Kusoma China

Kusoma China

mohame kholani

Senior Member
Joined
Jan 1, 2018
Posts
145
Reaction score
103
Habari wapendwa.

Naulizia kusoma course za Masters nchini China za business, Je ukirudi hapa Tanzania ajira zake zipoje na kozi zipi hasa hasa za business zina soko?

Naomba mwongozo na ushauri zaidi.
 
Kaka mi nakushauri usiende kusoma nenda kaibe ujuzi wa kijasiliamali, arrange 6 weeks trip, ukifika jibane tembelea viwanda vyao vidogovidogo tembelea technology exhibition zao, hiyo pesa badala ya kulipia ada itumie kununulia mashine za bei rahisi uje ufungue simple industry hapa nyumbani

Kwa mfano unaweza ukanunua mashine simple za kufyatua misumari kea around $500 ukaja kuanzisha simple nail industry hapa home, au mashine za kushonea mitindo mbalimbali ya nguo, au simple mashine za kufanya plastic moulding ukaja kuanzisha kiwanda kidogo cha kuunda chupa za plastic....

Hii itakusaidia kutokupoteza muda kukereka na akusubiria ajira na kuwa na kipato chako mwenyewe cha uhakika.
 
Kizzy Wizzy,

Ahaaaa sawa bro ipo hivi, kuna jamaa wanatoa full scholarship ila kuna kitu unalipia kwa agent Tsh. 2 million then unaenda huko sio kama mimi mwenyewe ndio naenda kujisomesha mwamba hapana.

Sina hata hiyo nauli ila kuna mtu anataka kunipa ufadhili wa kusoma huko maana nimeshakaa mtaani miaka 3 bila ajira ya kudumu zaidi ya intern tu.
 
Watu wengi asilimia 90 wanaoenda soma nje ya nchi ni kwenye vyuo visivyoeleweka ni vilaza
 
Habari wapendwa.

Naulizia kusoma course za Masters nchini China za business, Je ukirudi hapa Tanzania ajira zake zipoje na kozi zipi hasa hasa za business zina soko?

Naomba mwongozo na ushauri zaidi.
Yaani unasoma kozi za Masters !

Tena zinazohusu mambo ya Business!

Halafu Ukirudi Unatafuta Ajira.
 
Ahaaaa sawa bro ipo hivi, kuna jamaa wanatoa full scholarship ila kuna kitu unalipia kwa agent Tsh. 2 million then unaenda huko sio kama mimi mwenyewe ndio naenda kujisomesha mwamba hapana.
Agent wa aina hii nitakaa nae mbali sana. Kuna gharama wanaingia lakini kwa millioni 2 hapana. Sidhani kama Global wanachaji hata nusu ya hizo.
Kwa bei hii nitakomaa na website za vyuo.
 
Agent wa aina hii nitakaa nae mbali sana. Kuna gharama wanaingia lakini kwa millioni 2 hapana. Sidhani kama Global wanachaji hata nusu ya hizo.
Kwa bei hii nitakomaa na website za vyuo.

Sasa hapo unasoma miaka yotee kuanzia mwaka mmoja wa lugha mpaka miaka ya kozi utakayo maliza hiyo 2million ndogo au??
 
Back
Top Bottom