Anatuma kwanza pesa unahakikisha imeingia ndio unakabidhi mzigo Bro.Ingekua ngumu kweli kwangu mimi. Ila vp kwa upande wako, Wewe ungeweza kumuamini mtu ambae hujawahi kuonana nae akutumie pesa kesho bro? Na mzigo tayari umekabidhi ndugu yangu
N
Kila la kheri... Ila amini katika hili, lililo pangwa liwe lako utalipata na kama hukupangiwa basi mshukuru Mungu na amini utapata zaidi ya kile ulichopoteza... Good luck
hivi siku hizi kuna kusema nataka nikutumie mtandao fulani? hela toka NMB haiangalii mtandao. ila kama wameweza kusave NMB. kwenye cm hao ni ma PRO.
labda kama rafik yake kampiga,ila ingeonekana walipoenda NMB kama hela iliingia(miamala). Au jamaa alituma halaf akarudisha muamala(pia nayo ineonekana NMB)Kabsa aiseee, au rafiki yake nae kafanya maujanja?
Mkuu wewe ndie umekuja na majibu sahihi, hapa ndipo mdau kapigiwa. Nampa pole sanaAme edit meseji ya benki akaongeza tarakimu!!huu mchezo tumechezeana sana kwenye upatu na washkaji zangu !!!
Hili la kusema ''jambo lililopangwa''au ''kama riziki haikuwa riziki haikuwa riziki'' au ''tushukuru kwa kila jambo'' ni misemo ya kijinga sana na haina nafasi kwenye karne ya leo. Hivi wewe unafikiri kuna kiumbe kilipanga utapeliwe? Umetapeliwa kwa sababu hukuwa makini. Wewe ulipatana kumuuzia hiyo bidhaa na yeye akulipe meseji au fedha? Inakuwaje unampa bidhaa baada ya kuona meseji na siyo fedha? Kama ilikuwa ni jioni basi ungemwambia mauziano yafanyike kesho yake na wewe ukishahakikisha fedha imeingia kwako ndiyo unampa bidhaa. Duniani kote wanakofanya biashara kwa njia ya mtandao huwa wanapeleka bidhaa baada ya kuhakikisha fedha zimeingia kwenye account zao na siyo meseji.Asante kwa kunipa moyo ndugu. Kama ipo ipo, na kama haikua riziki.... basi yote kheri. Tunashukuru kwa kila jambo.
Hili la kusema ''jambo lililopangwa''au ''kama riziki haikuwa riziki haikuwa riziki'' au ''tushukuru kwa kila jambo'' ni misemo ya kijinga sana na haina nafasi kwenye karne ya leo. Hivi wewe unafikiri kuna kiumbe kilipanga utapeliwe? Umetapeliwa kwa sababu hukuwa makini. Wewe ulipatana kumuuzia hiyo bidhaa na yeye akulipe meseji au fedha? Inakuwaje unampa bidhaa baada ya kuona meseji na siyo fedha? Kama ilikuwa ni jioni basi ungemwambia mauziano yafanyike kesho yake na wewe ukishahakikisha fedha imeingia kwako ndiyo unampa bidhaa. Duniani kote wanakofanya biashara kwa njia ya mtandao huwa wanapeleka bidhaa baada ya kuhakikisha fedha zimeingia kwenye account zao na siyo meseji.
Ni jambo zuri kama utafuatilia kuliko kusema ''haikuwa riziki'' na kukata tamaa. Ila hata huko polisi uwe makini usije ukapoteza fedha zaidi na usipate chochote. Hawa matapeli wanakuwa wamejipanga sana na hizo namba wanazotumia nyingi zinakuwa na usajili fake. Usikubali kuwapa polisi fedha kiasi kikubwa. Na zaidi usikubali kwenda mganga wa kienyeji yeyote kama watu wanavyokushauri kwani huko nako ni matapeli tu.Ndo ishakua hivo sasa...nifanye tu utaratibu wa kusaka polisi. Thats the only option ilobakia
Polisi kitengo Cha cyber crime watakusaidia report mkuuAsante ndugu... masaa mawili sasa yamepita tangu anambie anawasiliana na wakala. Ila kwa sasa hv hapokei simu zangu
Hili la kusema ''jambo lililopangwa''au ''kama riziki haikuwa riziki haikuwa riziki'' au ''tushukuru kwa kila jambo'' ni misemo ya kijinga sana na haina nafasi kwenye karne ya leo. Hivi wewe unafikiri kuna kiumbe kilipanga utapeliwe? Umetapeliwa kwa sababu hukuwa makini. Wewe ulipatana kumuuzia hiyo bidhaa na yeye akulipe meseji au fedha? Inakuwaje unampa bidhaa baada ya kuona meseji na siyo fedha? Kama ilikuwa ni jioni basi ungemwambia mauziano yafanyike kesho yake na wewe ukishahakikisha fedha imeingia kwako ndiyo unampa bidhaa. Duniani kote wanakofanya biashara kwa njia ya mtandao huwa wanapeleka bidhaa baada ya kuhakikisha fedha zimeingia kwenye account zao na siyo meseji.
[/QUOTE/]
Ulichoandika ndo nilitaka andika nikaona nikae kimya...ndo maana hatusongi mbele..eti haikua riziki..hahhaaa..hakuandikiwa..jamani Mungu naye tunamchoshaaa!
Hili la fedha kukataa kutoka na ikatoka risiti tu tena imeandikwa kuwa umetowa fedha huwa linatokea mara kwa mara. Hata mimi lilishanipata. Mwanzoni nilichanganyikiwa ila nilipoulizia benki wakanimbia kama fedha hazikutoka basi nisubiri kesho yake nione kama zimepungua kwenye account yangu. Mimi nilicheki muda ule ule na nikakuta hazijapungua. Limeshanipata kama mara tatu na muda wote fedha hazikupungua kwenye account yangu.Lakini Kuna Jambo nimekumbuka wiki mbili zilizopita nikiwa foleni NMB IRINGA aliingia Dada mmoja kutia hell ATM akafanya transaction akiomba na risit pesa haikutoka, ikatoka risit tu..ilikua saa moja jioni Dada wawatu akadata hataki kutoka kwenye mashine Hadi hela itoke...nikamuuliza km kwenye rist salio limepunguzwa jibu likawa nindio! Kuna muda huduma za bank zetu nazo nitatizo, je kwa wakala Hali ikoje? Sijawahi kuweka hell ndefu kwa wakala...yule Dada sijui walimalizana VP na mlinzi asiejua lolote kuhusu banking!
Polee we,na karibu ndani ya club ya wahanga wa MITANDAONI. Juzi nilileta uzi wa kujinjwa pesa kupitia tigo pesa wachangiaji wakaninanga saana. Jàmani haya mambo yanaweza kukutokea ukabaki unashangaa hasa baada ya kuibiwa. Pole tena Jamaa yangu.Asante ndugu, Na mimi pia ndo wasiwasi wangu ukianzia hapo. Nilijaribu kuangalia hata message za tigo pesa ila sikuona hiyo nukta kwa mbele. Ikaniongezea mashaka zaidi
Mkuu pole sana umeshapigwa hela hapo,daah nilipigwa lake 3,nikaona nyingi kwa mtindo huo kumbe kuna watu wanapigwa mpk milioni.kua makini siku nyingine mkuu. Matapeli mjini ni wengi na husiamini mtu siku hiziWakuu habari yenu, jana kuna kitu nlimuuzia jamaa fulani hv. Yeye alisema yuko mkoani, so ikabidi tufanye arrangements ili tukutane na ndugu yake alieko Dar uko, ili nimpe mzigo wake.
Baada ya yule ndugu yake kuuona na kuridhika, ikabidi ampigie mteja wangu kwamba mzigo uko vizuri. Nikawa nimeongea nae akasema atanitumia kwenye number ya airtel iko kiasi tulichokua tumekubaliana. Kwa kua mimi sina number ya airtel ikabidi nimwambie rafiki yangu kuwa kuna muamala utatumiwa kwenye simu yake maana yeye ana line ya airtel.
Basi, kama baada ya dakika nane yule rafiki yangu anaetumia line ya Airtel akanambia ameona pesa imeingia kutokea NMB. Mimi nikasema sawa, nikamkabidhi yule ndugu yake mzigo tukaachama pale.
Ile message inaonekana imetokea NMB, kwamba katumia huduma ile ya benki mkononi kunitumia hela. Basi, kwa kua ilikua ni jioni sana hata mabenki yalikua yamefungwa nikasema asubuhi ya leo nitawahi bank nikaihangaikie. Cha ajabu nafika bank wananiambia hakuna muamala wa dzain hiyo kwa benki yao. Sikukata tamaa ikabidi niwacheki pia kwa mitandao yao ya kijamii (instagram) ila majibu yakawa ni yale yale.
Mteja wangu nliefanya naye biashara, wakati niko bank nilikuwa najaribu kumpigia ila hakupatikana, ila dakika 20 kabla ya kuanza kuandika huu uzi nlijaribu kumpigia akasema ngoja amcheki wakala ambae alimtumia kunitumia hiyo hela. Ndo niko namskilizia hapa.
Naombeni ushauri kama kuna mtu anaweza kuwa na idea na hiki kitu au anaeweza kuwa na wazo lingine anisaidie wakubwa.
Natanguliza shukrani.
View attachment 1488552View attachment 1488553
Hapa sasa ndo nimeelewa..Mkuu pole hapo umepigwa. Wametumia bulk SMS na kwenye jina la sender wameweka (NMB.)
Next time hakikisha salio linasoma ndo utoe bidhaa. Yaani kufanya hivyo naandika script ya mistari michache sana ya Python + Bulk SMS API yoyote faster kitu kinatumwa
Vibaka sio watu wazuri..Pole sanaDah mkuu mimi jana nimefua suruali tatu nikaanika kama saa tatu usiku, nikalala maana hazikuwa zimekauka, nimeamka asubuhi hazipo, nimekuwa na uchungu mkali kwa suruali tu, sasa nakufikiria wewe, dah! Mtafute huyo ndugu yake uliyempa mzigo ule naye sahani, OVA