Kutembea South Korea

Kutembea South Korea

Joined
Mar 11, 2014
Posts
78
Reaction score
6
Wakuu baada ya kuwa mpenzi wa kupitiliza kuhusu Drama za Korea, nmefikiria kwenda kutembelea south Korea ila Sina Idea yoyote ya huko...
Naombeni msaada wakuu najua humu ndani msaada tosha.

Najua humu ndani wako waliofika na wenye Idea kuhusu Korea... Asanteni sana kwa watakaonipa mchango wao.
 
kama unataka kwenda kutembea maisha ya huko hayakuhusu maana utafikia Hotel na kukaa siku unazo ziohitaji kisha unarudi zako bongo.Maisha yako juu naamanisha yako ghali si kama hapa nyumbuni.Japo nchi imeendelea sana tofauti na wengi tunavyodhani.Namna ya kwenda nenda ubalozi wao watakuelekeza jinsi ya kupata Visa yao.Kama unataka kwenda kutafuta maisha unahitaji maelezo zaidi.
 
Nliona you tube kuna Watu wanaelezea maisha ya huko hasa kwa mtu mweusi hebu jaribu kuangalia inaweza ikakupa mwanga kidogo
 
But mie siendi kuishi huko sister,
naenda kama kwa kutalii..
na kuhusu ubaguzi,i dont care kwa sababu hata hapa TZ upo!
 
kama unataka kwenda kutembea maisha ya huko hayakuhusu maana utafikia Hotel na kukaa siku unazo ziohitaji kisha unarudi zako bongo.Maisha yako juu naamanisha yako ghali si kama hapa nyumbuni.Japo nchi imeendelea sana tofauti na wengi tunavyodhani.Namna ya kwenda nenda ubalozi wao watakuelekeza jinsi ya kupata Visa yao.Kama unataka kwenda kutafuta maisha unahitaji maelezo zaidi.

asante mkuu,
Mie naenda kwa kutembea tu na kubadlisha mazingira..
mkuu unaweza kufunguka kama unaenda kutafuta maisha kukoje mazingira yake..
 
Wakuu baada ya kuwa mpenzi wa kupitiliza kuhusu Drama za Korea,nmefikiria kwenda kutembelea south Korea ila Sina Idea yoyote ya huko...
Naombeni msaada wakuu najua humu ndani msaada tosha...
Najua humu ndani wako waliofika na wenye Idea kuhusu Korea...
Asanteni sana kwa watakaonipa mchango wao 🙂

Sio kubaya mkuu,unaweza tu kwenda.Mimi sipo Korea, nipo nchi nyingine lkn kutokea hapa nilipo nishaenda holiday mara 2.Ni watu waliopiga hatua kwenye maisha na technology kwa ujumla.
 
Kumbe wewe ni dramaw addict wa Korean drama eee, aisee hao watu na wakubali sana, siku hizi huwa si watch drama zingine zaidi ya za kwao especially historical koren drama
 
Wakuu baada ya kuwa mpenzi wa kupitiliza kuhusu Drama za Korea,nmefikiria kwenda kutembelea south Korea ila Sina Idea yoyote ya huko...
Naombeni msaada wakuu najua humu ndani msaada tosha...
Najua humu ndani wako waliofika na wenye Idea kuhusu Korea...
Asanteni sana kwa watakaonipa mchango wao 🙂

Wazo zuri kutembelea Korea..nitarudi nikupe reliable information zaidi. Je, unapanga kutembelea huko wakati gani?pia, solo traveller ama?
 
Sio kubaya mkuu,unaweza tu kwenda.Mimi sipo Korea, nipo nchi nyingine lkn kutokea hapa nilipo nishaenda holiday mara 2.Ni watu waliopiga hatua kwenye maisha na technology kwa ujumla.

mkuu asante sana,
vp kuhusu bei za hoteli,vyakula na mazingira ya huko?
nawakubali sana hawa jamaa.
 
Bei za hotel sina uhakika sana. Mimi nilipitia kwa agent safari yangu. Yaani nililipa dolla 350hivi, hii ilijumuisha ticket ya ndege kwenda na kurudi na hotel siku 3, chakula unajitegemea.Mazingira mazuri, vyakula mi nilikuwa napendelea kula nyama ya kuchoma ya Ng'ombe, wanaweka vitu gani sijui kwenye nyama inakuwa laini na test nzuri sana mdomoni.Kuzuri mkuu, kwa ujumla jamaa sio Maskini na naamini hutajutia safari yako.
 
Wakuu baada ya kuwa mpenzi wa kupitiliza kuhusu Drama za Korea, nmefikiria kwenda kutembelea south Korea ila Sina Idea yoyote ya huko...
Naombeni msaada wakuu najua humu ndani msaada tosha.

Najua humu ndani wako waliofika na wenye Idea kuhusu Korea... Asanteni sana kwa watakaonipa mchango wao.

Internet imejaa info zote kama unataka kusafiri kwenda huko.

A: Plan gharama na namna ya safari
1. Anza ku-google masharti ya kupata visa zao za utalii na sehemu ya karibu unaweza ku-apply
2. Ingia kwenye sites za mashirika ya ndege yanayokuja Bongo kama Emirates ect uone ticket itagharimu kiasi gani
3. Google ''cheap hotels in South Korea'' na utapata listi za hotels zisizo na idadi.

B: Fanyia kazi plan yako
Ukishakusanya data sasa nenda sehemu uliyoona unaweza ku-apply visa ili u-submit application yako na kutekeleza mengine
 
Mkuu asante,
ndege nafuu ya kwenda huko ni Qatar Airways..
nafanyia ushauri wako uliobakia..
 
Bei za hotel sina uhakika sana. Mimi nilipitia kwa agent safari yangu. Yaani nililipa dolla 350hivi, hii ilijumuisha ticket ya ndege kwenda na kurudi na hotel siku 3, chakula unajitegemea.Mazingira mazuri, vyakula mi nilikuwa napendelea kula nyama ya kuchoma ya Ng'ombe, wanaweka vitu gani sijui kwenye nyama inakuwa laini na test nzuri sana mdomoni.Kuzuri mkuu, kwa ujumla jamaa sio Maskini na naamini hutajutia safari yako.

Mkuu package kama hio bongo hamna,rahisi sana..
 
Nimewahi kwenda huko Korea ni pazuri sana shida kubwa unayotakiwa kufanya maombi ni ndege isije kuzama baharini jumla jumla,,,,
 
Back
Top Bottom