Kutana na mlemavu wa kusikia Mtanzania aliyeikubali hali yake

Wangari Maathai

JF-Expert Member
Aug 13, 2018
34,962
70,488

Anaitwa James Fransic William,

Ni kijana aliyezaliwa kwenye familia ya watoto watatu yeye akiwa wapili kuzaliwa...akifanyia shughuli zake Kenya.

Tatizo lake la usikivu alilipata akiwa ana miezi 9 tu ...aligundulika ana malaria na amoeba...dk akampa Quinine ndo ikapelekea ulemavu wa kusikia.

Wazazi wake hawakumvunja moyo walimpenda na kumsisitiza kusoma na kufanya anachopenda...
Anasema anapenda kulala na kupiga picha.

James anasema anaingiza $400kwa siku. Wazazi wenye watoto wenye ulemavu msiwatenge watoto wapendeni na wabidisheni kusoma na wafanye wanachopenda!

Kuongezea tu James hana mpenzi😊!

Rip Mpauko!...
 
For the first time, ngoja nichangie neno hapa.

KUKATA tamaa ni jambo la kawaida kwa wanadamu wote, angalau kwa kiasi fulani. Hata hivyo, kwa wengine, hali ya kukata tamaa huwa mbaya sana hivi kwamba inakuwa afadhali kufa kuliko kuishi.

Huenda watu fulani leo wakakata tamaa kwa sababu ya athari zenye kuumiza za uzee, kifo cha mwenzi wa ndoa, au magumu ya kifedha. Wengine huona kwamba mkazo wa daima, kuendelea kukumbuka mambo yenye kuvuruga, au matatizo ya familia huwafanya wahisi kana kwamba wanatatanika katikati ya bahari, kila wimbi likifanya iwe vigumu zaidi kufika ukingoni. Mtu mmoja alisema: “Unahisi hufai kabisa kana kwamba hakuna mtu atakayekukumbuka ukifa".

Tutanufaika tukisema mambo waziwazi katika sala zetu. Ingawa huenda ikawa vigumu kueleza mawazo yetu, twapaswa kuwa huru kuzungumza na Yehova kuhusu jinsi tunavyohisi na kile tunachoona kuwa kiini cha tatizo. Twahitaji kumwomba nguvu ya kututegemeza kila siku. Tuna uhakikisho huu:

“Atawafanyia wamchao matakwa yao, naye atasikia kilio chao na kuwaokoa.”— Zaburi 145:19 .
Mbali na kusali, twapaswa kuepuka kujitenga na wengine. ( Mithali 18:1 ) Wengine wamepata nguvu kwa kutumia wakati na nguvu zao kusaidia wengine. ( Mithali 19:17; Luka 6:38 )
 
SIRI ya maisha yetu anaijua muumba,kuna walemavu wa viungo mbalimbali lakini wanamaisha wanaishi vizuri tu....kila anachofanya kina Kubali.
Sasa upande mwingine kuna watu wanaviungo kamili si walemavu lakini wanasota kila siku ni tabu za kufa mtu.

Kuwa mlemavu siyo sababu ya kukata tamaa ya maisha na kuamua kujitoa uhai au familia kumtenga mlemavu na kumuona hafai hii ni hatari sana kwa ustawi wa maisha ya mlengwa.

Ujumbe.
Tusikate tamaa... maisha ndiyo Haya haya kujiua ni dhambi kubwa sana wengi wetu tuna maisha magumu sana kama jiwe tupeane faraja, na tusaidiane kwa ushauri na chochote kidogo au kikubwa ndiyo ubinaadamu.
 
Dah hii kesi kama yangu kabisa.

Kwa kweli Aliyegundua hizi dawa za quinine, amegharimu usikivu wa watoto wengi sana.

Quinine na Chloroquine zinaweza sababisha "ototoxicity" Kama ulivuka salama kipindi cha matumizi ya hizi dawa kama tiba ya malaria kwa kweli shukuru sana Mungu.

Pole sana..wifi yangu amekuja pata ulemavu wa kusikia akiwa amezaa last born...mpk leo hasikii...inaumiza sana jamani
 
Ndugu yañgu angepata nafasi kama aliyepata huyu (family background) asingewai kwenda na pia huyu angepata nafasi kama ya nduguyangu uwenda ndio angewai kwenda mapema kabisa.

FAMILY BACKGROUND... Economy, Support, Connection, Network, Love n Care....But Always am lying on Economic Background.

Portfolio | 2020
 
Uko sahihi.
 
SIRI ya maisha yetu anaijua muumba,kuna walemavu wa viungo mbalimbali lakini wanamaisha wanaishi vizuri tu....kila anachofanya kina Kubali.
Sasa upande mwingine kuna watu wanaviungo kamili si walemavu lakini wanasota kila siku ni tabu za kufa mtu.

Kuwa mlemavu siyo sababu ya kukata tamaa ya maisha na kuamua kujitoa uhai au familia kumtenga mlemavu na kumuona hafai hii ni hatari sana kwa ustawi wa maisha ya mlengwa.

Ujumbe.
Tusikate tamaa... maisha ndiyo Haya haya kujiua ni dhambi kubwa sana wengi wetu tuna maisha magumu sana kama jiwe tupeane faraja, na tusaidiane kwa ushauri na chochote kidogo au kikubwa ndiyo ubinaadamu.
Sa unafika wakati hata mwanao anakuona hufai,,ufanye nini sasa ama unaona kabisa kila kitu huna(hata uhuru) basi unaupumzisha mwili wako!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom