Kutoa lugha ya matusi kwa njia ya mtandao

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,439
858
Habarini waheshimiwa,
X alianza kutoa lugha za matusi kwa Y kupitia simu yake ya mkononi pasipo Y kutambua X ni nani,Y alimuonya juu ya matusi yake, baadae Y uvumilivu ulimshinda nayeye akatumia lugha ya matusi dhidi ya X na mwishowe Y akamuonya tena X kuwa hataki amutukane lakini aliendelea kumutukana na mwishowe Y akaenda polisi kushitaki mpelelezi wa kesi hiyo akadai Y afute kesi lasivyo wote washitakiwe kwa kutukanana,Y akajibu yeye alitukana baada ya X kuzidi kumtukana wakati alisha mkanya,kesi haiendi mahakamani.

Hapo mwongozo wenu nini kifanyike?
 
.................Mpelelezi wa kesi hakudai ila alifanya kutoa ushauri ili kupunguza msongamano wa wafungwa magerezani maana wote hapa mna makosa,mkishaenda mahakamani mnakuwa na mna-deal na jamuhuri na kisheria jamuhuri inamtambua mtenda kosa iwe alifanya kwa kukusudia au kumjibu aliyemtenda.
 
Kwa hiyo mtu akivamiwa na kujeruhiwa kisha nayeye akajitetea na kumjeruhi adui yake wote watafungwa au wataachiwa ilinkupuka msongamano wa gerezani?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom