Kutoa hela kwa boyfriend

Kutoa hela kwa boyfriend

Nina rafiki yangu ana kazi nzuri tu ila wameachana na boyfriend wake kisa kikubwa alimuomba hela kama mara mbili hivi na hajawahi kumpa sasa hii mara ya mwisho huyo kaka aliomba akopeshwe mil 1.5 alipe mwisho wa mwezi alipoambiwa kuwa haipo ndo akachange hadi kumuacha huyo rafiki yangu kuwa siyo supportive, je wanaume ni sawa kuwa unaomba mkopo kwa girlfriend kila mara? Na wadada ni sawa kweli kumpa boyfriend hela au kushare biashara nae?
mm mke wangu mtarajiwa mpaka boxer ananinunulia
 
sio lazima kumpa hela ata kama uyo bi dada anakazi nzuri uyo ni boyfriend/girlfriend yan unaazaje kushirikiana nae biashara au ujenzi??unajipenda au ndomana kasepa baada ya kuona hapewi hela doh, ni mume tu ndio wa kushirikiana nae kwa faida ya wanenu,na kama kamwacha kwa sababu iyo uyo sio mwanamme ni bonge la mario akakope benki,saccos nyambafu
 
Mimi mwenyewe kwa upande wangu sikubaliani na swala la kuanza kukopeshana na kushare biashara na mwanaume ambae siyo mume wako kila mtu afanye vtu vyake mwenyewe wanaume wengi cku hizi wanapenda sana mtelezo kuliko hata wadada

Acheni ubinafsi nyinyi, kuna wanawake wangapi wanao lipiwa kodi za nyumba, kununuliwa magari na hata kusomeshwa na ma boyfriend zao?
 
mwambie hasijaribu kutoa hiyo hela atakuja kujuta pesa hatorudishiwa ila Mme atapata mwingine mwanaume gani akurudishie hiyo pesa? tunasharega wapenzi bila kujua ila sio pesa aku sikupi hela yangu tho niko radhi kukupa zawadi sio pesa loh


umenichekesha jamani
 
Si sawa aiseee mwanaume kama sio mume wako si sawa kumpa hata kumi. Ni heri umnunulie vizawadi ila sio mara kwa mara. Unamnunulia hata baada ya miezi mitatu basi. Kumpa saport mtu ambae hujui future nae na kawaida wanaume wakiwa na girlfriend anaewapa hela basi anae anaemtunza so atachukua kwako atapeleka. Mwanaume anaheshim pale anapopahudumia hiyo Ni nature. Ukikazana kumpa jua Kuna anaetunzwa. Msaada Ni pale unaona anaugonjwa Au anatatizo kubwa ikibidi mwambie sina labda nikutafutie sehem utarudisha na akipata ahueni kaba sana arudishe.

unafaa kua mwalimu hela isiwe lazima halafu hii tabia boys kutaka hela kwa lazima kwa girlfriends zao wanajifunzia wapi?
 
Wanawake hawataki haki sawa ila wanataka usawa.
Kuna equity and equality
Equity ni kumpa mwanaume boxer na mwanamke chupi
Equality ni kuwapa wote boxer.

Hivyo duniani wanawake hawataki kitu kinachoitwa equality. Wanapenda kupendelewa.
Kama umeshakuwa na wanawake katika mahusiano ni karibia wote wana tabia zinazofanana. Mwanamke hapendi kutoa anapenda kuingiza..hahahaha kwa hiyo wanaume endeleeni kuwa hudumia tu. Hamna namna


haahhaaaa nimekuelewa sana,ila una wazimuuu😀
 
Binafsi kukopeshana ni sawa,
Nahofia kusema siyo sahihi kukopeshwa pesa kwa sababu hujui kabisa maisha ya wengine na wayapitiayo,
Lakini kitamaduni za kikwetu daah Msichana kumlipia au kumkopesha B/frnd cash ni aibu,
Mwisho siyo vizuri kukatisha mahusiano kwa mambo ambayo siyo sahihi....

wewe umenena kabisa,uanamme wa vijana wetu wa siku izi una walakini,mtu huumwi au hujapata shida nzito labda ajali msiba nk mwanamme unainuka uyooo eti uhusiano basi ukiulizwa girlfriend ana hela ila hajanikopesha/kunipa nna shida zangu,na ukute apo ata anachokitaka kufanyia iyo hela hujui...
 
Si sawa aiseee mwanaume kama sio mume wako si sawa kumpa hata kumi. Ni heri umnunulie vizawadi ila sio mara kwa mara. Unamnunulia hata baada ya miezi mitatu basi. Kumpa saport mtu ambae hujui future nae na kawaida wanaume wakiwa na girlfriend anaewapa hela basi anae anaemtunza so atachukua kwako atapeleka. Mwanaume anaheshim pale anapopahudumia hiyo Ni nature. Ukikazana kumpa jua Kuna anaetunzwa. Msaada Ni pale unaona anaugonjwa Au anatatizo kubwa ikibidi mwambie sina labda nikutafutie sehem utarudisha na akipata ahueni kaba sana arudishe.

Kumpa mwanamke asie mkeo wa ndoa ndio mnaona sawa...poleni.
 
Wazimuuu tena!
Eeeh hauna kakazi kazuri na mimi unikopeshemoo hata kalaki

nahudumia mme tu now na mme ndio unatakiwa kumsaidia mana ni mwenzio sasa,pole asee
 
nahudumia mme tu now na mme ndio unatakiwa kumsaidia mana ni mwenzio sasa,pole asee
Asante aseeh. Mume anapeleka kwa mchepuko. BTW mwambie rafiki yako wala siombi na kukopa pesa kwa KE..
 
Back
Top Bottom