Kutendwa kumenifanya nisijielewe

Kutendwa kumenifanya nisijielewe

Valentina

R I P
Joined
Oct 12, 2013
Posts
24,688
Reaction score
28,834
Wapendwa ni matumaini yangu mpo wazima na mko vizuri katika majukumu yenu

Leo ninaomba kushare nanyi jambo ambalo limekua likinitatiza kwa muda sasa. Ninatambua kila mmoja wetu ana historia yake ya kimapenzi na wengi tumetendwa na wale ambao tuliwekeza mioyo yetu kwao kwa kuwaamini kwamba wataiendeleza furaha yetu, ila kwasababu mbalimbali au kwa bahati mbaya wengi hatukuweza kufikia matarajio yetu juu ya hao wenzetu.

Binafsi nilikua katika mahusiano na mtu ambae nilimpenda mno narudia tena nilimpenda tena mno. Na ndie mwanaume wangu wa kwanza kukutana nae kimwili.

Naye kwa upande wake alionyesha uaminifu na moyo wakujali,maneno yote mazuri yenye matumaini mtoto wa kike niliambiwa, kifupi tulipanga uhusiano wetu uzae ndoa.

Ilifika hatua mwezi wa sita mwaka jana akaja Arusha kwalengo la kujitambulisha nyumbani kwetu. Lakini ghafla katika hali ambayo sikuitarajia akabadilisha maamuzi yake akanipa visingizio.

Baada ya muda mfupi kabla ya yeye kurejea kwenye makazi yake, nikamfumania akiwa na rafiki yangu wa karibu, rafiki niliye mchukulia kama ndugu yangu na kushare nae baadhi ya mambo.

Waliosalitiwa bila shaka wanaelewa uzito wa maumivu hayo. Ikabidi niwe mpole,na kuwaambia waendelee mbele,siku zilivosonga yule binti akaanza mambo ya dharau kwangu ila namshkuru Mungu nilipata moyo wa kumsamehe na kupuuza dharau zake.

Ilipofika mwezi wa 9 yule binti aliacha kazi kwa shari na kurudi kwao.

Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu leo, nikwamba yule mwanaume anataka kurudi kwangu na mimi moyo wangu unakua mzito kumrudia, nimetokea kumchukia.

Jambo linalonisumbua zaidi kila ninapoanza mahusiano mapya hua nashindwa kuendelea mbele, hofu ya kwamba huyu atanifanyia kama yule inanijia mara kwa mara na matokeo yake nakua sababu ya kuvunjika uhusiano huo.

Wapendwa nifanye nini kukabiliana na hali hii ya pili? Ninatamani sana hali hii iniondoke. Karibu kwa mchango wako kimawazo.
Kwenye makosa ya kiuandishi mnisamehe maana natumia simu.
 
^^
Kwanza, sikushauri urudiane na huyo mwanaume, katika maisha yangu nimejifunza kuwa wanaume wengi wanaowarudia wenzi wao si kwa nia ya kuimarisha mahusiano! Naongea hivi nikijifanya kipofu wa jinsi wanawake msivyo na misimamo (si ajabu mkarudiana)
Pili,
Jifunze kuishi maisha mapya! Mchezo wa kutofuatilia mahusiano mwanzo mpaka mwisho utakugharimu sana hasa kama mwanamke! Tazama magumu uliyopitia kama funzo la kumtunza na kulipwa hisani kwa uliyotendewa nyuma.
Usiifunge milango mipya mpaka itakapokupa sababu ya kufanya hivyo
Tatu
Simama imara! Huna haja ya kulia tena
^^
 
Aiseeeeeeeeeeeeee! Unatakiwa ukubali kwamba kusalitiana kupo, sio kwa watu wengine au kwenye filamu na maigizo ila kwa watu kama wewe na kwako inaweza kutokea kama ilivyotokea. Kutokana na nilivyokuelewa naomba ufanye yafuatayo;
1. Kubali kwamba huyo jamaa hakuwa chaguo lako na Mungu alikuepusha na mengi. Imagine mngeingia naye kwa ndoa halafu anatembea na rafiki yako. Kwa sababu hiyo jipange, ulishakubai matokeo so jirekebishe, kama unataka kuwa na mahusaino na mtu mwingine kubali kwamba binadamu tunatofautiana kwa hiyo sio kila mara na kila mtu atakusaliti...
2. Usikubali hata kidogo kurudiana na huyo mtu, never ever! Urafiki/Uchumba sio ndoa. Hata ingekuwa ni ndoa mtu aliykuacha nisingekushauri urudiane naye...ameona wangapi huko? Kwanini leo anarudi kwako?
Ni hayo tu ila tofauti na wengi watakaokuja hapa watakwambia uamuzi ni wako, mimi nakwambia USIKUBALI KURUDIANA NAYE
 
In short usikubali kurudiana nae maana tayari ameshaonesha hana upendo wa dhati kwako!
(ukimrudia usije kulalamika tena hapa)
halafu muombe Mungu akusaidie kwenye hali kama hiyo!
Kingine nafikiri ungesubiri kwanza moyo wako upone ndo uanze uhusiano mwingine!
 
Ušije ukathubutu kurudiana naye kama unataka usife kwa presha.

Mara ya kwanza kakucheat na rafiki yako.

Mara ya pili atakucheat na ndugu yako.

mara ya tatu atakucheat na dada yako.

Mara ya nne atakucheat na mwanao. Na listi itaendelea.

Jasiri huwa haachi asili. Niamini nakuapia.
 
Me kwanza nikupe pole maana nimejenga picha hiyo siku uliomfumania tena na rafiki yako, sijui nguvu zilikuishia vipi. Kwa ushauri, kurudiana nae wa mwanzo itakua si sahihi, utaonyesha udhaifu kidogo, kama hakuna umuhimu basi kua single ni bora zaidi kama kuna umuhimu basi chagua alie bora na muombe Mungu akusaidie
 
Wapendwa ni matumaini yangu mu wazima na mko vizuri katika majukumu yenu:

Leo ninaomba kushare nanyi jambo ambalo limekua likinitatiza kwa muda sasa. Ninatambua kila mmoja wetu ana historia yake ya kimapenzi na wengi tumetendwa na wale ambao tuliwekeza mioyo yetu kwao kwa kuwaamini kwamba wataiendeleza furaha yetu, ila kwasababu mbalimbali au kwa bahati mbaya wengi hatukuweza kufikia matarajio yetu juu ya hao wenzetu....

Binafsi nilikua katika mahusiano na mtu ambae nilimpenda mno narudia tena nilimpenda tena mno. Na ndie mwanaume wangu wa kwanza ku........
Nae kwa upande wake alionyesha uaminifu na moyo wakujali,maneno yote mazuri yenye matumaini mtoto wa kike niliambiwa,Kifupi tulipanga uhusiano wetu uzae ndoa.

Ilifika hatua mwezi wa sita mwaka jana akaja Arusha kwalengo la kujitambulisha nyumbani kwetu. Lakini gafla katika hali ambayo sikuitarajia akabadilisha maamuzi yake akanipa visingizio. Baada ya muda mfupi kabla ya yeye kurejea kwenye makazi yake,nikamfumania akiwa na rafiki yangu wa karibu,rafiki niliye mchukulia kama ndugu yangu na kushare nae baadhi ya mambo.

Waliosalitiwa bila shaka wanaelewa uzito wa maumivu hayo. Ikabidi niwe mpole,na kuwaambia waendelee mbele,siku zilivosonga yule binti akaanza mambo ya dharau kwangu ila namshkuru Mungu nilipata moyo wa kumsamehe na kupuuza dharau zake. Ilipofika mwezi wa 9 yule binti aliacha kazi kwa shari na kurudi kwao.
Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu leo,nikwamba yule mwanaume anataka kurudi kwangu na mimi moyo wangu unakua mzito kumrudia,nimetokea kumchukia.

Jambo linalonisumbua zaidi kila ninapoanza mahusiano mapya hua nashindwa kuendlea mbele,hofu ya kwamba huyu atanifanyia kama yule inanijia mara kwa mara na matokeo yake nakua sababu ya kuvunjika uhusiano huo.
Wapendwa nifanye nini kukabiliana na hali hii ya pili? Ninatamani sana hali hii iniondoke. Karibu kwa mchango wako kimawazo.
Kwenye makosa ya kiuandishi mnisamehe mana natumia cm.

Valentina, nadhani tatizo ni wewe mwenyewe. Lazima kwanza ubadilike na ukubali kua chenye mwanzo kina mwisho wake. Hiyo hivyo basi sio kila uhusiano utakao uanzisha utakuwepo mpaka kifo. Hata ndoa huwa zinavunjika! You must be realistic with life! mambo yakufikirika ya ache.

Sisi tumeoa wakezetu hawakuwa bikira! Jiulize walipitiwa na wanaume wangapi, waliachwa na wanaume wangapi mpaka kunifikia mimi?

unatakiwa uwe na malengo, kwamba nataka mahusiano kwamaana yamtu wakukupa raha. Kama ikitokea ndoa basi ni sawa. Ndoa itakuwa nimatokeo ya mahusiano yenu mazuri, na sio vinginevyo!

Wewe tafuta mwanaume kula raha kwanza mama.
 
Ušije ukathubutu kurudiana naye kama unataka usife kwa presha.

Mara ya kwanza kakucheat na rafiki yako.

Mara ya pili atakucheat na ndugu yako.

mara ya tatu atakucheat na dada yako.

Mara ya nne atakucheat na mwanao. Na listi itaendelea.

Jasiri huwa haachi asili. Niamini nakuapia.

Mmmmhh! hiyo orodha........! hahahaha
 
Wapendwa ni matumaini yangu mu wazima na mko vizuri katika majukumu yenu:

Leo ninaomba kushare nanyi jambo ambalo limekua likinitatiza kwa muda sasa. Ninatambua kila mmoja wetu ana historia yake ya kimapenzi na wengi tumetendwa na wale ambao tuliwekeza mioyo yetu kwao kwa kuwaamini kwamba wataiendeleza furaha yetu, ila kwasababu mbalimbali au kwa bahati mbaya wengi hatukuweza kufikia matarajio yetu juu ya hao wenzetu....

Binafsi nilikua katika mahusiano na mtu ambae nilimpenda mno narudia tena nilimpenda tena mno. Na ndie mwanaume wangu wa kwanza ku........
Nae kwa upande wake alionyesha uaminifu na moyo wakujali,maneno yote mazuri yenye matumaini mtoto wa kike niliambiwa,Kifupi tulipanga uhusiano wetu uzae ndoa.

Ilifika hatua mwezi wa sita mwaka jana akaja Arusha kwalengo la kujitambulisha nyumbani kwetu. Lakini gafla katika hali ambayo sikuitarajia akabadilisha maamuzi yake akanipa visingizio. Baada ya muda mfupi kabla ya yeye kurejea kwenye makazi yake,nikamfumania akiwa na rafiki yangu wa karibu,rafiki niliye mchukulia kama ndugu yangu na kushare nae baadhi ya mambo.

Waliosalitiwa bila shaka wanaelewa uzito wa maumivu hayo. Ikabidi niwe mpole,na kuwaambia waendelee mbele,siku zilivosonga yule binti akaanza mambo ya dharau kwangu ila namshkuru Mungu nilipata moyo wa kumsamehe na kupuuza dharau zake. Ilipofika mwezi wa 9 yule binti aliacha kazi kwa shari na kurudi kwao.
Sasa kilichonifanya nije hapa mbele yenu leo,nikwamba yule mwanaume anataka kurudi kwangu na mimi moyo wangu unakua mzito kumrudia,nimetokea kumchukia.

Jambo linalonisumbua zaidi kila ninapoanza mahusiano mapya hua nashindwa kuendlea mbele,hofu ya kwamba huyu atanifanyia kama yule inanijia mara kwa mara na matokeo yake nakua sababu ya kuvunjika uhusiano huo.
Wapendwa nifanye nini kukabiliana na hali hii ya pili? Ninatamani sana hali hii iniondoke. Karibu kwa mchango wako kimawazo.
Kwenye makosa ya kiuandishi mnisamehe mana natumia cm.
. Achana naye
 
Zungumza na nafsi yako, sikiliza sauti kutoka ndani inakwambia nn, then move on.
 
This sounds like some1 i know! Back to the topic, najua ni ngumu kutorudiana na huyo mwanaume ukichukulia ndiye aliyezichana chana nyavu zako(wanawake wengi huwa anafanya kufuatana na hisia bila kujali madhara.). Huwezi jua huko alikotoka kapatwa na nini na ana mawazo gani juu yako. Wengi huwa tunarudi kwa wale tulowaacha ili kupooza machungu tuloyapata huko tulikotoka. Muepuke huyo mwanaume lakini furaha yako ni ya muhimu zaidi!
 
pole kwa yaliyokusibu.
swali: je kuna nafsi inakuambia urudiane naye au hata moyoni mwako hayumo?

kuna dada mmoja alitendwa vibaya sana na bf wake. akawa karibu sana nami. akaniambia mabaya mengi ya huyo jamaa(ambaye nilisoma naye) na akawa ananiapia kuwa hatarudiana nae tena.

baada ya muda mfupu nikamsikia anasema mara "jamaa ameokoka nimekutana naye kwenye semina", mara kilikwenda kikarudi....hatimaye wakarudiana.

hata mwezi haukuisha jamaa akamtenda tena yule dada. hadi leo dada wa watu kachanganyikiwa mno. kila me kwake ni sumu.

anyway, fanya yafuatayo:
1. usimpe nafasi ya kuumiza moyo wako tena
2. msamehe ili ufungue ukrasa mpya na wengine(najua ni ngumu lakini usipofanya hivyo hutapata amani ya moyo na kwa hiyo utishi na mume bila imani naye.
3. njoo kwangu, sijawahi kupenda, naanzia kwako, sitakusaliti.....teh teh teh!
 
^^
Kwanza, sikushauri urudiane na huyo mwanaume, katika maisha yangu nimejifunza kuwa wanaume wengi wanaowarudia wenzi wao si kwa nia ya kuimarisha mahusiano! Naongea hivi nikijifanya kipofu wa jinsi wanawake msivyo na misimamo (si ajabu mkarudiana)
Pili,
Jifunze kuishi maisha mapya! Mchezo wa kutofuatilia mahusiano mwanzo mpaka mwisho utakugharimu sana hasa kama mwanamke! Tazama magumu uliyopitia kama funzo la kumtunza na kulipwa hisani kwa uliyotendewa nyuma.
Usiifunge milango mipya mpaka itakapokupa sababu ya kufanya hivyo
Tatu
Simama imara! Huna haja ya kulia tena
^^

Maneno yako yamenitia nguvu,nashkuru sana
 
Back
Top Bottom