Kustaafu kwa Prof. Assad (CAG) na misimamo yake

asiyetabirika

Member
Oct 14, 2019
46
55
Yaani kupitia kauli zake na hoja zake kunaonesha hali fulani ya kujiamini, yaani tokea akiwa madarakani hata baada ya kutenguliwa nimemsikia akisema hajapewa barua ya termination.

Tofauti na matarajio kuwa angekaa kimya na kutafakari uelekeo mpya hasa baada ya kibarua chake kukoma, bado misimamo yake inaendelea na anaonyesha hali ya kujiamini kana kwamba hajali chohote na kwake ni kama ni tukio alilolitarajia kabla.

Hivi huyu Prof. ni mtu wa aina gani?, Je, anaringia elimu yake kuwa ataenda mamtoni kuitumia elimu yake kwenye taasisi za mabeberu, au anaongea kuisimamia haki?

Au tuseme ni kiburi cha kitaaluma tu anatakiwa apuuzwe?
IMG-20191104-WA0002.jpeg
 
Hana lolote ni kibaraka tu. Aliaminishwa na vibaraka wenzake kwamba hatafanywa lolote. Sio lazima upewe barua ya kufukuzwa kazi wakati mkataba wa kuajiriwa unao. Amuulize Zito Kabwe mshiriki mwenza.
 
Hivi kibaraka ni nini ? huenda wanaoita wenzao vibaraka ndio vibaraka.., hakuna mtu mwenye hati miliki ya hii nchi, kwamba anachosema ndio sawa na wengine kila wanachofanya sio sawa sababu eti tu inatofautiana na yeye
 
Hana lolote ni kibaraka tu. Aliaminishwa na vibaraka wenzake kwamba hatafanywa lolote. Sio lazima upewe barua ya kufukuzwa kazi wakati mkataba wa kuajiriwa unao. Amuulize Zito Kabwe mshiriki mwenza.
Wewe kibaraka mkubwa wa fisadi mkuu asiytaka kukaguliwa
 
Yaani kupitia kauli zake na hoja zake kunaonesha hali fulani ya kujiamini, yaani tokea akiwa madarakani hata baada ya kutenguliwa nimemsikia akisema hajapewa barua ya termination.

Tofauti na matarajio kuwa angekaa kimya na kutafakari uelekeo mpya hasa baada ya kibarua chake kukoma, bado misimamo yake inaendelea na anaonyesha hali ya kujiamini kana kwamba hajali chohote na kwake ni kama ni tukio alilolitarajia kabla.

Hivi huyu Prof. ni mtu wa aina gani?, Je, anaringia elimu yake kuwa ataenda mamtoni kuitumia elimu yake kwenye taasisi za mabeberu, au anaongea kuisimamia haki?

Au tuseme ni kiburi cha kitaaluma tu anatakiwa apuuzwe?View attachment 1254064
kuna watu wanaanza kumtizama huyu bwana
Kama mtaji wa kisiasa ,,soon watamuomba agombee uraisi nawajua💨💨
 
Kibaraka gani na kaiba kitu gani? Au amekuwa kibaraka baada ya ripoti yake kuonyesha 1.5 tillion hazionekani zimefanya nini?
Hana lolote ni kibaraka tu. Aliaminishwa na vibaraka wenzake kwamba hatafanywa lolote. Sio lazima upewe barua ya kufukuzwa kazi wakati mkataba wa kuajiriwa unao. Amuulize Zito Kabwe mshiriki mwenza.
 
Siku zote ukweli hudumu milele tofauti na uongo ambao huishi miongo michache.
Tutajaribu kuuficha ukweli leo ila kesho ukweli huo huo utajulikana.

Pembe la ng'ombe kamwe halijifichi na huwa naamini kwamba kichaa halazimishwi kuokota makopo.
 
Viongozi wengi wamesingiziwa kustaafu kabla ya muda ikiwemo RAS wa Morogoro hivi karibuni lakin huyu prof kakataa unafiki
 
Prezidaa ameonyesha wazi kwamba jamaa alimkera sana ndio maana ametoa kauli za kumponda profesa assad wakati akimuapisha CAG mpyaaa wa TRA
 
Duhhh....
Hivi kusema ukweli na kusimamia kile anacho kiamini, tayari mshabadili na kupata tafasiri zenu kama mnavyo taka wenyewe....!!??
 
Ulikuwa ma point ila ulipotumia tu jina beberu umeshanichefua. Waafrica sijui mkoje. Nyie ndyo mpo inferior mnaogopa kubaguliwa ila ndyo wakwanza kuita wenzenu mabeberu. Hivi bila hawa mabeberu hii post uliyoandika bila simu walizovumbua wao, ungetumia nini? Na unaweza kuta hapo ulipo umevaa nguo za mtumba kutoka kwa mabeberu.
 
Back
Top Bottom