo...km swala la master card last week limeboa mnoo...watu mnapanga foleni kwa bank masaa...hela yangu nimeisotea mwezi mzima halafu nataka kuchukua wanaleta usumbufu...
 
halafu hawajibu issue ya MasterCard.. Local Banks ni majipu hakuna Cha NMB,CRDB au NMB . wote ni mizoga.. Nilihamia NMB nikitokea CRDB kwa Huduma mbovu...

Sasa na nyie naona ni wale wale kesho naenda kuchomoa sent zangu zote nahamia Exim Bank naona nyie Level yenu ni ya Vicoba

Sent From My Nokia Ya Tochi
 
Mnooooo...km swala la master card last week limeboa mnoo...watu mnapanga foleni kwa bank masaa...hela yangu nimeisotea mwezi mzima halafu nataka kuchukua wanaleta usumbufu...

Na kweli staff mate wangu bana hawa jamaa ni shida kabisa bora nirudi kwenye kadi za njano izi za mastercard ni majipu haswa usishangae na kesho zikagoma tena
 
Toka mwaka 2015 ninahangaika mnipe laki tano yangu mpaka leo ni danadana tu. Kila nikiikumbuka hii hela na muda niliotumia kuifuatilia nakosa imani kabisa na nyie. Mnawezaje kujitapa kuwa ni benki nzuri wakati tatizo lililopo ndani ya uwezo wenu mnashindwa kulitatua?
 
Back
Top Bottom